Mkuu shirki kutokana na imani yangu, imegawika sehemu 4!
Nikihusisha shirki na hayo mambo ya nyota, ni wazi kuwa nyota ni moja kati ya shirki!
Nimeona hapo juu umemjibu mdau amtafute elimu, nikaona tena umesema hata wachungaji waliifata nyota ya Yesu hadi walimfikia!
Upande wa pili huku, temeambiwa tutafute elimu hata china! Elimu yeyote inaruhusika kusomwa na kutumika! Ispokuwa itumike kwa mambo mema, either kwa kusaidia watu!
Tupaache hapo!
Na kunakitu ningependa nijue:
Kama nyota zinaukweli ndani yake, kwanini imekatazwa kufatilia?
Natambua wenzetu (wazungu na wachina) hutumia nyota kuangalia vipaji vyao na kudetermine nini wafanye ili wapate maendeleo!
Na kunabaadhi ya watu (wanandoa) hutegea hata miezi ya kupeana mimba ili mtoto wao azaliwe ktk nyota wanayoitaka wao na kwa kuamini mtoto atakuwa vile wapendavyo!
Jee unaliongeleaje hilo?
...
Na pia niliskia na watu wazima kwamba kunasiku (tarehe/mwezi na mwezi/mfunguo) fulani ndani ya mzunguko wa mwaka, ukioa ndani ya siku hizo, ndoa yako haitadumu! Wakati kuna baadhi ya siku ukioa ndoa inakuwa imara!
Jee ulishawahi kuskia hilo?
Kama umewahi, kwanini iko hivyo?
Binafsi haya mambo yananichanganya sana, ningependa nitambue kuna nini nyuma ya pazia! Kwa nini iwe hivyo?
Cc:
MziziMkavu!