Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Status
Not open for further replies.
Well said MziziMkavu!
Kwa vile hapa tupo Jamii intelligence watuache tupumue!

Mimi napenda kufaham kuna nini nyuma ya pazia. Hasa apo kwenye kutiming tarehe ili kufanya tukio!
Kwanini hizo siku nyengine ziwe mzuri na hizo nyengine ziwe mbaya kwa kufanya tukio? Ni nini kinasababisha hilo?
Kwa kutolea mfano nipe wewe tarehe yako ya kuzaliwa na mwezi uliozaliwa nitakupa Data zote. Tarehe ya kuzaliwa na mwezi na mwaka ndio inakupa wewe Maisha yako yote jinsi yatakavyo kuwa na mwisho wa maisha yako yatakuwaje. tunaweza kusema kwa lugha ya kiingereza taehe yako na mwezi na mwaka wako wa kuzaliwa vinakupa (future of your life) chanzo. Mzizi Mkavu
 
89/25/07!
 
89/25/07!

Kutokana na wewe kuzaliwa mwaka 25/07/1989. Mwaka utakao fanikiwa kupata kipesa na

maisha yako yatakuwa ni mazuri ni mwaka 2016 ukifika mwaka huo kama utakuwa bado upo

hai basi ukae ukijuwa ndio mwaka wako wa mafanikio kipesa kwa hali yoyote ile ile. Utakuja

kunikumbuka ukifika huo mwaka kam mimi MziziMkavu nimekwambia maneno ya ukweli fanya

kuwa siri yako usimwambie mtuı tafadhali. Soma Maelezo ya nyota yako hapo chini kwa kirefu.

NYOTA YA SIMBA (LEO)

  • Hii ni nyota ya tano katika mlolongo wa nyota kumi na mbili.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21Julai na 21 Agosti.
  • Sayari yao ni Jua (Sun).
  • Siku yao ya bahati ni Jumapili.
  • Namba yao ya bahati ni 1 na 4.
  • Rangi yao ya bahati ni Njano au rangi ya Dhahabu.
  • Asili ya nyota yao ni moto.

KIPAJI CHA SIMBA (INSPIRED):

Wenye nyota hii wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.
Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi.

TABIA ZA SIMBA:

Watu wenye nyota hii ya Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Ni watu wanaopenda kutumia na wanataka waonekane na wanuwezo wa kuvumbua mambo amabyo watu wengine hawajui na wanapenda sana heshima.
ni wakarimu lakini ni wajeuri na wanapenda kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.

TABIA YA SIMBA KATIKA MAPENZI:

Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.

Furaha haina mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.
Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.
Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.
Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.
Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.
Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.
{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA SIMBA:

Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.
Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.
Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.
Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

FAMILIA ZA SIMBA:

Kwa asili Simba ni Mfalme na mamlaka yake yamezungukwa na hisia za kifalme. Wazazi wa simba huwa wana mila ya kuwapangia watoto wao namna watakavyoishi kwa sababu wanajivunia sana familia zao.
Wazazi wa Simba wanajiona kwamba wana nafasi kubwa katika dunia ambayo inawataka wajionyeshe kwa watu ubora. Pamoja na kwamba wenye nyota hii hupenda kuzunguka na watoto wao (na wao wenyewe wakati mwingine wana tabia ya utoto) hawakubali kupoteza heshima zao wakati wanafanya hivyo.
Wenye nyota hii ni wachangamfu, wenye moyo wa kupenda na wanapenda raha, pamoja na ukali wao wanaweza kuwa wepesi kwa watoto wao.
Watu wa simba kwa uhakika wanaona raha kuwa wazazi lakini wanatakiwa wawe makini kutowaharibu watoto wao kwa zawadi nyingi na maisha ya raha.
Simba wana uhakika na nafasi yao katika jamii kwamba wao ni viongozi hivyo watoto wao huwa wanapenda kujionyesha na wanategemea wawe wanaonekana kwa watu muda wote.

MADINI YA SIMBA:

(AMBER); Jiwe hili lenye rangi ya njano iliyochanganyika na kahawia linasemekana lina uwezo wa kumpa ukakamavu na ari ya uongozi kwa anayelivaa, vilevile linamwepusha mvaaji na maradhi ya kichwa.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(SIMBA NA NDOO):
Tabia ya Simba ya kutopenda kudhibitiwa au kudhibiti watu inakuwa ni faraja kubwa kwa wenye nyota ya ndoo ambao wanapenda uhuru na kufanya mambo yao bila kuingiliwa.

VYAKULA VYA SIMBA:

Wenye nyota ya simba wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao.
Vyakula hivyo ni machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo.

NCHI ZA SIMBA:

Watu wa nyota ya simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.

Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)

RANGI ZA SIMBA:

Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri.

Ushauri wangu huo hapa chini:

Tafuta rafiki aliyezaliwa tarehe 7 au tarehe 16 au tarehe 25 ndio atakayekufaa kimaisha kuwa rafiki yako na kushirikiana nao kimaisha au unaweza kumpata Mwaname aliye zaliwa kutoka tarehe
20 January mpaka 18February Huyo ndie atakuwa ni mume wako wa maisha yote.

Na pia ukitaka kutumia Pete jaribu kutafuta Pete zenye vito hiv hapa chini ndio pete zitkazo kufaa katika maisha yako soma hapa chini:

Mawe ya Vito vya Nyota ya Simba:

Mawe haya yafuatayo yote ni mawe ya nyota ya Simba na idadi yake ni sita 6. Yote yanatumiwa na mtu mwenye nyota ya Simba kwa sababu mbalimbali.
Soma maelezo ya matumizi ya mawe haya hapa chini ili uweze kujua zaidi namna ya kuyatumia.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Petrified Wood[/TD]
[TD] Garnet[/TD]
[TD] Diamond[/TD]
[TD] Jasper[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD] Quartz[/TD]
[TD] Onyx[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Petrified Wood
Jiwe hili lina uwezo wa kumfanya mtumiaji aweze kujua mambo yote ya maisha yaliyopita wakati wa taamuli (meditation) kama likitumika kwa ajili hiyo. Linamletea mtumiaji utulivu na ushwari wa moyo, usawa, uthabiti, afya njema na maisha marefu.
Linaleta ulinzi dhidi ya magonjwa na linasaidia kuponya mifupa, kuufanya imara uti wa mgongo na matatizo ya kusikia.

Garnet

Jiwe la kujitoa kwa ajili ya watu wengine, binafsi na katika malengo ya binafsi. Linaamsha "moto wa ndani" wa ubunifu. Linatoa ufufuo wa usawa kwa mtumiaji. Linahamasisha mapenzi na hisia kali za kimapenzi.
Jiwe hili linavuta bahati nzuri, ulinzi dhidi ya uchafu wenye sumu. Linakinga dhidi ya huzuni, mfadhaiko, upungufu wa damu na matatizo mbalimbali ya mwili.

Diamond (Almasi)

"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi.
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.

Jasper

"Jiwe kuu lenye jukumu kubwa la mafunzo na malezi". Linathaminiwa sana na Washamen kama jiwe takatifu na lenye nguvu linalotoa ulinzi na uthabiti. Linatoa ulinzi wakati wa safari za kinyota.
Linavuta nguvu za jua zenye uwezo wa kuufanya mwili kurudia hali ya ujana na kuupa nguvu. Linasaidia kuzalisha upya seli za mwilini (tisu) na mfumo wa harufu.

Quartz

Jiwe hili linakuza uwezo wa kutunza, malengo,kujirekebisha, kuhifadhi na na nguvu za kimwili na kiroho.
Linakuza uwezo wa kuhisi jambo kabla halijatokea. Pia lina uwezo wa kumfundisha mtumiaji kwa kadri ya uwezo wao na kasi zao. Vile vile linampa mtumiaji uwezo mkubwa wa mambo mbalimbali.
Onyx
Jiwe hili lina uwezo wa kumfanya mtu kujitawala mwenyewe. Linaleta kwa mtumiaji uwezo wa kufahamu mambo mbalimbali, ulinzi wakati wa Taamuli na ndoto. Linafichua uwezo wa ndani wa mtu uliojificha.
Linasaidia sana katika kutibu glakoma (ugonjwa unaotanua mboni ya jicho na kutatiza kuona), kifafa na uharibifu wa seli.

Thanks sana MziziMkavu kwa kunyambulisha!

Katika hayo mambo ya pete ndio nimebaki mdomo wazi! Siku zote niliamini watu huvaa pete kwa urembo na mambo ya majini tu! Kumbe hata mambo ya nyota nayo yana pete!!??!!!!!!
Hahahahahahahaaaa! Kweli kuwa uyaone!
...
Na jee MziziMkavu unaweza kutoa maelezo kwanini kunabaadhi ya siku watu wakioana ndoa hazidumu na kunabaadhi ya siku watu wakioana ndoa hudumu vizuri sana! (hii kitu niliwasikia wazee wakijadili na bahati mbaya hata hizo siku nimezisahau!) Nakumbuka walizizungumzia hizo siku ingeneral bila hata kuzingatia tarehe za kuzaliwa!

Hembu kama unafahamu lolote kuhusu hilo naomba unifafanulie! Na itakuwa vizuri zaidi ungeniambia na sababu zinazofanya kuwa hivyo!
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli kuna siku ukiowa au ukiolewa basi ndoa yako haidumu au waweza kupatwa na maradhi ya gafla ukafa wewe unaeolewa au huyo anaye kuowa mume wako. Hii inatokana siku yenyewe kuna siku mbaya na siku nzuri ingawa siku

nzuri na siku mbaya ni zote aliziumba Mwenyeezi Mungu. Kwa mfano siku mbaya kwa wiki ni siku 3 siku ya kwanza ni Jumamosi siku ya pili ni Jumanne na siku ya tatu ni jumatano. Siku hizo ukiowa au ukiolewa

basi ndoa yako inaweza isidumu, kwa mfano ukiolewa siku ya jumamosi basi ndoa yako itakuwa ni mashaka na mikosi isiyokwisha na huenda

ukapatwa na maradhi yatakayokusababisha ufariki yaani ukiolewa siku hiyo ya jumamosi hayo niliyosema yanaweza kukutokea moja wapo. Na yasipo kutokea ujuwe kwenye ndoa yenu kuna mashaka makubwa

hakuna baraka wala kila ukishika mimba inakuwa inatoka bila ya sababu na mume wako atakuwa anafukuzwa kazi au atakuwa na matatizo ya

nguvu za kiume yaani atakuwa hakufikishi wewe kileleni huyo mume akikuowa siku ya jumamosi. Na hivyo hivyo ukiolewa wewe siku ya Jumanne basi ndoa yako haiwezi kufikisha hata miaka 2 utapatwa na

ugonjwa wa wendawazimu au utaumwa gafla au kutupia pepo mchafu na maaduwi zako ndio itakuwa sababu ya wewe ndoa yako

kuharibika. Na hivyo hivyo ukiolewa siku ya jumatano utakuwa wewe mwanamke ni mgonjwa mgonjwa maradhi hayatakuwa yanakwisha mwilini mwako na kwa upande wa wakwe zako watakuwa wanakupiga

vita eti kwa sababu kwanini wewe huzai? Utakuw ani mgonjwa sana wa maradhi ya tumbo na kila unapopata siku zako utakuwa unaumwa sana na tumbo.

Siku nzuri za kuowa ni siku 2 Alkhamisi usiku kuanzia saa 5 usiku kwa Waislam na kwa ndugu zetu wakristo siku yao nzuri kuowa ni siku ya jumapili Asubuhi ndoa hapo itakuwa ni nzuri na yenye baraka.

Na pia siku ya ijumaa kwa ndugu zangu waislam kabla ya mshuko wa ijumaa pia ni siku nzuri sana kufunga ndoa. Mwanamke akiolewa siku ya ijumaa

atakuwa na nguvu ndani ya ndoa yaani mume wake atampenda sana mke wake kwa sababu siku ya ijumaa nyota inayo tawala ni nyota ya kike kwa hiyo wewe mwanamme ukimuowa siku ya ijumaa mke wako atakutawala kimapenzi

ndani ya ndoa yenu. Siku ya jumapili mwanamme akimuowa mke basi huyo mume atakuwa na nguvu ndani ya ndoa atakuwa kama vile simba anavyotawala porini ninaishia hapa kwa leo.
 
Hapa kuna sehemu kwa waislam siku nzuri ni ijumaa na wakristo ni jpill,Je kwa muislam ukioa j pill asubuhi kuna tatizo lolote?
 
Duh! nimevutiwa na uchambuzi wa kinyota wa mzizi mkavu, ila nataka kuuliza kidogo, mimi nimezaliwa 17/02/75. na toka 2011 mambo yangu hayaendi vizuri hasa katika kipato na mahusiano ya kimapenzi, kazi ndo nimetafuta mpaka nimechoka sanasana napata za mda mfupimfupi tu, biashara nimejaribu lakini haijaniinuia chochote, sasa ina maana nyota yangu haina mafanikio kwa miaka yote hii toka hiyo 2011? Na kama nataka kufanikiwa nifanye nini kwa nyota yangu?
 
hapo kwenye red -"you are right"
Sasa wewe hilo la kitovu ushawahi shuhudia na ukaona effect yake? sayansi inajaribu kuprove vitu vingi tu kwenye dini, biblia inavosema dunia ni round, sayansi nayo ikaprove hilo, biblia ilivosema binadamu aliumbwa wa mwisho hata evolution inasema vilianza vingine oceans, miti afu binadamu complete ni wa juzijuzi tu kwenye life tree ya evolution... Ila imani za ajabu ajabu zisizo na proof siwezi kuzisikiliza kabisa... I trust ndio kuna vitu spiritual ambavo scince haiwezi kuprove ila sio swala la nyota, swala la nyota is just a hoax watu wanapiga hela

Mpaka sayansi iprove ndio utaamini?we kweli akili zako ni za kushikiwa.sayansi unayotaka kuprove kwani lazima iende kwenye laboratory ndio ikawa proved?kama ndio hivyo basi tusingekuwa na social sciences ambazo huwa hazina concrete truth bali abstract truth ambazo ni valid kwani kuna njia za kuprove,kama unavyotaka kuprove hesabu,ukiifanya njia ile ile jibu litakuja vile vile.na ukijaribu kutoa baadhi ya vitu au kuhold on rest utaona tofauti ya majibu.

na kama ndio hivyo kwamba lazima tuprove kwenye laboratory basi wala tusingepata philosophers ambao walitumia tafakari na kutoa majibu sahihi kabla ya kuwa proved by experiment.wewe ni mwanasayansi wa wapi usiyeanza na theory unataka prove tu?

kwa taarifa tu mwanasayansi galileo galilei naye alikuwa msoma nyota na alikuwa anatabiri kama kawaida,na aliziangalia kwa utafiti zaidi kwani alikuwa more interested na effects za nyota katika maisha ya binadamu.

tatizo la wakristo wengi ni kama wanakondoo hawajui waendako na wale hawahoji mchungaji wao anapowapeleka kwan ni watii mno kwa wachungaji wao,wakristo wengi hawajui kwa nini elimu ya nyota na zinginezo zilipigwa marufuku na mungu.kwa kifupi tu elimu ya nyota ni elimu ya mbinguni ambayo binadamu hakutakiwa kujifunza kwani mungu hakumruhusu, bali elimu za nyota na zingine za uchawi zilifundishwa kwa wanadamu na malaika waliokuja kuzini na kuzaa na dada zetu kipindi cha akina nuhu na kuzaa mijitu mikubwa na maarufu ya kipindi hicho mfano akina sun wukong inasemekana alizaliwa kipindi hicho nk.hao malaika ndio wakawafundisha siri za mbinguni wanadamu.kwahiyo ni elimu kutoka mbinguni naomba msimkweze shetani eti ni elimu yake,maarifa yote hutoka kwa mungu.
 
Mpaka sayansi iprove ndio utaamini?we kweli akili zako ni za kushikiwa.sayansi unayotaka kuprove kwani lazima iende kwenye laboratory ndio ikawa proved?kama ndio hivyo basi tusingekuwa na social sciences ambazo huwa hazina concrete truth bali abstract truth ambazo ni valid kwani kuna njia za kuprove,kama unavyotaka kuprove hesabu,ukiifanya njia ile ile jibu litakuja vile vile.na ukijaribu kutoa baadhi ya vitu au kuhold on rest utaona tofauti ya majibu.

na kama ndio hivyo kwamba lazima tuprove kwenye laboratory basi wala tusingepata philosophers ambao walitumia tafakari na kutoa majibu sahihi kabla ya kuwa proved by experiment.wewe ni mwanasayansi wa wapi usiyeanza na theory unataka prove tu?

kwa taarifa tu mwanasayansi Galileo Galilei naye alikuwa msoma nyota na alikuwa anatabiri kama kawaida,na aliziangalia kwa utafiti zaidi kwani alikuwa more interested na effects za nyota katika maisha ya binadamu.

tatizo la wakristo wengi ni kama wanakondoo hawajui waendako na wale hawahoji mchungaji wao anapowapeleka kwan ni watii mno kwa wachungaji wao,wakristo wengi hawajui kwa nini elimu ya nyota na zinginezo zilipigwa marufuku na mungu.kwa kifupi tu elimu ya nyota ni elimu ya mbinguni ambayo binadamu hakutakiwa kujifunza kwani mungu hakumruhusu, bali elimu za nyota na zingine za uchawi zilifundishwa kwa wanadamu na malaika waliokuja kuzini na kuzaa na dada zetu kipindi cha akina nuhu na kuzaa mijitu mikubwa na maarufu ya kipindi hicho mfano akina sun wukong inasemekana alizaliwa kipindi hicho nk.hao malaika ndio wakawafundisha siri za mbinguni wanadamu.kwahiyo ni elimu kutoka mbinguni naomba msimkweze shetani eti ni elimu yake,maarifa yote hutoka kwa mungu.

Hapo kwenye red, galileo alikua hatabiri mtu anatakiwa kufanya kazi flani ili apate hela, utabiri wa kisayansi, vitu kama eclipses, acha uongo mtanzania...

Aya yako ya mwisho kuhusu wakristo sijui hilo umelitoa wapi, unaanza ushabiki wa kidini, tayari we ni mjinga hustahili kuongea na mimi, unawaita wakristo wajinga, ati elimu ya nyota ni elimu ya mbinguni binadamu hakutakiwa kujifunza, hilo ulijifunza wapi wewe? yani aya yako ya mwisho umeandika maujinga ujinga tu, hivi una maisha kweli we jamaa?

Na usinijazie maneno ambayo sijasema, we hayo ya nyota umeshayaprove? nshakaba wajinga wengi wananipa utabiri afu nafanya tofauti na walivosema, na mara zote nimewaprove kua wanachosema si sahihi, kama we nae umo sema unataka data gani nikupe unipe utabiri afu nifanye kinyume uone kama sitafanikiwa...

Sayansi hujui, bado umeandika mambo ya dini hujui, yani mjinga pande zote mbili, sijui utachomokea wapi we jamaa
 
Kwanza naomba uelewe nyota haikulazimishi kufanya chochote kuna kitu kinaitwa freewill na destiny,nyota inakuonyesha destiny but una freewill ya ama ufuate au usifuate,ukifuata utarahisisha maisha yako usipofuata ina maana unatafta njia zako mwenyewe kwa kupapasa na kubahatisha.

Wewe usiyejua kuhusu galileo nakupa pole,alikuwa astrologist aliyekuwa amebobea kwenye fani yake,hakufanya kuchagua eti hii ni mbaya au hii ni nzuri kuridhisha mtu wala kanisa na ndio maana alisimama hadharan kuipinga kanisa kuwa jua inazunguka dunia and not vice versa mpaka kanisa likaamua kumuua.

Inaonekana una jazba sana ulipoambiwa hamchunguzi maandiko,nenda kasome mwanzo6:1-3 ,halafu tafuta kitabu cha enock,kilisomwa mpaka na yesu ,kasome pia quran sikumbuki mstari vyote vinaelezea kwa undani kuhusu huo mstari wa kwenye biblia kwa undani zaidi.
 
Kwa wakristo BIBLIA TAKATITU imekataza kufuata utabiri wa nyota na mengine yafafananayo na hayo sijui kwa jirani zetu wa kibla

Ngoja pale mamajusi walipoona nyota upande wa mashariki unafikiria nini wewe?
 
Kwanza naomba uelewe nyota haikulazimishi kufanya chochote kuna kitu kinaitwa freewill na destiny,nyota inakuonyesha destiny but una freewill ya ama ufuate au usifuate,ukifuata utarahisisha maisha yako usipofuata ina maana unatafta njia zako mwenyewe kwa kupapasa na kubahatisha.

Wewe usiyejua kuhusu galileo nakupa pole,alikuwa astrologist aliyekuwa amebobea kwenye fani yake,hakufanya kuchagua eti hii ni mbaya au hii ni nzuri kuridhisha mtu wala kanisa na ndio maana alisimama hadharan kuipinga kanisa kuwa jua inazunguka dunia and not vice versa mpaka kanisa likaamua kumuua.

Inaonekana una jazba sana ulipoambiwa hamchunguzi maandiko,nenda kasome mwanzo6:1-3 ,halafu tafuta kitabu cha enock,kilisomwa mpaka na yesu ,kasome pia quran sikumbuki mstari vyote vinaelezea kwa undani kuhusu huo mstari wa kwenye biblia kwa undani zaidi.

Hapo ndo story za uongo zinapoanzia sasa, kutafta njia ya kujitetea once mtu akifaulu tofauti na hayo maprediction yanavosema, ati kuna free will na destiny.. Hahaha! hivo vitu viwili haviwezi vika exist pamoja, kukiwa na free will basi destiny doesn't exist, destiny ikiwepo basi si free will tena... na destiny ujinga kama huo ungekuwepo basi inamaana binadamu tunapoteza muda tu sema washachaguliwa binadamu watakaofika sehemu flani na ambao hata wafanyeje hawatofika, mfano mbinguni, sasa ya nini kujaribu kuokoa watu kama kuna destiny inaguide watu...
Kusema khs maandiko, ni vema usim-judge mtu kuhusu maandiko maana kila mtu ana njia yake anavoelewa, afu kudhani wewe uoivotafsiri ndio right na mwenzako sio basi unajidanganya...

yani ukitaka twende sambamba usianze ushabiki wa kidini, tujaribu kwenda na logic tu kama utani-convince basi ntakubaliana na wewe, sema kwa sasa hujani-convince bado...

Em nipe utabiri moja wa Galileo alioufanya kuprove statement yako kuhusu yeye, utabiri ambao sio scientific unaoenda na imani imani hizo ati nyota na destiny... nlichukua course ya astronomy part flani chuoni just for fun na nlisoma mengi kuhusu huyu jamaa, unavonambia alikua anacheza na destiny sijui utabiri wa nini nakushangaa maana yeye alikua anacheza na science, maths physics astronomy, real facts not superstitious
 
Hapa kuna sehemu kwa waislam siku nzuri ni ijumaa na wakristo ni jpill,Je kwa muislam ukioa j pill asubuhi kuna tatizo lolote?
Hakuna tatizo hata kwa Wakristo wakiowa siku ya ijumaa na Wewe Muislam ukiowa siku ya jumapili hakuna matatizo mkuu.
 
Duh! nimevutiwa na uchambuzi wa kinyota wa mzizi mkavu, ila nataka kuuliza kidogo, mimi nimezaliwa 17/02/75. na toka 2011 mambo yangu hayaendi vizuri hasa katika kipato na mahusiano ya kimapenzi, kazi ndo nimetafuta mpaka nimechoka sanasana napata za mda mfupimfupi tu, biashara nimejaribu lakini haijaniinuia chochote, sasa ina maana nyota yangu haina mafanikio kwa miaka yote hii toka hiyo 2011? Na kama nataka kufanikiwa nifanye nini kwa nyota yangu?
Pole sana kutokana na nyota yako ya tarehe uliyozaliwa utafanikiwa ukifika mwaka 2019 sasa hivi jitahidi tu lakini huo mwaka ndio wa mafanikio uako na nyota soma hapa chini:

NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)

  • Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 20 January na 18 February.
  • Sayari yao ni SATURN (ZOHAL).
  • Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
  • Namba yao ya bahati ni 8.
  • Rangi yake ya bahati ni Nyeusi.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.

KIPAJI CHA NDOO

(Sudden Revelation)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote.

TABIA ZA NDOO

Wenye nyota ya Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.
Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.
Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.

TABIA YA NDOO KATIKA MAPENZI.

Wenye nyota ya Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.
Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.
Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.
Katika ngono kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
{mospagebreak}

TABIA YA NDOO KATIKA FEDHA

Wenye nyota ya Ndoo ni watu ambao wenye ndoto na mipango mingi ya kifedha ya baadae, na wakati mwingine wanajikuta kwamba mawazo yao ya kifedha yanakuwa hayaendani na wakati uliopo.
Masuala ya kifedha kwao yanategemea sana aina ya kazi, ambayo mara nyingi inahusiana na mambo ya sanaa au sayansi, sehemu ambayo wao watajihisi wanatoa mchango wao kwa binaadamu.
Wanapokuwa matajiri mara nyingi inatokana na ustadi au umahiri na wale siyo uwezo wao.
Wenye nyota hii huwa wanapenda sana kupata fursa ya kufanya kazi sehemu tofauti na hawependi kufungika katika sehemu moja, kwao fedha ni chombo kinacholeta uhuru na wanaona vyema maisha yao yakamilike kuliko kuwa tajiri.
Mara nyingi wanachukia kuonekana kwamba wao ni wabinafsi. Hata hivyo wanapenda vitu vizuri lakini kwa sababu ya ubahili huwa wanaona raha wanapoviona vitu hivyo kwa watu wengine katika makumbusho au nyumba ya sanaa kuliko kuwa navyo wenyewe.

MAVAZI YA NDOO

Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya Kijivu, au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.
Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikono.

MATATIZO YA KIAFYA.

Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.
Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.
Matatizo yao makubwa yanasababisha na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi na ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.
Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndog ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.

KAZI ZA NDOO

Hawa ni watu wenye akili nyingi na wenye malengo maalum katika shughuli fulani. Ni wawekezaji asili na wana uwezo wa kuwabadilisha watu tabia zao kutoka mbaya kuwa nzuri.
Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.
Kazi zao wanazifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.
Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.
{mospagebreak}

FAMILIA ZA NDOO

Wazazi wa nyota hii ni wenye shauku na wasiotabirika na wanaopenda maendeleo ya watoto wao.
Wazazi wa Ndoo wako wazi na wanaweza kuzungumza chochote na wototo wao lakini ni wagumu kubadili mawazo yao ambayo wakati mwingine yanakuwa ya ajabu.
Huwa wanapenda kuwahimiza watoto wao wawe huru kujieleza lakini wao wenyewe hawapendi kushutumiwa. Kwa upande mwingine ni wazazi ambao hawana mbinu katika kushughulikia mambo yanayowahusu watoto.
Ni wazazi wanaowapenda watoto wao na wao wanapendwa sana na watoto na mara nyingi huwa hawalalamikiwi.
Ni muhimu kwa wazazi wa kiume wenye nyota hii kuwaelewa vizuri watoto wao vinginevyo tabia zao zinaweza zikasababisha migongano.
Kwa wazazi wa kike wanashauriwa waache tabia yao ya kigeugeu au ukali tabia ambayo mara nyingi watoto huudhiwa nayo.

MADINI YA NDOO

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa Aquamarine Madini hayo yenye kumeremeta yanaashiria hewa ambayo ndio asili ya nyota ya Ndoo.
Jiwe hili linaashiria urafiki na inasemekana huondoa uchovu wa akili.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(NDOO NA SIMBA)
Tabia ya kupenda kuwa huru na kujifanyia mambo bila kuingiliwa waliyokuwa nayo wenye nyota ya Ndoo, huwafariji wenye nyota ya Simba ambao nao hawapendi kuingiliwa katika mambo yao.

VYAKULA VYA NDOO.

Wenye nyota ya Ndoo wanashauriwa wepende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota zao.
Wapende sana vyakula vya nazi na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.

NCHI ZA NDOO

Ili kupata mafaniko ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni Sweden na Zimbabwe na Miji ni Humburg (Ujerumani) na Leningrad (Urusi).

RANGI ZA NDOO

Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.

FUATA HUO USHAURI UTAFANIKIWA AKIPENDA MUNGU.
 
Mkuu MziziMkavu nashukuru kwa namna unavyojitoa kutuelimisha kwa kutupa uzoefu wako,maarifa na ujuzi mbalimbali katika mambo tofauti tofauti. Binafsi ni msomaji wa majukwaa karibuni yote na hupendelea zaidi aidha kuuliza ama kucoment kwa jambo lolote la kheri. Je,unaweza kunisaidia nami kwa tarehe hii 12January? Kinyota nikoje japo nafahamu kuwa niko Mbuzi.
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndo story za uongo zinapoanzia sasa, kutafta njia ya kujitetea once mtu akifaulu tofauti na hayo maprediction yanavosema, ati kuna free will na destiny.. Hahaha! hivo vitu viwili haviwezi vika exist pamoja, kukiwa na free will basi destiny doesn't exist, destiny ikiwepo basi si free will tena... na destiny ujinga kama huo ungekuwepo basi inamaana binadamu tunapoteza muda tu sema washachaguliwa binadamu watakaofika sehemu flani na ambao hata wafanyeje hawatofika, mfano mbinguni, sasa ya nini kujaribu kuokoa watu kama kuna destiny inaguide watu...
Kusema khs maandiko, ni vema usim-judge mtu kuhusu maandiko maana kila mtu ana njia yake anavoelewa, afu kudhani wewe uoivotafsiri ndio right na mwenzako sio basi unajidanganya...

yani ukitaka twende sambamba usianze ushabiki wa kidini, tujaribu kwenda na logic tu kama utani-convince basi ntakubaliana na wewe, sema kwa sasa hujani-convince bado...

Em nipe utabiri moja wa Galileo alioufanya kuprove statement yako kuhusu yeye, utabiri ambao sio scientific unaoenda na imani imani hizo ati nyota na destiny... nlichukua course ya astronomy part flani chuoni just for fun na nlisoma mengi kuhusu huyu jamaa, unavonambia alikua anacheza na destiny sijui utabiri wa nini nakushangaa maana yeye alikua anacheza na science, maths physics astronomy, real facts not superstitious

That is a life riddle,ni sawa sawa na kukataa eti kwa sababu kuna mwanga basi hakuna giza,life is like a coin with two side.everything has its opposite.kuna watu wamezaliwa tayari majina yao yameandikwa na kuja kwao kumetabiriwa kabisa tofauti na wewe.huwezi kujifananisha na yesu wala mtume muhammad ambao majina yao yashaandikwa na kutabiriwa.wewe angalia nyota yako ukiifuata vema utafanikiwa pia

Halafu kwa nini unakimbilia kutafsiri tofauti,wakati maneno mengine yanajieleza wazi?sio kila mstari ni fumbo,nyie ndio mnaoingia kwenye mtihani unapewa swali rahisi unaanza kuhisi kutakua kuna mtego haiwezekan swali likawa rahisi
 
Haha mtanzania usiweke maneno ambayo sijayasema, nani kasema anakimbilia kutafsiri vingine?
alafu nani kajilinganisha na Yesu au Muhammad? haha, kwa hiyo utabiri wa hawa wawili ulitabiriwa kwa nyota? au ndo utaanza na wewe story za ile nyota ya Yesu iliyotoa guidance?

Haya tufanye mo mjinga, em nambie hizo nyota ndo zinafanyeje kazi? nimekwambia unipe convincing statement ili nikuamini ila hujanipa hata moja,
 
Galileo's Astrology by Nick Kollerstrom

Dreson4
Soma hiyo link inamuongelea galileo na alivyokuwa ana practise astrology(utabiri),hata kanisa nalo lilishawahi kumshtaki katika hilo suala.
Ingawa nao baadhi ya viongozi wa kanisa walimfuata kwa ushauri kisiri siri.

Kama unakubali akina yesu walitabiriwa na hata nyota zilionekana angani,hata wale mamajusi walipofika walimuulizia kama mfalme,kwani walishaisoma nyota yake angani na majibu walikuwa wanayo atakuwa ni mtu wa aina gani.
Ila kumbuka kitu kimoja vitabu vilitabiri lakini kuja kwa masihi hakukusemwa itakuwa lini hasa,ni watu wa nyota ndio walikuwa wa kwanza kuona ishara mbinguni na ndio tafsir na unabii ulipoangaliwa tena.

kwa hiyo bila mamajusi au watabiri wa nyota taarifa za kuzaliwa kwa bwana yesu zingepita kimya kimya.
 
Ni kweli kuna siku ukiowa au ukiolewa basi ndoa yako haidumu au waweza kupatwa na maradhi ya gafla ukafa wewe unaeolewa au huyo anaye kuowa mume wako. Hii inatokana siku yenyewe kuna siku mbaya na siku nzuri ingawa siku

nzuri na siku mbaya ni zote aliziumba Mwenyeezi Mungu. Kwa mfano siku mbaya kwa wiki ni siku 3 siku ya kwanza ni Jumamosi siku ya pili ni Jumanne na siku ya tatu ni jumatano. Siku hizo ukiowa au ukiolewa

basi ndoa yako inaweza isidumu, kwa mfano ukiolewa siku ya jumamosi basi ndoa yako itakuwa ni mashaka na mikosi isiyokwisha na huenda

ukapatwa na maradhi yatakayokusababisha ufariki yaani ukiolewa siku hiyo ya jumamosi hayo niliyosema yanaweza kukutokea moja wapo. Na yasipo kutokea ujuwe kwenye ndoa yenu kuna mashaka makubwa

hakuna baraka wala kila ukishika mimba inakuwa inatoka bila ya sababu na mume wako atakuwa anafukuzwa kazi au atakuwa na matatizo ya

nguvu za kiume yaani atakuwa hakufikishi wewe kileleni huyo mume akikuowa siku ya jumamosi. Na hivyo hivyo ukiolewa wewe siku ya Jumanne basi ndoa yako haiwezi kufikisha hata miaka 2 utapatwa na

ugonjwa wa wendawazimu au utaumwa gafla au kutupia pepo mchafu na maaduwi zako ndio itakuwa sababu ya wewe ndoa yako

kuharibika. Na hivyo hivyo ukiolewa siku ya jumatano utakuwa wewe mwanamke ni mgonjwa mgonjwa maradhi hayatakuwa yanakwisha mwilini mwako na kwa upande wa wakwe zako watakuwa wanakupiga

vita eti kwa sababu kwanini wewe huzai? Utakuw ani mgonjwa sana wa maradhi ya tumbo na kila unapopata siku zako utakuwa unaumwa sana na tumbo.

Siku nzuri za kuowa ni siku 2 Alkhamisi usiku kuanzia saa 5 usiku kwa Waislam na kwa ndugu zetu wakristo siku yao nzuri kuowa ni siku ya jumapili Asubuhi ndoa hapo itakuwa ni nzuri na yenye baraka.

Na pia siku ya ijumaa kwa ndugu zangu waislam kabla ya mshuko wa ijumaa pia ni siku nzuri sana kufunga ndoa. Mwanamke akiolewa siku ya ijumaa

atakuwa na nguvu ndani ya ndoa yaani mume wake atampenda sana mke wake kwa sababu siku ya ijumaa nyota inayo tawala ni nyota ya kike kwa hiyo wewe mwanamme ukimuowa siku ya ijumaa mke wako atakutawala kimapenzi

ndani ya ndoa yenu. Siku ya jumapili mwanamme akimuowa mke basi huyo mume atakuwa na nguvu ndani ya ndoa atakuwa kama vile simba anavyotawala porini ninaishia hapa kwa leo.

mziku mimi nimezaliwa tarehe 18/9/1981 niambie huo uongo wenu kuhusu maisha na nyota yangu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom