Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Status
Not open for further replies.
Daaaah hapo umenikuna na kunifanya nianze kufuatilia haya mambo,embu niambie tarehe 18.04 ni nyota gani na ipoje?tafadhali nataka kujifahamu na mimi
Wewe kwa nyota yako ni Kondoo au Punda kwa jina lingine hujatowa mwaka uliozaliwa siwezi kukwambia lini utapata nitakupa data za nyota yako na madini ya nyota yako . soma hapa chini
horoscope_aries_.jpg

NYOTA YA PUNDA AU KONDOO (ARIES)

  • Hii ni nyota ya kwanza katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21st March na tarehe 19 April ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Mars (Mariikh)
  • Siku yao ya bahati ni Jumanne
  • Namba yao ya bahati ni 9
  • Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu.
  • Asili yao ni Moto.

NYOTA YA PUNDA AU KONDOO KATIKA MAPENZI NA MAHABA


Kwa vile wao ni wenye nyota ya kwanza mara nyingi wenye nyota hii wanapenda kuwa mbele. Wanakuwa wakarimu na wenye pendo kwa wapenzi wao.


Ni watu wenye kupenda kushirikiana na watu wengine, wanapenda mikusanyiko ya jamii na wacheshi. Ni watu wazuri kuwa nao karibu na mara nyingi wao wanakuwa ndio maisha na roho ya kundi wanalojihusisha nalo. Hivyo inatokana na tabia zao za asili za uchangamfu. Hata hivyo wakiudhiwa huwa ni viumbe wenye hasira kali.

Wenye nyota hii ni wepesi sana kuvunjika moyo na hii inatokea wakati wapenzi wao wanapowaangusha au kuwadharau katika mapenzi ambayo wao wanayachukulia kwa uzito mkubwa.

Pamoja na uchangamfu walio nao wenye nyota ya Punda wana moyo dhaifu usiovumilia matatizo na wanaweza kudhuriwa kirahisi katika mapenzi.

Wanaingia katika mapenzi na kupenda kirahisi. Mara nyingi wanawafanya wapenzi wao ndio nguzo au kiegemezo na hapo ndipo matatizo yanapoanza.

Wasipopata njia ya kutatua matatizo ya kimapenzi huwa wanachanganyikiwa na wanafadhaika sana hasa wanapogundua kwamba wapenzi wao ni binadamu kinyume na walivyofikira wao.

Kwao wazo la kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja milele linapewa kipaumbele katika mambo ya mahaba, lakini wakiona mambo yanaenda kombo basi ni mwepesi sana kuondoka kwenda kutatufa mpenzi mpya sehemu nyingineyo.

Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kuwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.


NYOTA YA PUNDA KATIKA FEDHA

Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia nguvu au kulazimisha na siyo waoga. Mipango yao ya kifedha wanayoipanga inakuwa na ubora wa hali ya juu inayopendeza na inayowavutia watu wengine. Hii inatokana na uwezo wao, shauku na vipaji vya kiakili kuhusiana na masuala ya fedha.

Hakuna sehemu yeyote ambayo mwenye nyota ya Punda atafanya shughuli yeyote bila watu kupendezwa na mipango yao. muda wote wako tayari kuchukua majukumu bila kujali chochote na mwisho wake mafaniko yanakuwa makubwa. Suala la kujiliza ni kuwa je wanaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu?

Jibu ni hapana watu wa Punda wanatambulika kwa tabia yao ya ufuatiliaji wa mambo, bila kuchoka lakini tabia yao ya kiburi katika mambo madogo madogo ya kibiashara na kikazi wakati mwingine huhatarisha mradi au kazi zao zote.

Wanapenda kutumia fedha kiholela bila kupata uhakika kwamba zitarudi au zipo. Hulka yao ya kuwa mbele na kupenda kuishi kiuaminifu huwafanya wakose kinga kwa wajanja wanao penda kuwatapeli.

Kitu kimoja ni kwamba Mungu amewapa uwezo wa kufanya kazi vizuri wanapokuwa wao viongozi au wasimamizi. Wanakuwa na nia na moyo wa kufanya mambo mapya, lakini ajabu ni kwamba hawana subira wala mbinu za utawala hasa katika masuala ya fedha.

Papara zao za kujua mambo zaidi mara nyingi husababisha utatanishi kwa watu wote wanaowazunguka na wanao wakilisha.

Kimaisha wenye nyota ya Punda wanapenda sifa na kuonyesha matunda ya kazi zao au uwezo wao kifedha kwa kununua magari mazuri, nguo zenye thamani kubwa na vito vya thamani ili waonekane pamoja na ukarimu wao wakati mwingine hubadilika na kuwa wabinafsi na wachoyo.

Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu wenye ari na uwezo wa kuanzisha mambo na wanapenda kupata maendeleo ya kimaisha na kuwa na miradi mipya. "NATAKA" ndio neno lao kubwa. Wanahitaji sana fedha, uwezo na uvutio ni wakati mchache sana huangalia maslahi ya watu wengine. Huwa wanakabiliwa na tatizo la kuchagua fedha au mamlaka, hata hivyo mapenzi yao ya kuwa na uwezo huwa yanashinda.

{mospagebreak}

NYOTA YA PUNDA (AFYA ZAO)

Wenye nyota hii ni watu wenye nguvu na afya nzuri. Wakati wote wao wanakuwa hawana subira ya kungoja kufanya shughuli zinazowahusu. Ni watu ambao hawapendi kabisa kuugua au kupata maradhi. Mara nyingi wanakuwa na uwezo wa ajabu wa kupona maradhi yanyaosumbua.

Kwa vile nyota hii ya Punda inatwala kichwa maradhi yao mengi yanahusiana na kuumwa kichwa na homa za mara kwa mara ambazo hupotea kama zilivyokuja.


Tatizo lao kubwa la kiafya ni la "Adrenalini" (Hii ni Homoni inayotoka ndani ya mwili wakati mtu anaposhtushwa au kukasirika, ambayo inafanya moyo upige haraka na kuutayarisha mwili kupambana na khatari). Watu hawa wanafanya kazi bila kuchoka na inatakiwa nguvu zao zielekezwe sehemu inayohusika, ikitokea vinginevyo huwa wanakosa raha na kuwa na wasiwasi.


Wasiwasi huo unasababisha "Adrenalini" kumwagika kwa wingi wanakuwa wepesi kuudhika na kukasirishwa na kuwa na Hamaki au ghadhabu za haraka ambazo huwaletea matatizo ya mzunguko wa damu katika Ubongo na macho.

Watu wa Punda wanahitaji kufahamu kwamba wao hawana kinga hivyo mapumziko ni muhimu kwao. Wanatakiwa wapendelee kutembea kwa miguu au wajihusishe na michezo ili kuondoa mzigo wa uchokozi, hakami na hasira walionao.
Utaratibu maalum wa kula chakula vile vile ni muhimu, na wenye nyota hii wanashauriwa kukiepusha na kahawa na sukari nyeupe ambao inaongeza mfadhaiko katka mfumo wa neva na tezi za "Adrenalini". Ni wachache sana wenye nyota hii ambao wana matatizo ya uzito kwa sababu wanajishughuoisha sana na shughuli mbalimabli.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokata tamaa huwa wanaathirika, na tbaia yao ya haraka haraka inawafanya wawe katika vita na miili yao wenyewe. Matokeo yake ni kuathirika kiafya. Wanatakiwa wajifunze tabia ya nyota ya Mizani ya ushirikiano. Tabia hii pamoja na kwamba itawapunguza kasi zoa katika utendaji lakini itawasaidia kudhibiti matatizo yao ya kiafya.

NYOTA YA PUNDA (MAISHA YAO)


Punda wanapenda sana kujihusisha na masuala ya kuwafanya waishi vizuri kama binaadamu wengine. Wanapenda sana vitu vyenye msisimko vya pekee na utaona hivyo katika nyumba zao.

Kuweka makazi ya kudumu kwa mtu wa Punda ni moja ya mitihani mikubwa ambayo ana lazima atekeleze lakini kwa watu wengine jambo hili wanalichukulia kama mojawapo ya mambo mengi ya kimaisha ambayo wakipata fedha anataka watekeleze.

Moja ya hulka za Punda ni kuthibiti namna nyumba zao zinavyoendeshwa. Hivyo inamaanisha kwamba wanahitaji kupata mwenzi mwaminifu ambaye atatekeleza yote atakayoagizwa kuyafanya hapo nyumbani. Vinginevyo tabia zao za kutokupumzika na tamaa ya kufanya mambo mapya itawafanya wapoteze hamu ya maisha yao ya nyumbani.


Wanapokuwa tayari wameweka mizizi yao wanakuwa waaminifu kwa familia zao. Hata hivyo kuna hatari kwamba wasipoweza kupata wanachokitaka hapo nyumbani wanaweza kusimama na kuondoka.

Hawawezi kuficha hisia zao kwa yeyote wanayemualika katika nyumba zao ukikosa atakuambia na hawategemei hata walioalikwa nao kuficha hisia zao vile vile.
Kutokana na shauku na hamu kubwa ya kuthitisha maisha yao, ni vizuri Punda wakawa waangalifu, wasiwe wajeuri au wakandamizaji katika nyumba zao.
Ni watu wanaozipenda familia zao na mara nyingi wanatumia nyumba zao kama sehemu ya kufanyia kazi badala ya mapumziko.

{mospagebreak}

NYOTA YA PUNDA (LIKIZO NA SAFARI)

Nyota ya Punda ni nyota yenye asili ya moto, maana yake ni watu wenye ari na nguvu zisizo na mipaka, na mara nyingi wanatatufa vitu vinavyowafurahisha. Wanapenda sana kusafiri aidha katika biashara au kwa kujifurahisha.
Wenye nyota hii wana tabia ya kujenga uhusiano mkubwa katika tabia fulani. Hii inapotokea wanapenda kutumia muda wao mwingi katika mazingira hayo ili wayaelewe vizuri. Wanajua kabisa sehemu au mji ambao watajisikia wako nyumbani.
Muda mwingi huwa wanapenda mazingira mapya na hii inawafanya kupata uzoefu mkubwa mara nyingi wanakuwa ni waalimu
wazuri sana. Ukweli wa mambo ni kwamba walimu wengi wa shule wanaowaongoza wanafunzi katika safari za nje ni wenye nyota ya Punda.


Punda ni wasafiri majasiri na wanapenda vyombo vinavyokwenda kasi. Kwao ni bora kusafiri kwa ndege kuliko kupanda basi linaloenda polepole. Huwa wanapenda kusafiri daraja la kwanza kama wakikosa kabisa basi watasafiri daraja la pili.

Ukiwa katika likizo pamoja na mwenye nyota hii unaweza ukaudhika kwa sababu wao mara nyingi wanatafuta mambo mapya na wanakuwa hawatulii sehemu moja kwa kutegemea ujasiri wao.
Kwa ujumla kwa vile wenye nyota ya Punda ni watu wasiokuwa na subira kwa rafiki zao wa duniani hawapendi kungoja watu

wakubaliane na mipango yao ya safari ambayo wanaweza kubadilisha bila taarifa. Kwa sababu hiyo mara nyingi wanasafiri peke yao, au wanaweza kujitenga mbali na walio karibu nao. Hivyo watu wa Punda wanashauriwa kuwa na subira ya kuwangoja wenzi wao katika likizo au safari zao.


NYOTA YA PUNDA (TABIA ZAO)


Tabia ya wenye nyota ya Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisi na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote.
"SASA HIVI" hivyo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu wasiokuwa na surbira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Wenye nyota hii ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu. Wao wakati wote wanajiona kwamba "Wanajua sana".
Pamoja na kwamba wanakuwa wa kwanza kukamata mambo ya msingi ya jambo lolote wao wanakuwa wa mwisho kuliacha na ni wafuatiliaji wazuri.

Kwa upande mwingine watu hawa wewe wape njia ya kutatua tatizo au ya kufanya jambo jipya, utashangaa jinsi watakavyolichambua na kulitekeleza jambo lenyewe.

Jambo la kushangaza kwa wenye nyota hii ni kwamba tatizo lao kubwa linakuwa kusitasita au kuchelewesha jambo. Pamoja na kwamba wao wanapenda mambo ya haraka lakini yakiwa hayawavutii basi huwa hawana haraka nayo.
Vile vile wanaweza kuwa butu. Mara nyingine hufanya makosa makusudi au kuwachokoza wafanyakazi wenzao kuonyesha ubinafsi wao ili wafanikiwe.

Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu ambao wanajipendelea. Ni watu ambao "MIMI KWANZA" ndio tabia yao wanapenda waonekane kwamba wao ndio wanajua zaidi na tabia hiyo inawasaidia, ukweli wa mambo ni kwamba wenye nyota ya punda kila walitakalo wanalipata.

{mospagebreak}

TABIA YA PUNDA (KATIKA NGONO)

Wanapokuwa chumbani, tatizo kubwa la wenye nyota hii ni ubinafsi. Watu wa Punda huwa wanapenda kujishughulisha sana na mambo ya ngono na wanategemea kwamba wapenzi wao nao wajihusishe kikamilifu katika tendo hilo. Wakiona kwamba wapenzi wao hawako makini wakati wa ngono basi hujihisi kwamba hawapendwi na hawatakiwi.

Wenye nyota hii ni watu wenye bashashi na wacheshi na hiyo inawafanya wawe ni watu wenye hisia kali na haraka, hivyo inakuwa vigumu kwao kufanya mambo kwa mpangilioi na pole pole. Hivyo inawafanya wasiweze kuwachezea wapenzi wao kabla ya ngono.


Hisia zao kubwa ni kufanya tendo la ndoa na ni wakati huo huo bila kungoja.

Kutokana na ubinafsi huwa wanasahau kabisa hisia za wapenzi wao. Kwa kweli ni watu ambao wanajipendelea sana katika tendo la ndoa na hiyo huwa inawaletea matatizo katika uhusiano wao wa kimapenzi.
Wakati wanapochagua mpenzi Punda wanashauriwa wahakikishe kabisa wanapata wapenzi ambao wana ashiki au nyege za haraka haraka kama wao.

Katika kipindi cha kubembeleza pendo (kutongoza) watu wa Punda wanatakiwa waonyehse tabia ya asili ya ukarimu na mahaba ili wapendeke na vile vile wajaribu kuachana na tabia yao ya asili ya hisia kali na ukali.

Wanaume wa nyota hii wanapenda sana kujiona kwamba wao ni mabingwa na mashujaa katika ngono.

Kwa ujumla watu wa nyota hii ni wenye kuhitaji sana ngono. Ni watu ambao hawataki kukataliwa. Wanaume wa nyota hii wana ashiki na hamasa za kufanya ngono kuliko kupenda na wanaliangalia hilo wanapotafufa wapenzi kwa wanawake nao wana hamu kubwa ya kufanya tendo la ndoa.

Hakika wenye nyota hii wanaweza kuwa wapenzi wazuri.

NYOTA YA PUNDA (KAZI ZAO)


Wote wake kwa waume waliozaliwa katika nyota hii wana kipaji cha asili cha uongozi na wasiwasi wa kushindwa katika utekelezaji.

Kwao kitu cha pili au wao wenyewe kuwa namba mbili. Wanawake katika hali ya ushindani ambapo wanaweza kutekeleza kazi zao katika spidi au haraka wanayoitaka ambayo mara nyingi inakuwa mara mbili ya spidi ya kawaida, kila kitu kitakuwa sawa.

Wenye nyota hii huwa wanafanya vizuri shughuli zao za kazi au taaluma, mradi shughuli hizo ziwe zinazoleta athari. Hawapendi kuburuzwa wala kuishi bila kupata ushindani ni kawaida mara nyingi katika kazi zao hutokea migongano kati yao na wale wenye mamlaka juu yao. Wanapenda sana kupambana na hali ya ushindani wa kikazi na mara nyingi huwa wakiasisi shughuli mpya au kutoa mawazo mapya. Vile vile wanapenda sana ushindani wa kutafuata kitu kilichopotea.


Watu wa Punda ni watu ambao wanaweza kuhisi jambo lolote, ni watu wanaopenda kutumia nguvu katika kazi na wakifanya kazi yoyote wanaifanya kwa moyo mmoja. Wakiwa katika kazi, hupenda kufanya kazi peke yao au katika kazi hiyo wawe ni wasimamizi.

Kwa ujumla kwa vile watu wa Punda wanafanikiwa katika ushindani wanafurahi sana wanapofanya kazi ambazo zenye vipingamizi na ambazo utekelezaji wake unahitaji akili nyingi na nguvu.
Watu wa aina hii wakishindwa kutekeleza majukumu yao huwa wanavunjika moyo vibaya sana. Wanapenda sana kufanya kazi katika mazingira ambayo yanahitaji muda maalum kutekeleza mambo fulani.
{mospagebreak}

NYOTA YA PUNDA (FAMILIA ZAO)

Wazazi wenye nyota ya Punda wanakuwa wakarimu sana kwa watotowacheshi watafanya kila njia kuwahimiza wawe huru na watawaruhusu wafanye majaribio mbali mbali ya kimaisha na kuwahimiza kuchukua majukumu makubwa kwa gharama yeyote. vile vile watawahimiza watoto wao wawe na tabia ya ushindani badala ya kuwafundisha michezo.
Wazazi wenye nyota hii watawapa watoto wao nafasi kujisimamia wenyewe katika mambo yao. tatizo lao moja ni kuwa hawapendi watoto ambao ni ving'ang'anizi na wanaohofia usalama wao.

Watoto ambao ni waangalifu waoge na wanaofanya mambo kwa kufikiria wanakuwa hawaendani sana na wazazi wenye nyota ya Punda kwa sababu Punda hawapendi watoto wenye haya, waoga na wepesi kutishwa.

Wazazi wa nyota hii wanaweza kuwa wakali, wasiokuwa na mbinu na wenye kauli za ukali ambazo zinaweza kuudhi mtoto yeyote mwenye moyo mdogo. Tabia hii mara nyingi inasababisha migongano kati ya mzazi na mtoto na kutokuelewena kunakuwa kukubwa.

Wazazi wa Punda wanashauriwa kujilinda katika kuwashinikiza watoto wao kwa nguvu na haraka na kuwaruhusu watoto hao wakue na wafanye vitu katika njia za kawaida.

Kwa ujumla wazazi wa Punda ni wenye msukumo lakini wanajivunia sana watoto wao ni wazazi wenye makaka na wanapenda sana utani kwa vile hata wao mioyo yao ni ya kitoto. Mzazi wa kike anapenda ushindani hasa katika mausuala ya maisha na kuishi lakini hata yeye anapenda utani hasa anapokuwa nyumbani.

NYOTA YA PUNDA (MAUMBO YAO)

Wenye nyota ya Punda ni wenye uso mrefu mpana paji lao la uso hutanuka likiambatana na fuvu lililokaa vizuri. Macho yao ni makali na yenye kuonyesha uzima na uhai na yaliyotumbukia kwa ndani.
Nyusi zao ni nyeusi zenye kuonekana wazi au zilizo dhahiri kama zimepakwa wanja. Pua zao ni za bapa na midomo yao ni mipana.
Unapozungumza na wenye nyota hii naye atakusimamia wima mbele yako na kukuangalia moja kwa moja kwenye macho yako.
Tabia yao hiyo inawafanya waonekane wao ni wenye tabia za kigomvi au ushauri lakini ukiangalia kwa undani utagundua kwamba ni wakweli na wanaoweza kuaminiwa.
Hata hivyo kipindi cha kukusimamia wima inakuwa kifupi hasa anapokuona mpuuzi.

Kimaumbile ni watu wepesi na mwendo wao ni wa madaha. Miili yao kidogo imeinamia mbele ya misuli yao inaonekana imekakamaa, hiyo ni kwa sababu ya kujishughulisha sana bila kupumzika.

Sifa za wanaume wa Punda ni kwamba wako makini na wenye msimamo. Ni wembamba na miili yao ni yenye misuli iliyojikunja kunja.

Wanawake nao ni wembamba na maumbile yao siyo ya kupendeza sana, mikono yao na miguu yao ni yenye nguvu. Matamanio yao na uwezo wao huwa inawafanya wawe wanawake wenye tabia za kiume.

Kwa ujumla alama ya Kondoo ni pembe zake na mambo yote yanayohusiana na pembe hizo. Wenye nyota hii wanapenda kupambana na maisha. Kimaumbile athari zao huonekana mara moja. Kama vile kujiamini, namna wanavyosalimia watu na vicheko vyao. Vitendo vyao hivyo vinakujulisha kwamba huyu ni Punda.
{mospagebreak}

NYOTA YA PUNDA (VYAKULA VYAO)

Kama ilivyo katika tabia zao wenye nyota ya Punda vile vile wanapenda vyakula vya haraka haraka.
Ukweli ni kwamba mawazo yao mara nyingi yanakuwa katika maisha kuliko chakula pamoja na kwamba wanakuwa na hamu na uwezo mkubwa wa kula. Wanapenda chakula kizuri lakini kiwe cha haraka na rahisi kutayarisha.
Wanapenda sana kufanya karamu tafrija ambazo wana kipaji kikubwa cha kuzitayarisha na wanazifurahia. Katika karamu hizo vyakula vyao vinakuwa vya haraka ambavyo vinagawiwa wima wima bila kucheleweshwa.

Wakati wanapokuwa hawafanyi karamu au tafrija wanapenda chakula chochote kinachotayarishwa upensi na ambacho kinaweza kulika huko wanatembea, kama vile asusa na vyakula vyepesi kama biskuti, chipsi n.k.

Wanapenda ladha iwe nyepesi na viwe na pili pili na viungo vingi. wanapenda sana vyakula vinavyopooza au kutuliza njaa kama viazi, tambi na maziwa.

Huwa wanapenda sana ladha za uchachu kama limao limao au ndimu ndimu au mbilimbili vile vile wanapenda sana mkate na Jibini au vyakula vilivyo kaangwa kama nyama.

Wanatakiwa wawe waangalifu katika kula mafuta hasa vyakula vya kipuuzi puuzi ambavyo vinaweza kuwaletea madhara.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapenda sana tafrija, na vyakula wanapenda viwe vile vinavyotayarishwa mbele ya wageni na viwe vilivyokaangwa na vyenye ladha nzuri. Vyakula hivyo viwe ni vyepesi kutayarisha visivyopoteza muda.

NYOTA YA PUNDA (VIPAJI VYAO)

Wenye nyota hii wanapenda sana kupambana na maisha na wanakuwa na mambo mengi sana vichwani mwao kiasi kwamba wakati mwingine wanasahau vipaji vyao vya asili.
Tabia hiyo waliyo nayo haiwapi muda wa kufanya mambo mengine kama ya ubunifu. Kwa asili, wao ni watu wabunifu na wakati mwingine wanapata wasiwasi katika ubunifu wao.

Kuna wakati wenye nyota hii wanashindwa kutofautisha kati ya vipaji vyao na matakwa yao. ambayo yanakuwa makubwa na yenye shinikizo. Watapata msaada katika hili iwapo watafanya jitihada za maksudi za kuwasiliana na busara zao za asili kuwa kupata mapumziko na kufanya taamuli (Meditation).

Kipaji cha wenye nyota hii kinahusiana na kichwa ambacho ndio nyota yao inapotawala hivyo "Frenologia" (Ujuzi wa tabia ya mtu kwa umbo la kichwa chake iko chini ya nyota hii.

Kwa kuongezea wenye nyota hii wana kipaji cha kutafsiri ndoto na kipaji cha kusikia sauti ndani ya kichwa.

Kwa ujumla watu wa Punda wanapenda njia ya utabiri ambazo zinatoa matokeo ya haraka kama vile kutumia karata , dhumna, au dadu (dice).
Taamuli (meditation) ni jina au mbinu nzuri kwa wenye nyota hii kuongeza kipaji chao. Ikiwa watafanya taamuli kwa dakika ishirini wakati wa usiku au kitu cha kwanza wanapoamka asubuhi, akili na miili yao itatuliza. Hivyo itawafanya wawe na uwezo wa kutumia nguvu zao za kimwili na kiakili pamoja na kuendeleza au kukuza vipaji vyao.
{mospagebreak}

NYOTA YA PUNDA (BAHATI ZAO)

Watu wa nyota hii wana tabia ya kitoto ya kuamini kwamba mazuri yatatokea kwa amri ya Mungu. Kwa hiyo inawawia vigumu kufikiria uwezekano wa kushindwa katika jambo lolote.
Wakiwa ni waliozaliwa katika nyota yenye kuasisi mambo, wengi wao hudharau kutopata matumaini katika jambo moja na kurukia jambo lingine.
Kwa sababu shauku yao ni ya kuambukiza mara nyingi hufanikiwa kuwashawishi wengine wakubali kuongozwa nao hata kama kuna khatari.
Mara nyingi hawana muda wa kutoa mashitaka wala kuwaza makosa yaliyofanyika mwanzoni, wao wanaamini kwamba wakati wote mafankii yapo na kwa vile wamezaliw ana roho ya ujasiri wa kupenda vituko wako tayari wakati wowote kuyaweka maisha yao katika hatari ili wafanikiwe.

Tabia yao ya kutojali na misukumo au mihemko ya ghafla inawafanya wawe na sifa zilizokithiri za kubahatisha mambo.

Hakimu kwa bahati, hii kwao inakuw asiyo tatizo kwa sababu hawafanya kitu kimoja kwa muda mrefu, ghafla huwa wanarukia katika jambo lingine.

Watu wa Punda wana moyo wa ujasiri wa ushindani na wanafanya vizuri iwapo katika hali hiyo kutakuwa na uadui hasa mtu na mtu.

Katika michezo ya karata ua kupimana nguvu au kuwekeana dau watu wa Punda wana pata bahati sana.
Kwa ujumla watu wa nyota hii wanapenda kubahatika na wanachukia sana kukosa pamoja na kwamba faida zoa wanazopata zinalingana na hasara zinazowafika.

NYOTA YA PUNDA (URAFIKI)

Wenye nyota ya Punda ni wachangamfu, wanaosema kweli na wenye uwazi katika urafiki wao. Kama walivyo katika kila kitu kwenye maisha yao.
Ni wazuri katika kuanzisha urafiki, wakati mwingine wanakuwa wawazi sana katika mazungumzo yao na vitendo vyao kiasi kwamba huwaogopesha baadhi ya marafiki.

Kwa upande mwingine wao wanapendwa kwa sababu ya uaminifu wao na kusema kweli.

Watu wa Punda wanathamini sana uhuru wao na wanapenda kufanya vitu katika njia zao wanachukia sana kufugika au kuogopa watu kwa hiyo urafiki sio kitu muhimu kwa wenye nyota hii . wakati mwingine huwa wanajisikia furaha wanapokuwa katika kundi la watu wanaopenda vituko na mambo ya ajabu.

Watu wa Punda wako katika kundi moja na wale wenye nyota zenye asili ya moto na tabia zao zinafanana. Mfano wale wenye nyota ya Mshale wanakuwa marafiki wao wazuri ambao wanachangia tabia ya kupenda vituko.

Hata hivyo huwa hawapendi au hawaoni umuhimu wa kuwa na rafiki mwenye nyota ya Mapacha. Kwa wenye nyota ya Ndoo kwa vile wanathamini uhuru wao basi wao wanaweza kuelewana nao.

Watu wenye nyota zenye asili ya udongo Mbuzi, Ng'ombe na Mashuke wanakuwa marafiki wazuri wa Punda kwa Sababu wanamsaidia kutekeleza mipango yake kivitendo, pamoja na kwamba madhari na akili za hao Ngo'ombe, Mbuzi na Mashuke kupunguza nguvu ya urafiki wa kudumu.

{mospagebreak}
Kwa ujumla wote wenye nyota zenye asili ya moto mara kwa mara wanakuwa na tofauti na wenye nyota ya Punda hasa katika masuala ya ushindani mfano ni nyota ya simba na Punda wote huwa wananeemeka kutokana na uadui usioepukika katika urafiki wao, kama ikiwa katika kazi au nyumbani au kwenye starehe au wanapokuwa pamoja katika michezo.

NYOTA YA PUNDA (MITINDO)

Mitindo ya Punda ni yenye kuchangamka na nguo zisizo na madoido. Wanapenda wawe wanavaa kulingana na wakati. Mavazi yao huwa yanaambatana na mabegi, saa nzuri au mikufu na vito vyenye kupendeza.
Hata hivyo watu wa Punda hawapendi kupanga kununua au kushona nguo. Wanapendeza sana wakiwa katika mavazi ambayo ni mepesi kuliko nguo zile zilizosanifiwa na zenye madaha.

Suti zilizotafauti yaani suruali na koti tofauti, zikiambatana na buti pamoja na skafu na glavu ndio mavazi hasa na nyota ya Punda. Mavazi hayo yanaendana hasa na tabia yao ya ujasiri na mambo ya ajabu.

Wengi wenye nyota hii huwa wanapenda kuvaa suti za michezo ambazo pia zinaendana na namna yao ya maisha.

Wanapoamua kuvaa nguo, waume kwa wake wanakuwa wavaaji wazuri. Wanapenda nguo zilizoshonwa vizuri na zinazoeleweka.

Rangi zao zinakuwa Nyekundu na Njano na mara nyingi hupendelea nguo zisizo na nakshi.
Wanapenda mitindo thabiti na vitambaa ambavyo ni vyepesi kuvitunza. Wanawake wanapenda sana mikufu ya dhahabu na hereni za kuning'inia.
Kwa ujumla watu wa punda wanapenda kuvaa kulingana na mitindo na wanapenda nguo ambazo zinawafanya watu wakiwaona washituke wakiamua kuvaa nguo maalum basi mavazi hayo yataambatana na vitu vya ziada kama mikufu. Pete, saa visivyo ghali. Hiyo huwainawafanya waonekane na wakati katika mavazi ya aina yeyote.

NYOTA YA PUNDA (TASWIRA YA UMBO)

Inapofikia hali ya kuweka miili katika hali bora wenye nyota hii wana bahati kubwa kutokana na hali halisi ya maisha yao ya kujishughulisha. Kwa kuongezea labda wawe wanapenda kula lakini kama ilivyoanishwa na nyota yao ni watu ambao hawapendi sana vyakula vinavyoweza kuwaletea unene.
Hata hivyo wanafurahia chakula na wanapenda vyakula vyepesi. Kama ikiwa Kalori zinazoingia mwilini zinazidi zinazotoka basi uzito wao huongezeka.

Inapofikia hali ya kupunguza uzito wenye nyota hii wanakuwa hawana subira, wanapenda mlo ambao utapunguza uzito wao upesi na katika muda mfupi inavyowezekana ikiwa ni pamoja na kujiadhibu wenyewe kwa kujimyima chakula kwa muda mfupi wakiwa na imani yakupata matokeo.


Kwa wenye nyota hii muda wa siku chache au hata wiki moja ni muda tosha wa kujinyima chakula ili kupunguza unene.

Baada ya hapo ni juu yao kuwa na ratiba maalum ya ulaji wao ikiambatana na mazoezi ya kila siku, kama kuongelea, kukimbia, au kutembea kwa nguvu kwa muda mrefu wenye nyota hii wanahitaji mazoezi ya kila siku ili waweze kupunguza uzito. Vinginevyo itawawia vigumu baadaye.
{mospagebreak}
Kwa ujumla wenye nyota hii huwa wanapata uzito mkubwa kwa sababu huwa wanajishughulisha sana kula milo ya kawaida ikiambatana na vitu vitamu vilivyojaa Kalori wanapokuwa wamechoka.
Wanashauriwa kutumia muda wao kula tu milo ya kawaida hiyo itawasaidia kuondoa au kupunguza unene na kuboresha afya zao.

NYOTA YA PUNDA (USHINDANI NA UADUI)

Wenye nyota hii wanapenda sana ushindani na kuonyesha madaraka na uwezo wao, kwa sababu hii wanachukiwa na watu wengi. Wanapenda sana wawe wa kwanza na watatumia mbinu zozote ili wafanikiwe.

Punda wako wazi na waaminifu katika malengo yao ni watu wenye kusema ukweli na haamini visingizio, ulaghai wala kuficha siri.

Wanapenda kufanya mipango yao moja kwa moja na mtu yeyote akiingilia huwa unazuka ugomvi. Ikitokea hivi watu wa Punda huwaeleza wagomvi wao bila kuficha kinachoendelea.
Kutokana na ukweli na uwazi wao wenye nyota hii huwaudhi sana watu wengine kwa maneno yao na vitendo vyao.
Ni tabia yao kutojali hisia za watu na wala hawana muda wa kufikiri, maneno wanayosema au vitendo vyao vitawaathiri vipi wenzao.

Mara nyingi watu wa Punda, hushinda vita vyao kutokana na uwezo wao na nguvu zao za ukatili lakini ikitokea pakatakiwa kujieleza au kutoa hoja au diplomasia huwa wanashindwa kujieleza.

Wakiwa katika siasa hali ya uadui huibuka kutoka kila upande, wao huneemeka sana Kisiasa kutokana na upinzani na uadui mkali uliopo duniani ambao wao hufurahia.

Kwa ujumla watu wa Punda ni washindani katika sehehmu zote, ni madereva wanaopenda kwenda kasi hivyo wanapenda mashindnao ya magari. Mara nyingi watu wa nyota hii wanapenda michezo yenye ushindani au kutumia nguvu ikiwa kama jambo la kupitisha muda au kazi yake, na hii inawapa changamoto katika kuendeleza ushindani wao wa Asili.


NYOTA YA PUNDA (MANUNUZI)

Kama tulivyoona tangu mwanzo wenye nyota hii wanapenda ushindani, kushughulika na vitendo na hawapendi kabisa kufuata utaratibu kwa hivyo kununua vitu ni mojawapo wa mambo wanayoyapenda sana.
Vile vile wanapenda kupungua na kupanda kwa manunuzi au msisimko wa kwenda dukani katika mitaa inayopendeza au katika nchi za nje.
Wenye nyota hii wanapokwenda kufanya ununuzi hufanya juhudi ya kuamka mapema ili wawakwepe watu, na manunuzi yao wanayafanya haraka haraka.
Huwa wanakwenda kutoka duka moja hadi jingine wakizunguka kiuerevu kufanya manunuzi.

Wanapenda kununua vitu vya wiki nzima na orodha yao lazima vitakuwepo vyakula vya kupikwa kwa haraka au vya kuliwa papo kwa papo kama nyama za kopo au Samaki wa Kopo. Mara nyingi hawana muda wa kupika na hawapendi kutumia muda wao mwingi jikoni.


Kwa hiyo kitu ambacho hawa watu wa Punda wanapenda kununua. Jibu ni kwamba wanunue chochote ambacho kitaharakisha mwendo wa maisha yao.


Mfano wanapenda magari yanayo kwenda kasi au vitu ambavyo wanaviota, kama ramani, glavu za kuendesha gari na viatu.

Kwa ujumla watu wa Punda huwa hawapendi kwenda dukani kila siku lakini wanaona raha ikiwa kwa kufanya hivyo watapata ushindani.
Wanapenda kushindana na rafiki zao ili kuonyesha nani atanunua mwanzo na kitu kizuri au kubishana katika bei ya kitu fulani, hiyo inawafanya wajisikie raha sana.

[TABLE="class: ecxcontentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: ecxcontentheading"]Mawe ya nyota ya Punda Madini yake

[/TD]
[TD="class: ecxbuttonheading, align: right"]
[/TD]
[TD="class: ecxbuttonheading, width: 100%, align: right"]
[/TD]
[TD="class: ecxbuttonheading, width: 100%, align: right"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: ecxcontentpaneopen"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Mawe haya yafuatayo yote ni mawe ya nyota ya Punda na idadi yake ni tisa 9. Yote yanatumiwa na mtu mwenye nyota ya Punda kwa sababu mbalimbali. Soma maelezo ya matumizi ya mawe haya hapa chini ili uweze kujua zaidi namna ya kuyatumia.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Aventurine[/TD]
[TD] Bloodstone[/TD]
[TD] Carnelian[/TD]
[TD] Citrine[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Diamond[/TD]
[TD] Lapis Lazuli[/TD]
[TD] Lace Agate[/TD]
[TD] Quartz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD] Hematite[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Aventurine
"Mponyaji wa Roho na Moyo." Linaleta katika usawa nguvu za kiume na za kike, ubunifu, uongozi na furaha. Pia linasaidia katika kufikia maamuzi sahihi.
Jiwe hili lina uwezo wa kumfunika mvaaji katika blanketi la mapenzi.
Linakinga na kusaidia katika uponyaji wa magonjwa ya moyo, mapafu na adrenalini.


Bloodstone

Hili ni jiwe linaloleta nia na uwezo wa kufanikiwa, maisha marefu, nguvu ya mfano wa fimbo ya chuma pia linauwezo wa kuondoa ugumu wowote katika njia ya kutaka kufanikiwa.
Linaleta uaminifu na heshima katika uhusiano, kulirudisha tena penzi pamoja na kufuta madoa na vidonda vya penzi. Linampeleka mtumiaji katika maisha mazuri ya kimapenzi.
Linasaidia kutibu matatizo ya damu, mapafu, macho na moyo.

Carnelian

Malengo thabiti na msukumo. Jiwe hili linasaidia kuleta kwa mtumiaji kujiamini na ujasiri. Linahamashisha,linaanzisha uwezo binafsi na kuonyesha na kuamsha vipawa vilivyojificha vya mtumiaji.
Linauwezo wa kumlinda mvaaji dhidi ya mambo yote yasiyo mazuri na kutokujiamini.
Linasaidia kujikinga na kutibu Asthma (Pumu) na Shinikizo la damu.
{mospagebreak}


Citrine

"Jiwe la utajiri" linafungua na kuunganisha uwezo wa mtumiaji na uwezo wa kupata mafanikio katika alifanyalo ili kupata utajiri.
Ubunifu na uanzishaji, kudhibiti akili ili iweze kufikiria kwa mapana na marefu jambo linalotakiwa kufanyika ili liweze kufanikiwa. Pia huweza kudhibiti na kuongoza mawazo ili yawe yanawaza kufanikiwa katika mambo mbalimbali.
Linasaidia usagaji wa chakula katika mwili na mzunguko wa damu.

Diamond (Almasi)

"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi.
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.

Lapis Lazuli (Nili na zali)

Hili ni jiwe la "kurahisisha kipaji cha kutambua mambo". Lilitumiwa na Wamisri wa zamani kama kinga ya kuingia sehemu takatifu.
Lina uwezo wa kutakasa mwili na akili na kuondoa uchafu wote unaosababishwa na Mashetani na Mizimu. Vilevile linakufanya uwe na uhusiano mzuri na watu na unazipa nguvu sehemu zako za kinga ya mwili.

Mexican lace agate

Kuamsha nguvu za mwili. Lina uwezo wa kurudisha nguvu za mwili wakati unapojihisi kukosa nguvu ya kufanya baadhi ya mambo . Linafichua ukweli wa mambo (siri) na lina uwezo wa kumfanya mvaaji aweze kufahamu juu ya undani wa maisha na jinsi ya kuyashinda.
Linasaidia kutibu ngozi, moyo, uti wa mgongo na meno.

Quartz

Jiwe hili linakuza uwezo wa kutunza, malengo,kujirekebisha, kuhifadhi na na nguvu za kimwili na kiroho.
Linakuza uwezo wa kuhisi jambo kabla halijatokea. Pia lina uwezo wa kumfundisha mtumiaji kwa kadri ya uwezo wao na kasi zao. Vile vile linampa mtumiaji uwezo mkubwa wa mambo mbalimbali.

Hematite

"Jiwe linalotawala akili." Linamuwezesha mtu kukumbuka kitu vile kilivyo, uhakika, kusawazisha, na utulivu wa akili. Linaondoa matatizo au mambo yaliyo kinyume na kuyabadilisha na kuyafanya kuwa upendo.
Jiwe hili vile vile linaleta mapenzi, na uhusiano wa amani.
Pia linasaidia kuponya upungufu wa damu na uvimbe katika kichwa.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Ushauri wangu kwa kuwa wewe umezaliwa Tarehe 14/04 watu wa kuweza kushirikiana na wewwe kimaisha au kimapenzi ni watu waliozaliwa tarehe 9 au tarhe 18 au tarehe 27 hawa watu ukiwapata utashirikiana nao kwa mapenzi makubwa na mchumba wako awe amezaliwa tarehe kati ya
21Julai na 21 Agosti.mwaka wowote ule ndio atakaye kufaa kuwa mke wako au mume wako au rafiki yako wa ukweli na kuhus Pete utachaguwa wewe mwenyewe kito gani chenye faida na wew ndio utavalia pete yako. Ukiwa na shida mbali mbali na ushauri unaweza pia kuniandikia Email baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com Au pia wawezakunitembelea blog yangu bonyeza hapa http://mzizi-mkavu.blogspot.com.tr/





 
mkristo ni nani? na ni lini mlianza kuitwa wakristo?

usipanic njoo taratibu kuna somo leo utajifunza, naomba kudeclare mapema mimi siyo muislamu and over my dead body siwezi kuwa mwislamu.

Mkristo no kiongozi, aliongoza, anaongoza na ataongoza milele yote. Obama aulizwe Leo ni dini gani utasikia jibu lake.
 
Samahani kama unaamini ni uongo katafute wanaosema uongo wapate kukwambia,mimi siwezi kukwambia imekula kwako hiyo samahani sana sina muda wa kukwambia maneno ya uongo.

tena muongo mkubwa sana nyinyi kazienu kupotosha na kudanganya watu na kuwaingiza ktk ushirikina tu bas na kuwaibia pesa zao kwa ulaghai hana lolote
 
Mkuu MziziMkavu nashukuru kwa namna unavyojitoa kutuelimisha kwa kutupa uzoefu wako,maarifa na ujuzi mbalimbali katika mambo tofauti tofauti. Binafsi ni msomaji wa majukwaa karibuni yote na hupendelea zaidi aidha kuuliza ama kucoment kwa jambo lolote la kheri. Je,unaweza kunisaidia nami kwa tarehe hii 12January? Kinyota nikoje japo nafahamu kuwa niko Mbuzi.
Mkuu Mgaya D.W Kwa

tarehe 12January uliyonipatia nitakueleza nyota yako na baadhi ya ushauri mdogo kwa sababu

hukunipa mwaka uliozaliwa. ungenipa na mwaka uliozaliwa ningeweza kukuambia utafanikiwa

mwaka gani? lakini Tarehe na mwezi inatosha nikuambie mambo yatakayo kuwa katika maisha

yako Kinyota yako Soma hapa chini:



Capricorn.jpg


NYOTA YA MBUZI (CAPRICON)

  • Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 Dec na 19 Jan ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni SATURN (ZOHAL)
  • Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
  • Namba yao ya bahati ni 8.
  • Rangi yao ya bahati ni rangi ya Kijivu au Nyeusi.
  • Asili yao ni Udongo.

KIPAJI CHA MBUZI(GRADUAL)

Wenye nyota hii wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni.

TABIA ZA MBUZI

Wale wote waliozaliwa katika nyota hii ni watu ambao wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata kama ikiwa ni ya kipuuzi.
Ni viumbe waaminifu sana na ni watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote.
Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu.

TABIA YA MBUZI KATIKA MAPENZI

Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.

Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.

Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.
Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.

TABIA YA MBUZI KATIKA FEDHA


Kwa watu wenye nyota hii fedha ni kitu muhimu sana katika maisha.

Watu wa Mbuzi wanaamini kabisa kwamba fedha ndio zitawapa uwezo wa kuweza kupambana au kukabiliana na mazingira ya Dunia, hivyo basi suala lolote la fedha na mali wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana.
Inawachukua muda mrefu kutekeleza malengo yao ya kifedha lakini wakishazipata basi huwa hawatetereki tena. Wana uwezo wa kuhifadhi walichonacho.

Ni watu wabahili sana na hata kama wakiwa na fedha nyingi utaona wanaishi maisha ya kawaida na wala huwezi kuwajua.

Fedha zao zinatoka kwa sababu maalum ya dharura na wala siyo katika starehe au vinginevyo na hiyo ni kwa sababu hupenda kukumbuka walikotoka katika hali ya umasikini au ufukara.
{mospagebreak}

MAVAZI YA MBUZI

Wenye nyota ya Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi.
Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.
Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi.
Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi.

MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi.
Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha.
Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu, nguvu nyingi, na akili hutumika.
Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi kama Baridi Yabisi (rheumatism).
Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa.

KAZI ZA MBUZI

Wenye nyota ya Mbuzi kitu muhimu katika maisha yao ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao.
Ni watu ambao wanazingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani.
Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.
Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.

FAMILIA ZA MBUZI

Wazazi wenye nyota ya Mbuzi ni watu ambao wamepangilia kabisa mipango ya watoto wao kabla hawajazaa.
Ni wazazi ambao wanayachukulia kwa uzito mkubwa majukumu yao ya kulea na hawakubali kabisa watoto wao kufanya michezo michezo ya kipuuzi. Wanapenda kuwahimiza watoto wao kuwa na malengo ya maana.
Wanapenda sana nidhamu katika familia zao.
Mara nyingi wazazi wa kiume huwa hawapati muda kuwa na watoto wao kutokana na kazi nyingi walizonazo lakini kwa wazazi wa kike wanakuwa wanatumia akili ya hali ya juu katika kutatua matatizo au hisia za watoto wao.

MADINI YA MBUZI

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinayoitwa Black Jet.
Jiwe hili inaaminiwa lina uwezo wa kuongeza ujasiri na kumletea mvaaji mafanikio ya kibishara.

UHUSIANO WA KIMAPENZI (MBUZI NA KAA)

Tabia ya Mbuzi ya ubahili na kutopenda anasa hulainishwa na tabia ya Kaa ya upendo, mapenzi na huruma.

VYAKULA VYA MBUZI

Wenye nyota ya Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo. Ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao.
Wapende sana vyakula vya Nazi na Nyama yeyote.
Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba (Shellfish).

NCHI ZA MBUZI

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi.
Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India.

RANGI ZA MBUZI

Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi

MADINI AU VITI UTAKAVYOTAKA KUVAA KWENYE PETE ZAKO ZA BAHATI HIVI HAPA:

Mawe haya yafuatayo yote ni mawe ya nyota ya Mbuzi na idadi yake ni matano 5. Yote yanatumiwa na mtu mwenye nyota ya Mbuzi kwa sababu mbalimbali.
Soma maelezo ya matumizi ya mawe haya hapa chini ili uweze kujua zaidi namna ya kuyatumia.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Diamond[/TD]
[TD] Tiger eye[/TD]
[TD] Malachite[/TD]
[TD] Quartz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD] Garnet[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Tiger eye

Jiwe hili lina uwezo wa kutengeneza hali nzuri sehemu ambayo kuna machafuko. Linaleta amani na maelewano, kusawazisha hisia, huleta hali ya kuwa makini na uthabiti kwa mtumiaji.
Inaboresha hisia za nafsi na uwezo wa kutambua mambo, linavuta urembo, uzuri, wingi wa vitu na hekima.
Jiwe hili linasaidia kuponya vidonda, michubuko, macho na koo.

Malachite

"Kubadilisha". Mponyaji mwenye nguvu, jiwe hili lina uwezo wa kuondoa maradhi moja kwa moja. Linasafisha na kuonyesha njia ya wazi ya kufanya mambo. Linasaidia katika kufanya mambo ambayo moyo unayataka ili yawe ya kweli na yatokee.
Jiwe hili la Malachite lina uwezo wa kuupa nguvu mwili wa kujua mambo bila kuambiwa na kujua chanzo cha tatizo. Linalinda dhidi ya mnunurisho.

Garnet

Jiwe la kujitoa kwa ajili ya watu wengine, binafsi na katika malengo ya binafsi. Linaamsha "moto wa ndani" wa ubunifu. Linatoa ufufuo wa usawa kwa mtumiaji. Linahamasisha mapenzi na hisia kali za kimapenzi.
Jiwe hili linavuta bahati nzuri, ulinzi dhidi ya uchafu wenye sumu. Linakinga dhidi ya huzuni, mfadhaiko, upungufu wa damu na matatizo mbalimbali ya mwili.

Diamond

"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi.
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (Diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.

Quartz

Jiwe hili linakuza uwezo wa kutunza, malengo,kujirekebisha, kuhifadhi na na nguvu za kimwili na kiroho.
Linakuza uwezo wa kuhisi jambo kabla halijatokea. Pia lina uwezo wa kumfundisha mtumiaji kwa kadri ya uwezo wao na kasi zao. Vile vile linampa mtumiaji uwezo mkubwa wa mambo mbalimbali.


USHAURI WANGU BINAFSI KWAKO WEWE:

Kwa Tareh ya
12January wewe ukita mke itabidi umpate Mke aliyezaliwa Kutoka Tarehe 21 Juni na tarehe 20 July ya mwaka wowote. Ndie atakaye kuwa mke wako wa kimaisha mnutaelewana nae

sana na kupata baraka kindoa na kifamilia. Na kama una Marafiki pia waliozaliwa hizo Tarehe waweza

kushirikiana nao kimasha mukaelewana. Na pia Ukipata Marafiki waliozaliwa tarehe hizi hapa mojawapo tarehe 3 au tarehe 12 au 21 au tarehe 30 itakuwa ni vizuri sana kushirikiana nao kimaisha. Ukiwa na Tatizo lolote la kimaisha unataka nikutatulie unaweza kuniandia kia kwa baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com au pia waweza kunitembelea blog yangu ukapata faida katika maisha yako bonyeza hapa.
http://mzizi-mkavu.blogspot.com.tr/
 
Last edited by a moderator:
Haha mtanzania usiweke maneno ambayo sijayasema, nani kasema anakimbilia kutafsiri vingine?
alafu nani kajilinganisha na Yesu au Muhammad? haha, kwa hiyo utabiri wa hawa wawili ulitabiriwa kwa nyota? au ndo utaanza na wewe story za ile nyota ya Yesu iliyotoa guidance?

Haya tufanye mo mjinga, em nambie hizo nyota ndo zinafanyeje kazi? nimekwambia unipe convincing statement ili nikuamini ila hujanipa hata moja,

Ndio maana nikakushauri hebu jaribu kutulia ufanye utafiti,soma link nimekupa kuhusu galileo na inaelezea nyota inavyofanya kazi ukiacha jinsi galileo alivyojihusisha na nyota.

maelezo ya ziada kuhusu nyota yako ningekushauri uwafuate maexpert ambao ni profession yao kama akina mzizimkavu

Halafu kama unakubali huwezi kujilinganisha na akina Yesu na ujio wao ulishaonekana angani na wazee wa nyota,nakushauri ukachunguze zaidi hii elimu ni pana sana hata mimi sijisifu kuwa nipo deep kwani sio profession yangu na huwa natafuta ushauri wa kinyota,ila ninajua umuhimu wa nyota na historia yake na jinsi inavyoathir maisha ya binadamu na nimeona ukweli ndani yake.
 
Akhsante, Mzizi mkavu kwa majibu ya kina, je mtu aliyezaliwa 17/06/75 naye anawezafanikiwa mwaka gani? na anatofauti gani na yule aliyezaliwa tarehe hizohizo lakini mwaka 87?
 
Thanks in advance Mkuu MziziMkavu nimeweza kuchota kitu kutokana na majawabu yako na kwakweli niseme tu dhahiri mwenyezi Mungu akubariki sana kwa yote ufanyayo na hasa kwa namna unavyoweza kutupa uzoefu na kushare nasi what you have.
 
Mkuu MziziMkavu na mimi naomba ushauri wako.mwaka wangu huo hapo 85/11/19
Kutokana na Tarehe yako ya kuzaliwa Tarehe 19/11/1985. Wewe utafanikiwa kimasiha yako yatabadilika kutoka hapo ulipo kunako mwaka 2018 mambo yako yatakuwa mazuri utapata pesa na kila unalo taka utapata kwa hivi sasa pia jitahidi sana usilegeze kamba. soma chini maelezo ya nyota yako.



NYOTA YA NG'E (SCORPIO)


  • Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na 21 Novemba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
  • Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
  • Namba yao ya bahati ni 9.
  • Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
  • Asili yao ni MAJI.


KIPAJI CHA NG'E (MYSTICAL)

Wenye nyota hii wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji.

TABIA ZA NG'E

Wenye nyota ya Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni watu wenye uelewa mkubwa na ni majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Ni wenye tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.

Ni watu wenye tabia ya siri na wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana.Wenye nyota hii kama ilivyo alama yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.

Ni watu wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Watu wa Nge vile vile wana tabia au wanaweza kujidhuru wao wenyewe.Mambo yanapowawia magumu.

TABIA YA NG'E KATIKA MAPENZI

Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.

Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.

Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
{mospagebreak}

TABIA YA NG'E KATIKA FEDHA

Hakuna kitu kinachoshindikana kwa wenye nyota hii, na chepesi zaidi ni namna ya kupata fedha. Wana uzoefu mkubwa wa kuhimili matatizo ya kifedha wanapoanguka, hata wakiwa matajiri na wakafilisika.
Watu wa Nge wana bahati ya kuvumbua fedha au utajiri katika njia ambazo watu wengine si rahisi kugundua.

Ni watu ambao sio rahisi kudanganyika wakiona mpango wowote wa kifedha. Mara nyingi ni kawaida yao kuchukua kitu au kufanya mradi ambao wengine wanauona wa kipuuzi na wakaugeuza kuwa wa thamani kubwa.

Ni wakarimu sana wanapokuwa na fedha, na hawapendi kujidai kwa utajiri wao. Wako tayari wakati wowote kuwatumia watu wengine kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla wao ni wataalamu wa kutafuta fedha katika njia ambazo watu wengi hawazifahamu.

MAVAZI YA NG'E

Wenye nyota ya Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong'ara, zenye kuonekana na maridadi,zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja.
Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta.
Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.

MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi(cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).
Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono. Wakati mwingine hisia zao zinakuwa kubwa sana kiasi kwamba wao wenyewe wanajishuku vibaya.

Inapotokea hivi wanahitajika kusafisha miili yao kwa fadhaa iliyowajaa kutokana na mfadhaiko wa hisia zao.

Kwa ujumla ni watu wenye afya nzuri na wanapona haraka maradhi yanayowasumbua. Wenye nyota hii wana tabia ya aidha kula, kunywa au kuvuta kupita kiasi au wengine hawafanyi mambo hayo kabisa.
Kwa vile nyota hii inatawala sehemu zinazoondoa uchafu wa mwili ni vizuri watu wa Nge wakawa waangalifu na mambo yanayochafua mwili wao.

Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.

{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'E.

Nyota ya Nge ambayo alama yake ya asili ni Maji ni nyota mojawapo ya nyota zenye nguvu katika mambo ya kikazi.
Ni watu wenye milipuko ya hisia wanapokuwa katika miradi yao ya kazi. Wanafanya shughuli zao kwa hisia kali na hamaki na wanategemea wapate majibu ya kuridhisha.
Ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni watu waerevu na wenye kung'amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono.

FAMILIA ZA NG'E

Wazazi wenye nyota ya Nge ni watu ambao wanaonyesha utulivu wa hali ya juu. Kimaumbile huwa hawaonyeshi hisia walizokuwa nazo juu ya watoto wao, wanaweza wakawa na chuki kubwa lakini hawapendi kuiionyesha.
Kwa ujumla wazazi hao wanapenda watoto na wanatumia muda mwingi na hisia zao kuwangalia na kuwadhibiti watoto wao.
Pamoja na ukarimu wao ni wazazi wenye kupenda nidhamu na wanataka watoto wao wafuate maadili mema. Wazazi hao walivyokuwa wadogo wamepitia ujanja wote hivyo hawakubali watoto wao wawadanganye.
Watoto watagundua kwamba wazazi wao ni watu wa kutisha na kuogopwa lakini uhusiano wao unakuwa ni mzuri. Wazazi wa kike wanakuwa na hisia kali kwa watoto wao kitendo ambacho kinawafanya watoto wawe katika shinikizo.

MADINI YA NG'E

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa BERYL NA RED CORNELIUS. Mawe haya yenye rangi ya damu ya mzee (Maroon) na rangi Nyekundu yanaakisi au kuashiria asili ya Nge ya uhusiano wake wa asili na kitu chochote cha miujiza na uchawi.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(NG'E, NG'OMBE)
Tabia ya Nge ya wasiwasi, wivu, hisia kali za kimapenzi na dhana mbaya kwa wapenzi wao hutulizwa na kuzimwa na nyota ya Ng'ombe ambao wana tabia ya utulivu, uaminifu, wasioyumba na wanaopenda kusikiliza wanayoambiwa.

VYAKULA VYA NG'E

Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

NCHI ZA NG'E

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
Miji hiyo ni Liverpool(Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

RANGI YA NGE

Wenye nyota hii wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).

PETE ZA MAWE YANAYO KUFAA KWA AJILI YA NYOTA YAKO NI HAYA HAPA:


MAWE YA NYOTA YA NGE:


Mawe haya yafuatayo yote ni mawe ya nyota ya Nge na idadi yake ni Kumi 10. Yote yanatumiwa na mtu mwenye nyota ya Nge kwa sababu mbalimbali.
Soma maelezo ya matumizi ya mawe haya hapa chini ili uweze kujua zaidi namna ya kuyatumia.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Ruby[/TD]
[TD] Rhodochrosite[/TD]
[TD] Kunzite[/TD]
[TD] Moldavite[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Diamond[/TD]
[TD] Opal[/TD]
[TD] Selenite[/TD]
[TD] Quartz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
ImageProxy.mvc
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD] Unakite[/TD]
[TD] Topaz[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ruby

"Malkia wa mawe yote". Jiwe la mapenzi, linamzungushia mtumiaji hali ya uzuri na lina uwezo mkubwa wa kubadilisha muonekano wa mtu.
Linamlinda mtumiaji dhidi ya mambo yote mabaya, kuumia na maradhi. Linavuta uimara, uthabiti, kuimarika, uaminifu, utiifu na uwajibikaji. Inaaminiwa kuwa kama hili jiwe litakuwa ni la duara basi utajiri ni lazima utaupata.
Jiwe la Ruby linatoa mtikisiko wa joto linaloponya; na kwa mujibu wa habari za kale, iliaminiwa kuwa jiwe hili linauwezo wa kutoa joto(moto) lekundu ambalo lina uwezo wa hata kuchemsha maji, ambalo lina uwezo wa kugeuza na kubadili moto wa mapenzi.
Jiwe hili linasaidia kuponya moyo, uchafu wote katika damu na kuondoa sumu mwilini.

Rhodochrosite

Jiwe hili linaitwa "Mwalimu wa Kimalaika wa mapenzi na usawa", linaunganisha na kuleta uwiano kwa mume na mke na lina uwezo wa kukuvutia mpenzi wa uhakika kwa yule anayelivaa na kukupa uwezo wa namna ya kupenda.
Jiwe hili linahamasisha mapenzi ya kujipenda wewe mwenyewe na dunia kwa ujumla.

Kunzite

"Jiwe la Umoja" Jiwe lianunganisha moyo, kichwa na koo na linakuwezesha kuwa na hisia za mapenzi, ufahamu na uwezo wa kujieleza. Linauwezo wa kuusafisha mwili na vile vile linakuwezesha kuzungumza mbele za watu na uhuru wa ndani ya mwili na pia linatibu Moyo.
{mospagebreak}

Selenite

"Jiwe la mchawi" Jiwe hili linauwezo wakukupa wewe mvaaji uwezo wa kujua matatizo ya mtu na kumtibu. Linasaidia na kusafisha uti wa mgongo na kutibu maradhi ya kigeugeu, vile vile linatibu magonjwa yasiyotibika.

Moldavite

"Mponyaji kutoka ulimwengu mwingine" Linauwezo wa kumuwezesha mtumiaji kuwasiliana na Falme za juu mbinguni. Linatoa nuru na mwanga katika mawasiliano na mbingu nyingine.
Linamtayarisha mtumiaji kwa ajili ya kujibadilisha kwa ajili ya kupaa katika mbingu nyingine. Lina uwezo wa wa kupitisha nuru maalum ambayo inataka kufanana na miale ya leza (Laser beam) ambayo ina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Opal

Hili ni jiwe linalomuwezesha mtu kupata maono mbalimbali. Linaongeza nguvu za kujua mambo kabla hayajatokea. Lina uwezo wa kumuonyesha mtumiaji mambo mengi yaliyojificha katika nafsi za watu, linavuta nguvu za utambuzi, na ubashiri.
Hili jiwe la Opal linamfunika mtumiaji kwa usiri, mambo ya siri na haiba kubwa. Jiwe hili lina uwezo wa kumsaidia mtumiaji kutoweka na kutokuonekana anapoamua kufanya hivyo.
Linatibu maambukizo mbalimbali, linaponya na kuwezesha macho kuona zaidi pia linasaidia katika kazi za umetaboli (uwezo wa mwili kusaga chakula)

Diamond

"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi.
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.

Quartz

Jiwe hili linakuza uwezo wa kutunza, malengo,kujirekebisha, kuhifadhi na na nguvu za kimwili na kiroho.
Linakuza uwezo wa kuhisi jambo kabla halijatokea. Pia lina uwezo wa kumfundisha mtumiaji kwa kadri ya uwezo wao na kasi zao. Vile vile linampa mtumiaji uwezo mkubwa wa mambo mbalimbali.

Unakite

Tiba ya kibinafsi. Jiwe hili linasawazisha hisia na linatumainisha Pendo Kuu.
Linatayarisha na kusaidia katika namna ya kuzaliwa upya na katika namna halisi ya kuzaliwa kwani jiwe hili lina uwezo wa kuchangamsha tiba ya njia ya uzazi na lina uwezo wa kufichua sababu za maradhi.

Topaz

"Jiwe la jua" linasaidia mtumiaji kuwaza na kutimiza ndoto zake. Jiwe hili linatoa joto na mwanga wenye nguvu za kisumaku za kuponya, kuondoa wasiwasi na mashaka, maumivu na maradhi.
Lina uwezo wa kuvuta mapenzi na mafanikio pia kuwasiliana na milki nyinginezo.
Linasaidia kuvunja kuganda kwa nguvu za mwili na katika kuondoa uchafu wa sumu katika mwili.

USHAURI WANGU:

Kutokana na wewe umezaliwa Tarehe
19/11/1985 Mke atakaye kufaa wewe kumuowa ni yule mwanamke aliye zaliwa Tarehe 21 April na May 20 ya mwaka wowote ndie atakaye kuwa mke wako wa milele na utakuwa nae baraka tele mtafute mke mwenye kuzaliwa hiyo tarehe kutoka tarehe 21 April au 22 April au 23

Aprilau 24April mpaka mwisho wa Tarehe 20 May mwanamke yoyote yule aliyezaliwa tarehe hizo moja wapo ndie atakaye kufaa kuwa mke wako mutasikilizana sana. Na Watu wa kushirikiana nao kimasha au kiurafiki ni watu

waliozaliwa Tarehe 1 au tarehe 10 au tarehe 19 au tarehe 28 Mwezi wowote ule. Pete nitakayo kushauri utafute na uvae tafuta pete yenye kito cha Ruby ndio itakayo kufaa au pete yenye kito cha (
BERYL NA RED CORNELIUS)

ukipata pete yenye hicho kitu nitafute nitaweza kukupa ushauri jinsi ya namna ya kuitumia kwake.
Unaweza pia kuniandikia baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com Au pia unaweza kunitembelea kwenye blog yangu ukapata faida nyingi bonyeza hapa http://mzizi-mkavu.blogspot.com.tr/


 

Attachments

  • Scorpio-Art-scorpio-for-life-36885723-806-992.jpg
    Scorpio-Art-scorpio-for-life-36885723-806-992.jpg
    177.3 KB · Views: 432
Akhsante, Mzizi mkavu kwa majibu ya kina, je mtu aliyezaliwa 17/06/75 naye anawezafanikiwa mwaka gani? na anatofauti gani na yule aliyezaliwa tarehe hizohizo lakini mwaka 87?
Kwa Mtu aliyezaliwa Tarehe (17/06/75) Atafanikiwa mwaka 2023. Na Mtu aliyezaliwa Tarehe 17/06/87 atafanikiwa mwaka 2017.
 
Duh! Sasa mbona mwaka 2023 kwa mtu aliyezaliwa 75 ni mbali sana anawezaje au afanye nini ili iwe karibu na sio mbali hivyo?n Na huyu akitaka kupata mafanikio mapema zaidi afanye nini? na Nyota yake mbona hujaidadavua kwa undani?
 
Kwa wakristo BIBLIA TAKATITU imekataza kufuata utabiri wa nyota na mengine yafafananayo na hayo sijui kwa jirani zetu wa kibla

Mbona wale mamajusi waliifuta nyota mpaka wakafika mahali yesu alipozaliwa mambo haya yapo yalikuepo na yataendelea kuwepo
 
MziziMkavu
Thanks sana mkubwa nimekuelewa vzuri sana na nitaanza kufuatilia ila kwenye hayo mawe mbona kila moja naliona linanifaa na muhimu kwangu na yapo sita inakuwaje? Na je vp mwaka gani nitafanikiwa ninachokihitaji? Nimezaliwa 1980
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu

Thanks sana mkubwa nimekuelewa vzuri sana na nitaanza kufuatilia ila kwenye hayo mawe mbona kila moja naliona linanifaa na muhimu kwangu na yapo sita inakuwaje? Na je vp mwaka gani nitafanikiwa? Nimezaliwa 1980
 
Last edited by a moderator:
Thanks sana mkubwa nimekuelewa vzuri sana na nitaanza kufuatilia ila kwenye hayo mawe mbona kila moja naliona linanifaa na muhimu kwangu na yapo sita inakuwaje? Na je vp mwaka gani nitafanikiwa? Nimezaliwa 1980
Kutokana na wewe umezaliwa mwaka 1980 mara ya mwisho ulifanikiwa au mambo yako yalikuw animazuri mwaka 1999 na utafanikiwa mnapo mwaka 2027 kama bado utakuwa upo hai inshallah. Ukiwa na Tatizo lolote au shida yoyote waweza kuniandikia Baruwa ya Pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com au waweza kunitembelea Blog yangu bonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
mkuu Mzizi mkavu nataka kujua hivi vito hata ukiwa nacho mfukoni kazi yake si sawa tu na kuvaa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom