Mkuu wa chuo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 7,620
- 5,335
Hapana maana ya Kafiri siye aliyekufuru kumbuka hilo fungu la Yuda nililokupa ni la muda mrefu kabla hata kina Sayyidina Abubakari, Umari, Uthumani na Ali hawajaandika Qurani na wala Uislamu haujaanzishwa na Muhammad hajazaliwaSafi sana Mkuu wa chuo. Napenda sana ukiambatanisha na aya kwa hoja zako.
JIBU.
Hapana simkubali Yesu kristo, na kafir maana yake ni aliekufuru.
Ni nani aliekufuru?
Jibu:
QURAN 5:72-73
72. Hakika wamekufuru
walio sema: Mwenyezi
Mungu ni Masihi mwana
wa Maryamu!
Na hali Masihi
mwenyewe alisema: Enyi
Wana wa Israili!
Muabuduni Mwenyezi
Mungu, Mola wangu
Mlezi na Mola wenu
Mlezi. Kwani anaye
mshirikisha Mwenyezi
Mungu, hakika Mwenyezi
Mungu atamharimishia
Pepo, na mahala pake ni
Motoni...
Mkuu wa chuo najua huamini Qurani.
Sasa msikilize unaemwita Mungu yeye anasemaje ili ujue kati mimi na wewe nani kafiri.
Marko 12 18.
Bwana Mungu wetu ni bwana mmoja.
Yohana 5 30.
Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.
Yohana 20 17.
Ninaapa kwenda kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
Kabla hatujaendelea naomba uniambie ni kwa namna gani unaiamini biblia.
Jee unaamini aya zote?
Au unaamini baadhi na kuacha baadhi?
kwa hiyo kwa maana hiyo katika hilo fungu yule anayemkana Bwana wetu Yesu Kristo ni Kafiri, kwa maana hiyo wewe ni Kafiri kwa muktadha huo, kwa sababu hilo sio neno geni na wala alijaanzia kwenye Quran, na Biblia ilikuwepo kabla ya Quran
KAFIRI (KAFIRUNA) ni neno la kiarabu lenye maana ya MPINGAJI yaani anayepinga maneno ya Mwenyezi Mungu, nitatoa mfano, ili kuwe na mpingaji yaani KAFIRI ni lazima kuwe na kauli tangulizi iliyo tangulia , kusema kwa hiyo Kauli itakayofuata ya kupinga inaitwa kauli ya MPINGAJI kwa kiarabu KAFIRI, angali huu mfano
Mwanzo 2:16-17
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Angalia hapo kwenye bold hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu, sasa angalia kauli ya shetani hapa chini
Mwanzo 3:1-4
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Angalia hapo pia kwenye bold hiyo ni kauli ya Ibilisi
kwa hiyo kauli iliyofuata baada ya kauli tangulizi. Huyo ni Kafiri, Mungu alisema ukila UTAKUFA HAKIKA akaja Ibilisi akasema ukila HUTAKUFA HAKIKA, kwa hiyo kauli iliyofuata ya kupinga maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya UPINGAJI, kwa hiyo Ibilisi ni KAFIRI wa kwanza
Quran 38:4 Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
Angalia hiyo aya kutoka kwenye Qurani, kulingana na hiyo aya makureshi wa kabila la Muhammad ambalo ni makafiri, alipowaambia kuwa yeye ni mtume walistaajabu ndipo waliposema huyu ni mchawi na muongo, walimpinga kwa kuwa wanajua huyu ni miongoni mwetu, kwa hiyo Muhammad alikuwa miongoni mwa makafiri
Halafu kuhusiana na swala la Biblia naiamini...
Okay tuendelee...