Maiti ya Mchungaji John Chida iliyosubiriwa ifufuke kwa miezi miwili yazikwa Iringa, Agnes Mwakijale anashikiliwa na Polisi kwa kuishi na Maiti

Maiti ya Mchungaji John Chida iliyosubiriwa ifufuke kwa miezi miwili yazikwa Iringa, Agnes Mwakijale anashikiliwa na Polisi kwa kuishi na Maiti

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la El-Huruma (E.H.C), John Chida aliyetarajiwa kufufuka, umezikwa leo Desemba 6, 2024 katika makaburi ya Mlolo Manispaa ya Iringa.

Mwili wa mchungaji huyo ambaye alifariki dunia Oktoba, uligunduliwa Desemba 3, mwaka huu ndani ya nyumba yake ukiwa na muumini wake, Agnes Mwakijale ambaye alikaa naye akiamini angefufuka.

Pia, Soma: Iringa: Mwili wa Mchungaji aliyefariki Oktoba 2024 wakutwa ndani. Waumini wake waliamini hawezi kufa bali atalala tu

Agness anashikiliwa na polisi mkoani Iringa, akidaiwa kuishi na maiti hiyo kwa miezi miwili.
GeHeWiMWoAAWaER.jpg
 
Imani nzuri ikiwa ya kiasu ikizidi ni hatari mtu kujilipua haoni shida

Biblia kuna kifungu kinasema kuwe na kiasi kwa kila kitu
 
Kwa nini polisi hawajampeleka huyo Agnes hospitali ya wagonjwa wenye akili mpaka sasa??
 
Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la El-Huruma (E.H.C), John Chida aliyetarajiwa kufufuka, umezikwa leo Desemba 6, 2024 katika makaburi ya Mlolo Manispaa ya Iringa...
Aisee! Hili kanisa linapatikana ir. tu??
 
Hii nchi inawajinga wengi sana.
Na sioni kama Agnes anaenda kutiwa hatiani hapo.
 
Hawa ndugu zetu wanatia aibu sana imani. Kwa matokeo haya atakuwa amewapotosha vya kutosha waumini wake kawalisha mafundisho potofu ya imani.

Unakuta mwingine hataki kwenda hospitalini kutibiwa akiamini atapona bila kutibiwa na binadamu. Dhana ya imani hupotoshwa kunapokuwa na mafundisho yasiyo sahihi
 
Wange muacha tu, kwani alileta kero kwa wengine ,mbona watu wanazika ndani wangemuacha waone mwishowe
 
maiti iliweza kukaa vipi miezi 2 bila kuharibika? hii habari ina ukakasi
 
Back
Top Bottom