Maiti za wanajeshi wa Afrika Kusini zasafirishwa kupitia Rwanda

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Baada ya sintofahamu iliyotokea kuhusiana na usafirishaji za maiti za wanajeshi wa Afrika Kusini waliokufa wakipigana na kundi la waasi la M23, hatimae wamesafilishwa kupitia Rwanda.

Kamati ya bunge ilipokua ikimhoji waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi, walitangaza kwamba Rwanda ilikubali kutoa njia ili wasafirishwe, nchi yao ikakataa. Leo, gari lililobeba maiti hizo, limepitia mpaka wa Goma, La corniche, kuelekea mpaka wa Cyanika, wa Rwanda na Uganda. Itasafirishwa kwenda Kampala, kwa ajili ya safari kuelekea Afrika Kusini.

Baada ya sintofahamu iliyotokea kuhusiana na usafirishaji za maiti za wanajeshi wa Afrika Kusini waliokufa wakipigana na kundi la waasi la M23, hatimae wamesafilishwa kupitia Rwanda.

Kamati ya bunge ilipokua ikimhoji waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi, walitangaza kwamba Rwanda ilikubali kutoa njia ili wasafilishwe, nchi yao ikakataa. Leo, gari lililobeba maiti hizo, limepitia mpaka wa Goma, La corniche, kuelekea mpaka wa Cyanika, wa Rwanda na Uganda. Itasafilishwa kwenda Kampala, kwa ajiri ya safari kuelekea Afrika Kusini.

View: https://x.com/Mamaurwagasabo1/status/1887814434908762398

Je, ni kwamba hakuna njia nyingine ya kuingia goma ama kutoka goma zaidi ya Rwanda? Naona kila anaetoka goma anapitia Rwanda.
 
Ukiwa Goma, mpaka wa ardhini ulio karibu ni wa hapo(ipo miwili), ipo umbali wa kama km3 )kati ya mpaka na mwingine. Ili uende Burundi, lazima uende Kivu kusini(kupitia ardhini au majini)ambapo ni mbali. Japo na kutoka Bukavu kwenda Goma, wengi hupita Rwanda maana ndo karibu. Kwa airoprt, Kigali ndo ipo karibu ukiondoa ya Goma. Km 165 hivi.
 
Miili na mabaki ya wanajeshi wa Tanzania, Afrika Kusini na Malawi waliopoteza maisha Kongo imerejeshwa kupitia Rwanda ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=eRNJ6k5Bqao

Nchi za Afrika Kusini, Malawi na Tanzania kwa kushirikiana na Rwanda wafanikiwa kurudisha miili ya wanajeshi wao waliokuwa kwenye jeshi la nchi za SADC huko Mashariki ya Kongo.
 
Ukiwa Goma, mpaka wa ardhini ulio karibu ni wa hapo(ipo miwili), ipo umbali wa kama km3 )kati ya mpaka na mwingine. Ili uende Burundi, lazima uende Kivu kusini(kupitia ardhini au majini)ambapo ni mbali. Japo na kutoka Bukavu kwenda Goma, wengi hupita Rwanda maana ndo karibu. Kwa airoprt, Kigali ndo ipo karibu ukiondoa ya Goma. Km 165 hivi.
Pia mji wa Goma uko karibu na mji wa Gisenyi ( Rwanda)
 
Update za kubomoa madaraja mpaka wa burundi kaskazini,na sababu 'haswa'!?

Kuna askari watoro wa jeshi la Burundi wanakimbia kutoka Bukavu Kongo na silaha zao, wanaweza kuingia na silaha hivyo ni kufanya ugumu watoro hao wasio na nidhamu za kijeshi kuingia Tanzania na kufanya tatizo la kiusalama au kutumia ardhi ya Tanzania kuishambulia Rwanda na kuleta tatizo la kidiplomasia n.k
 
Acha waishambulie hata wakiwa Tz, then Rwanda arudishe majibu.
 
Baada ya sintofahamu iliyotokea kuhusiana na usafirishaji za maiti za wanajeshi wa Afrika Kusini waliokufa wakipigana na kundi la waasi la M23, hatimae wamesafilishwa kupitia Rwanda.

Kamati ya bunge ilipokua ikimhoji waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi, walitangaza kwamba Rwanda ilikubali kutoa njia ili wasafilishwe, nchi yao ikakataa. Leo, gari lililobeba maiti hizo, limepitia mpaka wa Goma, La corniche, kuelekea mpaka wa Cyanika, wa Rwanda na Uganda. Itasafilishwa kwenda Kampala, kwa ajiri ya safari kuelekea Afrika Kusini.

View attachment 3227884
😅😅😅hawana hata Ndege?

Viongozi wa Afrika wanapenda sisi tufe tukiwa tunawatumikia ila hawajali kabisa.

Angekuwa hata Mke au ndugu wa Waziri wa SA angesafirishwa kwa gari?
 
Mamlaka nyingi UN, MONUSCO, SAMIDRC, AU, SADC na nchi husika South Africa, Malawi, Tanzania zilibidi kushirikiana na Rwanda ili kuwezesha zoezi hili kwa kuzigatia sheria za kimataifa, protokali na kanuni za Geneva
Hili si swala la siku mbili tu au tatu?
 
Tunawapa pongezi serikali ya Rwanda kuwaruhusu marehemu kupitia Rwanda bila tozo ya aina yoyote..nchi nyingine za kiafrika ziige kutoka Rwanda ili hata sisi tukifa tupitishwe Nigeria ,Burkna Faso,Rwanda na nchi zote za maziwa makuu.
 
Kuna askari watoro wa jeshi la Burundi wanakimbia kutoka Bukavu Kongo na silaha zao, wanaweza kuingia na silaha hivyo ni kufanya ugumu watoro hao wasio na nidhamu za kijeshi kuingia Tanzania na kufanya tatizo la kiusalama au kutumia ardhi ya Tanzania kuishambulia Rwanda na kuleta tatizo la kidiplomasia n.k
Nope,sababu hafifu,tuna kambi ya jeshi kigoma
 
Back
Top Bottom