Majadiliano ya Corona sio siasa ni mtihani mgumu sana tusitukanane

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Sisi wote ni Watanzania na tuna wapedwa na sisi wenyewe ambao tunaogopa huu ugojwa ambao umeingia. Nasikitika sana tofauti zetu kugeuzwa kisiasa. Kwenye hili hakuna jibu zuri na kufurahisha kila mtu ni maamuzi tu ndiyo yanapishana

1. Je tufunge sehemu kwa muda kuzuia mpasuko wa huu ugojwa ambao hauna dawa mpaka sasa? Lakini tukifunga kwa mwezi kuha mtihani mkubwa wa uzalishaji wa uchumi na uchumi binafsi wa watu

2. Je tuache tu tusifunge sehemu yeyote na tuwe makini bila kujali ongezeko la ugojwa huu?

Kuchangua upande mmoja wa hoja haina maana yeyote za kisiasa. Wengine washapoteza watu wa karibu mfano mimi binafsi nitakuwa mwoga zaidi baada ya best friend wangu kufariki wiki mbili zilizopita. Na mpaka sasa nimeshatafuta sehemu ya kupata Oxygen kama nitahitaji maana hiki ndicho kilimwondoa rafiki yangu mwishoni. Binadamu huwezi kusema matokeo hayaingii kwako. Hata huyu Mbowe mtoto wake ana Corana na yeye kakoswa koswa atakuwa na maono tofauti na yule ambaye anaona hili jambo liko mbali naye.

Lakini hatuwezi kuacha kufikiri wakati huohuo je uchumi wetu tukifunga hata mwezi mmoja shughuli za makusanyiko tutakuwa wapi Je tutaweza kulipa kodi, polisi wanaweza kuendelea kupewa mishahara, maji yataendelea kuwa safi, umeme utaendelea kuwaka. Hivyo wengi wa Watanzania hatujui kwa undani sana serikali inaendeshwa vipi na mapato yanatoka wapi.

Tatizo ni kwamba kuna wanaofikiri upande mmoja tu ndiyo uko sawa hata Magufuli amekosea kuingiza siasa kwenye hili Mbowe ambaye mtoto wake anaumwa hawazi kufikiri sawa na Magufuli ambaye yupo kijijini kwake na hakutani na watu ovyo hata kama mliona wakati Mwigulu akiapishwa alikaa mbali na Camera ilikuwa moja tu pale. Amefanya vizuri kujilinda lakini ni lazima naye ajiweke kwenye viti vya watu wengine. Mtu akifiwa na mume, kaka kwa ugojwa ambao haujulikani vizuri usimseme akiwa mwoga ni ubinadamu tu na wala hakuna sababu ya kupigana madongo wala kulaumu maana uhai ni muhimu kuliko pesa kama ukosaji wa pesa ni kwa muda. Hivyo tuweke utamadumi wa kupishana kimawazo bila kuonana kama vile wengine ni wasaliti.

Papa mkuu wa kanisa la katoliki kafunga Je wanaosema wanaofunga makanisa na Papa naye ni msaliti, Je yeye aliyetoa amri ya kufunga kajenga yeye Roma?

Saudi wamefunga sehemu zote za waislamu kwenda kusali na Iran nao wamefunga je wenyewe si wadini au hawamjui Mungu?

Kuna wanaosema Mungu hapimwi anakupa njia za kugundua mabaya mfano ukiruka kwenye gorofa bila sababu huwezi kusema unaomba Mungu azuie usianguke.

Vile vile tuwe wa wazi kama kifaa mfano kinatoa positive test ya uongo basi hicho kifaa vilevile kitakuwa kinatoa negative za uongo lakini tunaongelea upande mmoja bila kujua hata chombo chenyewe.

Kwenye swala la Corona hakuna jibu zuri. Tunachagua kati ya majibu mabaya. Je ni jibu gani ambalo sio baya kama lingine.

Narudia jichunge wewe na familia yako na usisubiri serikali kwenye kila kitu. Mawazo ya Magufuli ni ya kibinadamu na inawezekana hata nyumbani kwake kuna wenye mawazo tofauti ni maswala magumu na sio siasa
 
Kiongozi sio mwelewa anatupeleka pabaya sana.
 
Kwa sasa corona Tanzania Ni ccm Na upinzani.Umoja Wa taifa letu unaparaganyika.
 
Back
Top Bottom