Majaji hawa 7 ndiyo adui wa demokrasia TZ

Majaji hawa 7 ndiyo adui wa demokrasia TZ

Majaji hawakusema ugombea binafsi haufai, tena waliutetea, ila walisema wao hawaandiki Katiba. Ambao ulikuwa uamuzi sahihi.
 
Ki ukweli majaji hao wametuaibisha sana sisi wanasheria, na hii imedhihirisha wazi kuwa lazima tuwe na mahakama maalum ya katiba itakayoshughulikia issue zote zinazotokana na vifungu vya katiba. Cha kushanga, kifungu cha 125 cha katiba kinaweka mahakama maalum ya katiba lakin kifungu cha 126 kinsema kazi pekee ya mahakama maalum ya katiba ni kushughulikia suala lolote linalohususika na tafsiri ya katiba ikiwa tafsiri hiyo inabishaniwa kati ya serikali ya muungano na serikali ya zanzibar! Je hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya mahakama ya katiba? Mimi nafikiri mahakama ya katiba ihusike moja kwa moja na shauri lolote linalohusu kifungu chochote cha katiba na sio kama inavyotafsiriwa kwenye vifungu hivyo!
 
Nchi hii imewahi kuwa na Jaji Mmoja tu nakumbuka alikuwa akiitwa Rugakingira!

umenikumbusha mbali, huyu jaji anaheshimika sana ktk tasnia ya sheria km uwanja wa haki! Ukifika pale Mwananyamala kuna jengo la kumbukumbu yake.
 
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?

Hawa majaji ni weledi sana. Ukitaka kudhihirisha hilo, soma hukumu zao. nadhani walikuwa na shinikizo kutoka serikalini. Lakini ni majaji makini sana ukiacha marehemu Lugakingira, Mroso, Katiti na wengineo.
Sasa wakati umefika kuweka mgombea binafsi kwenye Katiba. Tukishindwa hapa basi tumekwisha
 
umenikumbusha mbali, huyu jaji anaheshimika sana ktk tasnia ya sheria km uwanja wa haki! Ukifika pale Mwananyamala kuna jengo la kumbukumbu yake.

Huyu alitukuka. Hukumu zake nyingi ziko kwenye TLR. We are yet to get another judge of that intellect!!!!
 
this happens only in Tz, you are not a graduate kisha unachaguliwa kuwz jaji.ccm oyeee
 
As long majaji wanakuwa appoited,ufanisi wao lazima uwe wenye utata
hata utaratibu wa kumpata waziri mkuu ulitakiwa ubadilishwe ili angalau aweze kukohoa mbele ya rais.

Sasa hivi waziri mkuu yupoyupo tu kama TV ambayo remote kaishika rais.
 
Back
Top Bottom