Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi hii imewahi kuwa na Jaji Mmoja tu nakumbuka alikuwa akiitwa Rugakingira!
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?
Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!
Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?
umenikumbusha mbali, huyu jaji anaheshimika sana ktk tasnia ya sheria km uwanja wa haki! Ukifika pale Mwananyamala kuna jengo la kumbukumbu yake.
hata utaratibu wa kumpata waziri mkuu ulitakiwa ubadilishwe ili angalau aweze kukohoa mbele ya rais.As long majaji wanakuwa appoited,ufanisi wao lazima uwe wenye utata