Uchaguzi 2020 Majaliwa anafanya Kampeni kwa kutumia ratiba ya nani? Kwa nafasi gani ya Kitaifa?

Uchaguzi 2020 Majaliwa anafanya Kampeni kwa kutumia ratiba ya nani? Kwa nafasi gani ya Kitaifa?

Msafara wa Majaliwa unatumia Mafuta na Rasilimali za Serikali kwa ajili ya shughuli za kichama. Haya ni matumizi mabaya ya Kodi zetu tunazolipa kwa tabu nyingi. Niseme tu CCM pamoja na Majaliwa acheni kabisa kutumia vibaya kodi zetu na nafasi zenu kuhujumu uchumi wa taifa.
Umeandika punch zinazo-make sense aisee. Hili swali inabidi tuulizane. Anatumia zile rasilimali kama waziri mkuu au kama nani ? Ni za chama au serikali ? Hapa kuna haja ya kupata majibu kwa minajili ya kuifikia Tanzania tunayoitaka
 
Pamoja na Cheo chake cha Uwaziri Mkuu, Tabia na kitendo cha Majaliwa kuzunguka Peke yake na kufanya Mikutano ya hadhara ya kuomba KURA ni ukiukwaji wa Taratibu. Anapswa kurudishwa Ruangwa akamtafutie Magufuli Kura kweli.

Msafara wa Majaliwa unatumia Mafuta na Rasilimali za Serikali kwa ajili ya shughuli za kichama. Haya ni matumizi mabaya ya Kodi zetu tunazolipa kwa tabu nyingi. Niseme tu CCM pamoja na Majaliwa acheni kabisa kutumia vibaya kodi zetu na nafasi zenu kuhujumu uchumi wa taifa.

Kama sasa hivi wakaibuka watu wakaanza kumfanyia Rungwe Kampeni kwenye Mikoa AMBAYO hajafika je Tume ya Uchaguzi itawazuia?Kama jibu ni ndio basi nafikir Pia ni Vyema Majaliwa kazuiwa.

Nawasilisha
Hili suala la Ndugu Majaliwa Kassim Majaliwa kufanya kampeni na kumuombea kura Rais Magufuli wa CCM ni hivi: NEC kwa kutumia Sheria ya Uchaguzi ikiwa inasomwa na Sheria nyingine za nchi, pamoja na KATIBA, huwa inakaribisha kila mgombea Urais kuteua idadi Fulani ya "wapambe wake" kumsaidia kwenye kampeni. Komredi Magufuli na CCM, wameteua timu hiyo ikiwa ni pamoja na Komredi Majaliwa. Hii ni sahihi kwa mujibu wa sheria zetu, kama nyie hamna hizo timu au mna mtafaruku wa kipesa na Umoja ndani ya CDM, poleni sana.
Kuna Ratiba za kampeni kwa nchi nzima sasa anapokua mahali anakua kwa ratiba ya nani
Anakuwa kwa ratiba ya NEC ndiyo maana hujaona wala kusikia muingiliano au mgongano wa ratiba za kampenini kule anakopita Komredi Majaliwa na wagombea wengine au na Lissu. Kama huelewi vile, basi lichukulie hili na ulilinganishe na mikutano ya kampeini ya Komredi Mama Samia Suluhu Hassan, hii nayo haijagongana na ratiba nyingine zozote. Nisemalo ni kuwa hizi ratiba zote zinaratibiwa na NEC. Hivyo NI HALALI. Hapa mchawi NI PESA YAO.
 
Anafanya kampeni kwa kutumia RATIBA za wagombea Ubunge na Udiwani wa maeneo au Majimbo na Kata husika.
 
Back
Top Bottom