Unaweza ukamuona PM Majaliwa kama mtu ambaye hana muelekeo kisiasa, au hana nguvu sana kama zinavyohitajika ktk nchi hii, lakini kwa mtazamo wangu ktk nafasi yake ya PM, ameweza kuwa mtu ambaye anakwepa blunders (makosa ya kijinga). Majaliwa ni mtu makini asiyetamka bila kuhusisha ubongo wake. Tuachane na matizo yake ya sulfur ya korosho na kuwasuka-suka TPRI ili tu sulfur ipitishwe (ufisadi).
Akiwa na Magufuli alikwepa makosa ya lugha mbaya zisizojali utu na kadamnasi ya kitanzania, wakati Magufuli alijawa na lugha ya aina hiyo. Amekuwa na Samia, pia sijasikia akiropoka kama Samia mwenyewe alivyofanya hadi kufikia kudhalilisha wanamichezo wa kike. Majaliwa ana umakini wa aina fulani. Lakini maagizo yake mengi hayatoi matokeo. Tangu lile la BoT, watumishi wa hazina na mengine yanayofuata. Au wanampoza?