Majaliwa chini ya Magufuli v/s Majaliwa chini ya Samia

Majaliwa chini ya Magufuli v/s Majaliwa chini ya Samia

Wa-TZ wana mengi ya kusema. HAKIKA!
 
Unaweza ukamuona PM Majaliwa kama mtu ambaye hana muelekeo kisiasa, au hana nguvu sana kama zinavyohitajika ktk nchi hii, lakini kwa mtazamo wangu ktk nafasi yake ya PM, ameweza kuwa mtu ambaye anakwepa blunders (makosa ya kijinga). Majaliwa ni mtu makini asiyetamka bila kuhusisha ubongo wake. Tuachane na matizo yake ya sulfur ya korosho na kuwasuka-suka TPRI ili tu sulfur ipitishwe (ufisadi).

Akiwa na Magufuli alikwepa makosa ya lugha mbaya zisizojali utu na kadamnasi ya kitanzania, wakati Magufuli alijawa na lugha ya aina hiyo. Amekuwa na Samia, pia sijasikia akiropoka kama Samia mwenyewe alivyofanya hadi kufikia kudhalilisha wanamichezo wa kike. Majaliwa ana umakini wa aina fulani. Lakini maagizo yake mengi hayatoi matokeo. Tangu lile la BoT, watumishi wa hazina na mengine yanayofuata. Au wanampoza?wat

duh....watanzania wasahulifu sana..huu sijui ni usahaulifu wa kujitakia ama ni ujinga....yani umeshasahau ni majaliwa huyu huyu alinganya umma akiwa msikitini kwamba jpm yuko hai na fit...wakati wote twajua baadae kuwa haikuwa kweli....hapa umerefusha tu maneno...ungesema tu kuwa huyu jamaa ni binge la mnafiki....yaani mtu mwenye ndimi mbili...
 
Mzee wa matamko lkn hakuna anaehangaika nayo.
Mnakumbuka alivyomfukuza kazi injinia lkn MFUGALE akamuwekea ngumu. Just imagine MFUGALE sio waziri Wala katibu mkuu.
 
Mbona mnataka abebe mzigo usio wake, majaliwa hana ubavu wa kuagiza jambo likawa endapo bosi wake haoni mantiki. Vipi akiagiza na boss akasinichi utamlaumu vipi majaliwa? Na wengine wanasema kabisa wao wanamdharau mwenye mbwa mwenyewe ije kuwa mbwa, kwahyo eleweni hii game ikoje. Mkitaka majaliwa aagize mpeni nchi ndo mtajua nani ni nani
 
Back
Top Bottom