Majaliwa: Kiti cha Urais sio mchezo, kinahitaji mtu makini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa amesema kiti cha urais siyo cha mchezo, kinahitaji mtu makini.

“Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, linataka kiongozi makini, kiongozi anayetetea rasilmali na anayetetea wanyonge dhidi ya rushwa na ufisadi,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Septemba 24, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Hungumalwa na Ngudu wilayani Kwimba, mkoani Mwanza kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya sokoni.

“Wengine watakuja kuomba kura lakini kazi yao kubwa ni kukashifu kila jambo linalofanywa na Serikali. Naomba kura za wananchi wote, wana CUF, CHADEMA, ACT mkipigie kura Chama cha Mapinduzi sababu maendeleo hayana chama.”

“Wakija hapa muwasikilize; mkiwauliza Ilani yao watakwambia wanayo ila iko kwenye website. Sisi ya kwetu tunayo hii hapa,” alisema huku akionesha Ilani ya CCM ya 2020 – 2025.”

Amewataka wakazi hao wafanye maamuzi thabiti ya kutafuta viongozi tena wanaozungumza lugha moja. “Viongozi hao ninawaombea kura ni Rais, Mbunge na Diwani. Msichague viongozi ambao kazi yao ni kusema hapana kwenye mambo ya maendeleo au kwenye bajeti ya Taifa. Naomba kura kwa viongozi hao watatu,” amesema.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Kwimba, Bw. Shanif Mansoor, mgombea udiwani wa Hungumalwa, Bw. Bukaba Majoge na madiwani wa kata zote za wilaya ya Kwimba.

Wakati huohuo, mgombea ubunge wa jimbo la Geita Vijijini, Bw. Joseph Kasheku Msukuma ambaye aliwepo kwenye mikutano huo, alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali iwajengee soko la kisasa wakazi wa Hungumalwa kwa sababu eneo hilo pana biashara kuwa ya dengu, choroko na kunde.
 
Naomba kura za wananchi wote, wana CUF, CHADEMA, ACT mkipigie kura Chama cha Mapinduzi sababu maendeleo hayana chama.”
Huyu anapishana kauli na bosi wake. Bosi wake (Magufuli) Mara zote amekuwa akisisitiza "hawezi kupeleka maendeleo ktk majimbo yaliyoshikiliwa na upinzani", na kutolea mfano wa tochi kwamba "haiwezi waka kama betri zimechanganywa na mabunzi" (Alipokuwa Bunda mjini, na Jimbo la Bwege-Lindi)

Amewataka wakazi hao wafanye maamuzi thabiti ya kutafuta viongozi tena wanaozungumza lugha moja.
Kama Majaliwa na Magufuli hawazungumzi lugha moja, ni halali wanainchi kwa sasa kugeuza upepo wa kisiasa kwa kuamua kufanya mageuzi makubwa ya kuangalia upande mwingine wa shillingi (Vyama vya upinzani) ili kuwapata viongozi wenye kuzungumza lugha moja na waliothabiti wakiongozwa na TUNDU LISSU "The hero man".
 
Magufuli raisi wangu umeua chama ukishachukuwa awamu ingine badilika baba
 
Tulikosea kumchagua Magufuli 2015!Haturudii makosa hayo mwaka huu!
 
MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa amesema kiti cha urais siyo cha mchezo, kinahitaji mtu makini.

“Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, linataka kiongozi makini, kiongozi anayetetea rasilmali na anayetetea wanyonge dhidi ya rushwa na ufisadi,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Septemba 24, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Hungumalwa na Ngudu wilayani Kwimba, mkoani Mwanza kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya sokoni.

“Wengine watakuja kuomba kura lakini kazi yao kubwa ni kukashifu kila jambo linalofanywa na Serikali. Naomba kura za wananchi wote, wana CUF, CHADEMA, ACT mkipigie kura Chama cha Mapinduzi sababu maendeleo hayana chama.”

“Wakija hapa muwasikilize; mkiwauliza Ilani yao watakwambia wanayo ila iko kwenye website. Sisi ya kwetu tunayo hii hapa,” alisema huku akionesha Ilani ya CCM ya 2020 – 2025.”

Amewataka wakazi hao wafanye maamuzi thabiti ya kutafuta viongozi tena wanaozungumza lugha moja. “Viongozi hao ninawaombea kura ni Rais, Mbunge na Diwani. Msichague viongozi ambao kazi yao ni kusema hapana kwenye mambo ya maendeleo au kwenye bajeti ya Taifa. Naomba kura kwa viongozi hao watatu,” amesema.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Kwimba, Bw. Shanif Mansoor, mgombea udiwani wa Hungumalwa, Bw. Bukaba Majoge na madiwani wa kata zote za wilaya ya Kwimba.

Wakati huohuo, mgombea ubunge wa jimbo la Geita Vijijini, Bw. Joseph Kasheku Msukuma ambaye aliwepo kwenye mikutano huo, alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali iwajengee soko la kisasa wakazi wa Hungumalwa kwa sababu eneo hilo pana biashara kuwa ya dengu, choroko na kunde.
Kweli tunahitaji rais makini lakini sio huyu wa sasa, hafai kabisa.
 
Back
Top Bottom