Majaliwa na maana ya uokoaji, Precision Air na deni kwa kijana huyu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Yanasemwa mengi juu ya ajali mbaya ya ndege ya Precision Air kule Bukoba ikiwa imebakiza mita 150 kabla haijatua. Kila mwenye ujuzi wa kuandika anaandika kila mwenye maarifa ya ukosoaji anafanya hivyo kwa nguvu kubwa.

Kijana Majaliwa mwenye kujishughulisha na biashara ya dagaa ndiye aliyeibuka shujaa kwa kuweza yeye peke yake kuokoa abiria 23 kati ya 42, zaidi ya nusu ya wote. Baada ya kuvunja mlango na wakaweza kutoka nje vinginevyo muda huu tungekuwa tunaongea mengine mabaya zaidi.

Naona kila taasisi inayoguswa ina mchangia chochote kijana huyu jasiri wa huko Bukoba, GSM wametoa milioni tano na bado zile pesa zinazotoka kwa mtu mmoja mmoja.

Najua kuwa kampuni ya Precision Air inao msiba mzito wa kupoteza hao abiria 19. Lakini sioni kama ni dhambi yoyote ile wao kama kampuni kumpatia chochote kijana huyu. Amesaidia japo katika hali ya taabu kutunza jina la kampuni hiyo, wangeweza kupoteza abiria wote 42.

Huu uwe ni muda wa menejimenti kufanya tafakari ya kina kuangalia namna wanavyoweza kumpa mkono wa asante kijana huyu.

Pia nahisi kama maamuzi ya Mheshimiwa Rais ya kumpeleka kijana akasomee jeshi la uokoaji kama ni ya kukurupuka. Angeweza kutuma wasaidizi wake wakaongea nae ili kujua wito wake haswa ni upi.

Kumpangia kuwa muokoaji ni kama kumlazimisha, yale yale ya mtoto anajua sana kuimba na kuchora halafu Baba na Mama wanamlazimisha kutwa kucha akasomee udaktari!. Matokeo ya kidato cha sita yakija kijana wao kaondoka na zero.

Pengine wangeangalia uwezekano wa kumnunulia boti ya kisasa ya uvuvi, wangeangalia uwezekano wa kumnunulia nyavu za kisasa za uvuvi, ili abakie mle mle katika kufanya kitu ambacho roho yake ina amani ya kukifanya.
 
Hapo mwisho ndo naona panaweza kutazamwa kama kipaumbele, lakini hapo hapo yaweza kua kijana huyu anafanya kazi ya uvuvi kwa sababu ya kujikomboa ki uchumi, kwani si kila mvuvi anaipenda kazi hiyo ila unakuta anafanya kwa sabu ndiyo njia ya kujipatia kipato ambayo aliona yeye ipo ndani ya uwezo wake kulingana na mazingira yanayo mzunguka....

Hapo wazungumze nae wajue chenye ni ndoto yake alitamani kufanya na ana uzoefu/idea nacho ndiyo wamwezeshe...
 
Yanasemwa mengi juu ya ajali mbaya ya ndege ya Precision Air kule Bukoba ikiwa imebakiza mita 150 kabla haijatua. Kila mwenye ujuzi wa kuandika anaandika kila mwenye maarifa ya ukosoaji anafanya hivyo kwa nguvu kubwa.

Kijana Majaliwa mwenye kujishughulisha na biashara ya dagaa ndiye aliyeibuka shujaa kwa kuweza yeye peke yake kuokoa abiria 23 kati ya 42, zaidi ya nusu ya wote. Baada ya kuvunja mlango na wakaweza kutoka nje vinginevyo muda huu tungekuwa tunaongea mengine mabaya zaidi.

Naona kila taasisi inayoguswa ina mchangia chochote kijana huyu jasiri wa huko Bukoba, GSM wametoa milioni tano na bado zile pesa zinazotoka kwa mtu mmoja mmoja.

Najua kuwa kampuni ya Precision Air inao msiba mzito wa kupoteza hao abiria 19. Lakini sioni kama ni dhambi yoyote ile wao kama kampuni kumpatia chochote kijana huyu. Amesaidia japo katika hali ya taabu kutunza jina la kampuni hiyo, wangeweza kupoteza abiria wote 42.

Huu uwe ni muda wa menejimenti kufanya tafakari ya kina kuangalia namna wanavyoweza kumpa mkono wa asante kijana huyu.

Pia nahisi kama maamuzi ya Mheshimiwa Rais ya kumpeleka kijana akasomee jeshi la uokoaji kama ni ya kukurupuka. Angeweza kutuma wasaidizi wake wakaongea nae ili kujua wito wake haswa ni upi.

Kumpangia kuwa muokoaji ni kama kumlazimisha, yale yale ya mtoto anajua sana kuimba na kuchora halafu Baba na Mama wanamlazimisha kutwa kucha akasomee udaktari!. Matokeo ya kidato cha sita yakija kijana wao kaondoka na zero.

Pengine wangeangalia uwezekano wa kumnunulia boti ya kisasa ya uvuvi, wangeangalia uwezekano wa kumnunulia nyavu za kisasa za uvuvi, ili abakie mle mle katika kufanya kitu ambacho roho yake ina amani ya kukifanya.
Nalipia bango miji yote, hili tangazo liwekwe.
 
Back
Top Bottom