Uchaguzi 2020 Majaliwa: Uongozi wa nchi hauendi kwa upepo na ushabiki

Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania...
Atutoleee ujinga huyo viti maalumu jitu limeshindwa kumshawishi mwanamke kubadili dini litawezaje kuwashawishi watu wachague kijani?
 
uongozi haujaribiwi kwani majaliwa wapi kuna chuo cha uraisi kura ndo zinaweka watu madarakani
 
Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania...
Hana hoja za maana apishe demokrasia tena anapaswa kurudi jimboni kwake akafanye kampeni kama alivyoagizwa na bashiru.
 
Tulishawajaribu wao sasa watuachie tumjaribu Mwingine. Na kama walitaka wawe peke yao wasingekubali uchaguzi huu uwe chini ya vyama vingi.

Nilikuwa namheshimu sana Majaliwa lkn kuanzia leo nae namchukulia....kama yule mama wa risasi tatu tu chali.
 
Majaribio ni sehemu ya demokrasia pia,ndio maana ya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.
 
Huyu mpaka piko kichwani asionekane mzee ..nimemdharau unaanzaje kuwateka wapinzani wako kisiasa..ndio maana Magu analifanya atakavyo
 
Mtanzania yoyote mwenye akili timamu anaweza kuwa rais wa nchi hii. Kama JK na Magufuli wameweza kuwa marais, nani atashindwa kazi hiyo?
Ndiomaana nasema yeyote yule aliyepitishwa na tume anafaa kuwa rais wa nchi hii kama hafai basi na tume haifai na aliyeiteua tume naye hafai.
 
Wananchi walishatafakari siku nyingi! Yeye anaona ni sawa kwake kupita bila kupingwa? Watu wa namna hii sijui hata mnawezaje kuwasikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…