Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Kapicha basi japo ka Jambazi kamoja tu? hivi Kibiti ni Majambazi au Magaidi? maana Sijasikia wakiiba hao wauaji wa Kibiti!
 
Majibizano hayo hakuna Polisi aliyejeruhiwa duh! pengine hao Jamaa walijificha na Njaa ikawaumbua wakajitokeza kizembe na kichovu
 
Kwahyo bado ngap ili polisi wasawazishe iwe droo...maana kuna msemaji wa polisi mmoja alikuwa analeta utani...btw gud move
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Kama Majambazi Watupa Risasi Polisi Watawakamataje?
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
sijui kilichotokea, ila kama wewe ni raia mwema kwanini urushiane risasi na polisi?

mwananchi SMG unamiliki ya nini?
 
Jamani mi mwenzenu saivi bila kithibiti chochote siamini maneno ya Siro maana na yeye Ni mwasaniasa kama CCM wengine tu. Naomba niondoleeni huu mkanganyiko wa mawazo!!!!!!Naombeni picha zao maana ndo utamaduni wenu.
 
Watu 13 wanaodaiwa kuwa ahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
Safi sana IGP Siro, hayo majitu yamesha kengeuka sio binadamu wa kawaida na hawatakiwi kuishi kwenye jamii.

Mwendo huohuo, yakikutwa hakuna kupoteza muda ni kuyanyanga'nya silaha haraka haraka kabla hayajasababisha madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kila siku wanauwawa tu,maiti ziko wapi basi hata majina yao.Kwanini hawakuachwa basi ili wafikishwe mahakamani.Kila wakati wote wameuwawa.Siro napata mashaka na taarifa hizi.
 
Back
Top Bottom