Majanga kama hili la Moto Kariakoo yanazidi kutukumbusha umuhimu wa Sekta Binafsi kwenye Uchumi

Mkuu umemaliza kila kitu.. umeeleza vema kabisa.. efficiency ya private sekta ipo mbali sana.

Watu wanazungumzia mambo ya fire hydrants kutokuwepo kariakoo, hivo vyote kama sekta binafsi wangekuwa na tenda, lazima wangeshaona hiyo risk.. miaka 60 tuna uhuru bado hatuwezi kuzima moto, si bora tungekuwa tunatawaliwa tu
 
Mkuu kukiwa na dhamira itawezekana. Ni uzembe wa viongozi tu ndiyo unafanya lisiwezekena. Nchi karibu zote nizotembea nimekuta zimamoto zipo chini ya halmashauri za majiji au miji. Na zina function vizuri tu. Hapa kwetu ni uzembe tu kama zilivyo idara zote. Hili unalo-suggest litafanya walalahoi wakamuliwe tena. Kila mwezi wataanza kukusanya fedha za ''fire'' kutoka kila kaya na maduka kama wanavyokusanya za kuzoa taka. Kinachotakiwa ni kusuka upya muundo wa zimamoto.
 
NB: Mbona kikosi cha kutuliza ghasia kina vifaa vya kisasa na kipo tayari muda wote? 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Tena yanaweza kutokea matukio mengi kwa wakati mmoja na kote wanakuwepo. Moto ni matukio ya mara moja moja tu.
 
litaongeza gharama kwa wananchi
Hii ni fursa ya kuweka bima za majengo dhidi ya moto..... So watu wakiingizwa kwenye scheme then moto ukitokea kuna mfuko wa kufidia gharama ikiwezekana iwe hta ya kaya hta 5 zinachanga micro-insurance inayopelea serikali itoe ruzuku au hta kurelax vikodi/tozo fulani kwa hizi kampuni ziwe cheap.

Uwajibikaji private sector ni mkubwa sana na wapo kibiashara hta customer care ipo juu ndani ya dakika wanafika..... Thou utaona gharama ila ni cost-effective kuliko vya bure ila mtaji wote unateketea.
 
Kikosi cha zima moto ni kama kime sahulika

Ova
Umewahi kusikia hata siku moja fujo zikitokea mahali kikosi cha kutuliza ghasia kimechelewa kufika au kikafika halafu wakawa hawana mabomu na risasi? Au magari yao yakiwa machakavu? Kitu kingine ni kwamba kazi ya kuzima moto inaendana na mipango miji. Nyumba zinapojengwa suala la namna ya kukabiliana na ajali ya moto ni lazima lipewe kupaumbele. Halafu mitaani ni lazima kuwe sehemu za watu wa zimamoto kujaza maji kwa haraka. Kwa mfano soko kama hilo la Kariakoo lilipaswa kuwa na sehemu ya fire kujaza maji kwa karibu.
 
Kwa nchi zetu watu hawatakuwa na uwezo. Nauliza tena: mbona kikosi cha kutuliza ghasia kiko vizuri? Hapa inaonyesha kuwa kukiwa na dhamira kila kitu kinawezekana.
 
Kuna hoja ya mdau hapo juu ameongelea kuhusu KPI kwenye sekta binafsi vs serikalini kwa Tanzania.

Hizo nchi nyingine sekta ya serikali inaweza kuwa efficient sana kulingana na namna wanavifanya kazi.

Ila kwa Tanzania, ni kama mfumo mzima wa huduma zinazotolewa na serikali umepoteza ufanisi, ndo mana nafikiria sekta binafsi inahitajika sana Tanzania kwa sasa
 
Umeeleza vyema kwani najiuliza kuhusu hili.
Kwanini knight support ilhali tuna kituo pale fire, pua na mdomo na soko? Majiji na halmashauri kule kunakopotea mabilioni na hakuna wa kuhoji, ilipaswa hii huduma iwe moja ya majukumu yao
 
Hakueleweka
Alieleweka kwenye kitabu cha kurasa 340 cha mahitaji ya wananchi
sijakiona hicho kitabu, kimsingi kuna watu wamejitolea kulipatia muelekeo wenye matumaini Taifa letu lakini wanaishia kutishiwa uhai,kudhalilishwa na kunyanyaswa na watawala.

sielewi watawala wanapata raha gani wanapozungukwa na wananchi masikini, wasio na muelekeo wala tumaini lolote la kuboresha maisha yao.

maisha yangu yote nimekuwa nikiamini msingi wa maisha yangu ya furaha na mafanikio ni kuishi katika jamii yenye matumaini.
 
Hawa ndiyi fire
Wanawahi moto

Ova
 

Attachments

  • VID-20210711-WA0021.mp4
    3.2 MB
Naee pia jiulize: Unapolipia gari yako bima kila mwaka, (au bima nyingine youote) je hiyo gari inapata ajali kila mwaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…