Majanga makubwa yakitokea nchi zenye vyombo vya habari makini kipaumbele huwa ni Tukio, ila kwetu kipaumbele ni Kuipamba Mamlaka!

Majanga makubwa yakitokea nchi zenye vyombo vya habari makini kipaumbele huwa ni Tukio, ila kwetu kipaumbele ni Kuipamba Mamlaka!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Binafsi nilitegemea baada ya Tukio la Hanang Mkoani Manyara Media ya Tanzania ingekuwa inatupa Elimu zaidi ya nini kimesababisha na hata kutoa tahadhari zaidi kwa eneo husika au maeneo mengine yenye Jiografia kama ya Hanang ili kujiepusha na Majanga makubwa mengine.

Ila cha kushangaza na kunisikitisha wao (Media ya Tanzania) wanachokifanya hasa ni kututangazia idadi ya Vifo, Zawadi zinazotolewa na Kuisifu Mamlaka na Kujipendekeza kwa mwenye Mamlaka Mkuu.

Halafu nikiwadharau na kusema kuwa Tanzania hakuna Media bali kuna Makorokocho Media tupu hamtaki Kuamini na Kuniamini.

Media ambazo kamwe hutokuta Upuuzi huu wa Media ya Tanzania ni Media za Kenya, Uganda Rwanda, South Africa, Ghana, Algeria na Egypt.
 
Kiufupi taaluma ya habari bado sana tuna wana habari wasio jielewa wenye kuendekeza hisia zaidi ya uhalisia..... Yaani media zinaacha taarifa za muhimu zinakwenda kutoa taarifa za kipumbavu tu na kuhamasisha kubeti waandishi wa bongo nibmanyoko tu kama ndugu yao aliepo humu hana jipya uchawa usio eleweka ndio anaweza
 
Kuna mtaalam mmoja alielezea clouds fm kitaalam kilichotokea ila video yake wakaifuta baada ya mda siasa inatuharibia sana nchi hela za kununua goli moja million kumi taifa unazo ila za maafa mpaka msaada taifa stars walipewa million 500 ila wakazi wa hanang wameambiwa wasubirie msaada kutoka nje.
 
Na ukijifanya kuwa mkweli na kui eleza ukwel wenye mamlaka wanakuzima kama anology kwenda digitally........

Na kuwapambania watanzania ni kupoteza muda na nguvu

Li gentamicin sulfate injection huwaga linasemaga ukwel na sio li nafiki viva kwake 😊

✌️✌️✌️✌️
 
Kuna wataalam kibao wa miamba,udongo nk wapo mlimani pale wachukuliwe wapelekwe wakafanye analysis kisha watoe mapendekezo yao nini kifanyike. Ili kuepusha madhara mengine ya wakati ujao.
 
Taaluma ya habari imevamiwa
Hivi karibuni ,wana habari nguli
Wakina Pascal Mayalla wenyewe
Wamefichwa

Ova
Binafsi nilitegemea baada ya Tukio la Hanang Mkoani Manyara Media ya Tanzania ingekuwa inatupa Elimu zaidi ya nini kimesababisha na hata kutoa tahadhari zaidi kwa eneo husika au maeneo mengine yenye Jiografia kama ya Hanang ili kujiepusha na Majanga makubwa mengine.

Ila cha kushangaza na kunisikitisha wao (Media ya Tanzania) wanachokifanya hasa ni kututangazia idadi ya Vifo, Zawadi zinazotolewa na Kuisifu Mamlaka na Kujipendekeza kwa mwenye Mamlaka Mkuu.

Halafu nikiwadharau na kusema kuwa Tanzania hakuna Media bali kuna Makorokocho Media tupu hamtaki Kuamini na Kuniamini.

Media ambazo kamwe hutokuta Upuuzi huu wa Media ya Tanzania ni Media za Kenya, Uganda Rwanda, South Africa, Ghana, Algeria na Egypt.
Kwa niaba ya media fraternity, nimeipokea hii changamoto!.
P
 
Back
Top Bottom