Majangaa kundi la nyuki wavamia nyumba ya mpwa wangu iliyopo mjini Dar mtaa wa Idrissa

Uzuri wa nyuki kama hujawachokoza wala hawawezi kushughulika na wewe.
Kimbembe wajaribu kuuwa nyuki mmoja tu hapo, mtaa mzima watakimbia nyumba zao, na hakuna atakaekuwa na uwezo wa kushika simu kuwa record kama hivi. Nyuki ni jeshi linaloshambulia kwa pamoja, na huwa hawakati tamaa wala kukubali kushindwa.

Nashauri mtafute wataalam wa maliasili wanaohusika na uvunaji wa asali waje wafanye mpango wa kuwachota kupitia vyombo vyao maalumu.
MMiaka hiyo katika kusaka mkate..nyuki walivamia pahala..katika jitihada za kuoka mtu..aise nyuki wanaumaa1😀😀😀
 
Ingekua kwetu tungesema hiyo ni ndagu mali imeingia ndani. Tumia rungu wataondoka
 
Mkuu umesoma nilichoandika kweli.

Mbona nimeweka wazi kuwa wakichokozwa wanaweza kushambulia mtaa mzima haijalishi ni nani aliewachokoza.

Lakini narudia tena kuwa nyuki kama haukuwachokoza, wala hawawezi kushughulika na wewe, ndomaana unaona mtimkavu amepata ujasiri wa kusimama pembeni kuchukua video. Kama wangekuwa wanashambulia tu hovyo bila kuchokozwa basi hao waliochukua video wasingepata ujasiri au uwezo huo wa kuchukua video huku wanaongea.
Usilete mazoea kwa nyuki wewe eti useme usipowachokoza! Nyuki hata ukimpunga tu kama unafukuza nzi wanakushambulia wote, sasa jiulize ni wangapi hapo watakuwa wavumilivu wakizungukwa na nyuki wasiwapunge kwa mkono?
 
Mkuu ulichoongea ni sahihi nakumbuka nipo second semester ya pili naenda kwenye paper nikaona kama nzi ananizonga ile kumpiunga si akafa...
Cha moto nilikipata walinishambulia alieniokoa ni dereva boda alikuwa anapita akaniambia dandia fasta alikimbiza chombo hatari ndio pona yangu.

Na mtihani nilishindwa fanya nikaomba special exam
 
Jamaa anaeta masihara na nyuki huyu!
 
Waone maliasili waliopo karibu yako wao watawatoa safely. Nyuki ni mali watu wanawasaka sana huko porini, kuna mizinga ya nyuki imetegwa muda mrefu bila mafanikio. Sijapenda mlivyowaua
 
Uzuri wa nyuki kama hujawachokoza wala hawawezi kushughulika na wewe.
Kimbembe wajaribu kuuwa nyuki mmoja tu hapo, mtaa mzima watakimbia nyumba zao, na hakuna atakaekuwa na uwezo wa kushika simu kuwa record kama hivi. Nyuki ni jeshi linaloshambulia kwa pamoja, na huwa hawakati tamaa wala kukubali kushindwa.

Nashauri mtafute wataalam wa maliasili wanaohusika na uvunaji wa asali waje wafanye mpango wa kuwachota kupitia vyombo vyao maalumu.

Hakuna haja ya mtaalamu.

Wasubiri giza liingie, wanunue dawa ya kuulia wadudu awapulizie watakufa wote na kudondoka chini kama maua.
 
Nadhani hao walimuua nyuki moja, akaachia ‘feromones’ zake na kuita wenzake, hii ni ‘defensive’ strategy yao..
 
Magomeni iko mjini kabisa lakini bado hii sehemu imetawaliwa Sana na uchawi, ulozi na ushirikina. Mara Mia nikae Sinza kuliko Magomeni.
Ndiyo haohao wenye asili ya hiyo Sinza mambo yao yako jiji zima
 
Usilete mazoea kwa nyuki wewe eti useme usipowachokoza! Nyuki hata ukimpunga tu kama unafukuza nzi wanakushambulia wote, sasa jiulize ni wangapi hapo watakuwa wavumilivu wakizungukwa na nyuki wasiwapunge kwa mkono?
Mimi nafikiri wewe haujui hata ulichoandika. Mimi nimekwambia wakichokozwa, kumpunga mdudu kama huyo ni sawa na kumchokoza pia.

Hao waliopo hapo hawajawapunga wala kuwachokoza, ndio maana umeona wamepata ujasiri wa kuwarekodi huku wakiongea. Usithubutu kufikiri kuwa hapo ndani kuna mtu atakuwa aliwachokoza au kuwapungia hata mmoja. Laiti angetokea mtu hata mmoja akawachokoza au kumpungia mmoja akaanguka chini basi hakuna ambae angethubutu kushika simu yake kuwa rekodi.

Sasa sijui hoja yako inasimamia wapi na inapinga nini nilichoandika?
 
Back
Top Bottom