MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa Tangazo kwamba, tarehe 27-04-2022 Kuanzia mda wa saa nne Asubuhi litaanza MAJARIBIO ya TRENI ya Umeme nchini Tanzania kwa Kipande Cha Kwanza (Dar-Moro) chenye urefu wa 205km.
Majaribio hayo yataanza kwa kujaribu njia ya Umeme wa 25kV kwenye njia nzima ya Reli hiyo. TRC imewataka wananchi wote wa Dar, Moro, na Pwani kuwa makini wakati wa majaribio hayo kwani lolote lile linaweza kutokea.
Majaribio hayo yatafanyika kwa kutumia kichwa Cha TRENI ya Umeme cha Mkandarasi ambacho kiliwasili nchini Mwezi Machi mwaka huu. Majaribio hayo yatakuwa Mubashara TBC.
Ewe Mtanzania na Mzalendo wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, unakaribishwa katika kushiriki uzinduzi huu wa Aina yake katika Historia ya Afrika Mashariki.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika,Amen.