Majaribio ya Reli ya Kisasa (SGR) Tanzania

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa Tangazo kwamba, tarehe 27-04-2022 Kuanzia mda wa saa nne Asubuhi litaanza MAJARIBIO ya TRENI ya Umeme nchini Tanzania kwa Kipande Cha Kwanza (Dar-Moro) chenye urefu wa 205km.

Majaribio hayo yataanza kwa kujaribu njia ya Umeme wa 25kV kwenye njia nzima ya Reli hiyo. TRC imewataka wananchi wote wa Dar, Moro, na Pwani kuwa makini wakati wa majaribio hayo kwani lolote lile linaweza kutokea.

Majaribio hayo yatafanyika kwa kutumia kichwa Cha TRENI ya Umeme cha Mkandarasi ambacho kiliwasili nchini Mwezi Machi mwaka huu. Majaribio hayo yatakuwa Mubashara TBC.

Ewe Mtanzania na Mzalendo wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, unakaribishwa katika kushiriki uzinduzi huu wa Aina yake katika Historia ya Afrika Mashariki.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika,Amen.
 
Takataka na uchafu kama huu unafanya nini kwenye Kenyan section? Hii ungeipeleka kwenye mapenzi section.
Najua wewe NI Mkenya. Lakini kumbuka TRENI hii ya Umeme Ni Pride ya Afrika Mashariki kwa ujumla(Tz,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,S.Sudan na DR Congo). Kwahiyo bila kujali utaifa Ni wajibu wetu sote wana EAC kushangilia,Bara la Afrika tumebaki nyuma kwa mda Mrefu Sana hasa kwenye Miundombinu ya Reli za Umeme. Tanzania imeonesha Nia na Ni wajibu wa Mataifa mengine ya EAC kufuata mkondo.
 
Duh! Ina maana mpaka leo hamjaanza kutumia hicho kipande cha Dar-Moro, ndio mnaandaa kufanya majaribio? Huo mradi mumeiburuza kwa kweli, anyway hongereni.
 
Mkuu hii hongera mbona inaonekana ni ya wivu na kuna hatari ukaturushia hata jini tuhangaike nalo ili tisifanikiwe
 
TRC imewataka wananchi wote wa Dar, Moro, na Pwani kuwa makini wakati wa majaribio hayo kwani lolote lile linaweza kutokea.

Lolote linaweza kutokea??!!😗

Ewe Mtanzania na Mzalendo wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, unakaribishwa katika kushiriki uzinduzi huu wa Aina yake katika Historia ya Afrika Mashariki.

Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayekuja ukizingatia onyo kwamba; "lolote linaweza kutokea."
 
Mkuu hii hongera mbona inaonekana ni ya wivu na kuna hatari ukaturushia hata jini tuhangaike nalo ili tisifanikiwe

Mchawi wenu ni nyie wenyewe, mradi wenyewe mumeuchelewesha hadi basi, na mpaka sasa hamuonekani kujiamini, halafu hivi hiyo Bongo mumeshakidhi mahitaji yenu ya umeme kabla kuanza kusukuma treni kwa umeme, maana nawafahamu hamjambo kwa mgao wa umeme, kutwa majenereta yanarindima mjini....nahisi kama mlikurupuka kwenye hili, mngeanza kwa kutambaa kabla kujitutumua kukimbia.
 
Hivi Sasa huko kwenu diesel hakuna, Ina maana Hilo train lenu halifanyi kazi?, Kwanini msingesubiri hadi Yale mafuta yenu kule Turkana muanze kuyavuna ndio mjenge hiyo reli yenu ya diesel Engine, nani ni mkurupukaji mkubwa?

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Mchawi wenu ni nyie wenyewe, mradi wenyewe mumeuchelewesha hadi basi, na mpaka sasa hamuonekani kujiamini, halafu hivi hiyo Bongo mumeshakidhi mahitaji yenu ya umeme kabla kuanza kusukuma treni kwa umeme, maana nawafahamu hamjambo kwa mgao wa umeme, kutwa majenereta yanarindima mjini....nahisi kama mlikurupuka kwenye hili, mngeanza kwa kutambaa kabla kujitutumua kukimbia.
Wivu usio na tija utakuua.
 
Wewe hujakuja Tz siku nyingi ama aliyekuhadithia hajafika huku tangu 90s Tanzania we have stable electricity hakuna mgao siku hizi
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa Tangazo kwamba, tarehe 27-04-2022 Kuanzia mda wa saa nne Asubuhi litaanza MAJARIBIO ya TRENI ya Umeme nchini Tanzania kwa Kipande Cha Kwanza (Dar-Moro) chenye urefu wa 205km.

Majaribio hayo yataanza kwa kujaribu njia ya Umeme wa 25kV kwenye njia nzima ya Reli hiyo. TRC imewataka wananchi wote wa Dar, Moro, na Pwani kuwa makini wakati wa majaribio hayo kwani lolote lile linaweza kutokea.

Majaribio hayo yatafanyika kwa kutumia kichwa Cha TRENI ya Umeme cha Mkandarasi ambacho kiliwasili nchini Mwezi Machi mwaka huu. Majaribio hayo yatakuwa Mubashara TBC.

Ewe Mtanzania na Mzalendo wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, unakaribishwa katika kushiriki uzinduzi huu wa Aina yake katika Historia ya Afrika Mashariki.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika,Amen.
Legacy ambayo inaishi..JPM lala salama tutakukumbuka daima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe hujakuja Tz siku nyingi ama aliyekuhadithia hajafika huku tangu 90s Tanzania we have stable electricity hakuna mgao siku hizi
Juzi tu kulikuwa na mgao wa umeme TZ kwa sababu kiwango cha maji kilikuwa kimepungua. Na shirika lenu la umeme Tanesco lilitangaza mgao huo wazi.
 
Wewe hujakuja Tz siku nyingi ama aliyekuhadithia hajafika huku tangu 90s Tanzania we have stable electricity hakuna mgao siku hizi

Hivi unajua unachoandika hapa Watanzania wenzio wanasoma na kukushangaa, eti hamna changamoto za umeme Bongo? Huyo waziri Makamba nusra mumtoe nje kisa hayo matatizo.
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa Tangazo kwamba, tarehe 27-04-2022 Kuanzia mda wa saa nne Asubuhi litaanza MAJARIBIO ya TRENI ya Umeme nchini Tanzania kwa Kipande Cha Kwanza (Dar-Moro) chenye urefu wa 205km.

Majaribio hayo yataanza kwa kujaribu njia ya Umeme wa 25kV kwenye njia nzima ya Reli hiyo. TRC imewataka wananchi wote wa Dar, Moro, na Pwani kuwa makini wakati wa majaribio hayo kwani lolote lile linaweza kutokea.

Majaribio hayo yatafanyika kwa kutumia kichwa Cha TRENI ya Umeme cha Mkandarasi ambacho kiliwasili nchini Mwezi Machi mwaka huu. Majaribio hayo yatakuwa Mubashara TBC.

Ewe Mtanzania na Mzalendo wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, unakaribishwa katika kushiriki uzinduzi huu wa Aina yake katika Historia ya Afrika Mashariki.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika,Amen.
Mgao wa umeme uliotangazwa na Tanesco hivi majuzi umekwisha huko Tanzania au bado unaendelea?

Hivi hilo jaribio lishafanyika? Maana nimefuatilia huu uzi hadi mwisho na sijaona mrejesho.
Ama kila mmoja aliamua kukaa mbali? Ukisikia neno "lolote laweza tokea" yabidi ukae mbali sana.
 
Hivi unajua unachoandika hapa Watanzania wenzio wanasoma na kukushangaa, eti hamna changamoto za umeme Bongo? Huyo waziri Makamba nusra mumtoe nje kisa hayo matatizo.
Wakitangaza wanakata hiyo ni routine maintenance shida iko wapi?
 
Back
Top Bottom