john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 142
- 281
Majaribu 10 ya Waisraeli kwa Mungu tangu Misri hadi Kanaani
Musa ni nani katika safari kutoka Misri hadi Kanaani
Musa ni mtu mmoja maarufu zaidi katika Agano la Kale. Wakati Ibrahimu anaitwa "Baba wa Imani" na mpokeaji wa agano la Mungu lisilo na masharti la neema kwa watu Wake, Musa alikuwa mtu aliyechaguliwa kuleta ukombozi kwa watu Wake. Mungu hasa alimchagua Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka utekaji nyara katika Misri hadi wokovu katika Nchi ya Ahadi ya Kanaani.
Musa pia anajulikana kama mpatanishi wa Agano la Kale na hujulikana sana kama mtoaji wa Sheria. Hatimaye, Musa ndiye mwandishi mkuu wa Torati, vitabu vya msingi vya Biblia nzima. Jukumu la Musa katika Agano la Kale ni aina na kivuli cha jukumu la Yesu katika Agano Jipya.
Tunakutana na Musa mara ya kwanza katika sura za ufunguzi wa kitabu cha Kutoka. Katika sura ya 1, tunajifunza kwamba, baada ya mzee Yusufu kukomboa familia yake kutokana na njaa kubwa na kuiweka katika nchi ya Gosheni (katika Misri), wazao wa Ibrahimu waliishi Misri kwa amani kwa miaka 30, hadi akainuka farao mwingine kutawala Misri, ambaye "hakumjua Yusufu" (Kutoka 1:8).
Farao huyu alitawala watu wa Kiebrania (Waisraeli/Wayahudi) na kuwatumia kama watumwa kwa ajili ya miradi yake mikubwa ya ujenzi. Kwa sababu Mungu aliwabariki watu wa Kiebrania na ukuaji wa haraka wa idadi, Wamisri walianza kuogopa idadi inayoongezeka ya Wayahudi wanaoishi katika nchi yao. Hivyo, Farao aliamuru kifo cha watoto wote wa kiume waliozaliwa na wanawake wa Kiebrania (Kutoka 1:22).
Katika Kutoka 2, tunaona mamake Musa akijaribu kumwokoa mtoto wake kwa kumtia katika kikapu na kumweka katika mto Nile. Kikapu hicho hatimaye kilipatikana na binti ya Farao, naye akamchukua kama wake mwenyewe na akamleta katika kasri ya farao mwenyewe. Musa alipokuwa mtu mzima, alianza kuhisi na taabu ya watu wake, na baada ya kushuhudia Mmisri akimpiga mtumwa wa Kiebrania, Musa aliingilia na kumwua Mmisri. Katika tukio lingine, Musa alijaribu kuingilia kati katika mabishano kati ya Waebrania wawili, lakini mmoja wa Waebrania alimkemea Musa na kusema kwa kejeli, "Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri?" (Kutoka 2:14). Alipotambua kwamba tendo lake la uhalifu limefahamika, Musa, akiwa na miaka 40, alikimbia kwenda nchi ya Midiani ambapo aliishi kwa miaka mingine 40.
Alipokuwa Midiani, alikutana na Mungu kwenye kichaka cha moto (Kutoka 3:4), ambapo Mungu alimwita Musa kuwa mwokozi wa watu Wake. Licha ya udhuru wake wa awali na ombi la wazi kwamba Mungu atume mtu mwingine, Musa alikubali kumtii Mungu. Mungu aliahidi kumtuma Haruni, nduguye Musa, kwa kusudi la kusaidiana naye.
Musa na ndugu yake, Haruni, walienda kwa Farao katika jina la Mungu na kutaka kwamba awaachilie watu kwenda kumwabudu Mungu wao. Farao alikataa kwa kiburi, na mateso kumi ya hukumu ya Mungu yaliwaangukia watu na nchi. Dhiki ya mwisho ilikuwa ni kuuawa wa mzaliwa wa kwanza. Hapo ndipo Farao aliamua kuwaachia Waisraeli.
SAFARI YA MIAKA 40 KUTOKA MISRI HADI KANAAN
Wakiwa njiani kwenda Kanaan, Waisraeli walikuwa na manung'uniko dhidi ya Mungu.
Hesabu 14:22 “kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya, WAMENIJARIBU MARA HIZI KUMI, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona; 24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki”.
Kati ya Misri na Kanaani, maandiko yanaonyesha Waisraeli walimjaribu Mungu mara 10.
Jaribu la 1: Mkabala na bahari ya Shamu
Kutoka 14:9 “Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. 10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana. 11 Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?
12 Neno hili silo tulilokuambia huko Misri”?
Hili ndilo jaribu la kwanza wana wa Israeli walilomjaribu nalo Mungu, ijapokuwa walishaona matendo yake makuu kwa Farao na Misri yote kwa ujumla, jinsi alivyoipiga Misri na kuiharibu kwa ishara kubwa 10 na maajabu mengi. Lakini hapa wanamjaribu Mungu kuangalia kama atawapigania tena kinyume na Farao au la. Jambo hilo ni dhambi kwao kwani tayari wanaujua uweza wa Mungu, na hivyo hapakuwa na haja ya kumjaribu ili kuona atakachokifanya.
Jaribu la 2: Maji ya Mara
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. 24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? 25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko”.
Hili ni jaribu la pili. Baada ya kuona uweza wa Mungu wa kupasua bahari, lakini bado wakamjaribu Mungu kuangalia kama atawafanyia muujiza wa MAJI au la. Na Bwana akawapa maji kama walivyotaka lakini bado hawakuridhika.
Jaribu la 3: Katika bara ya Sini, kutaka Nyama
Kutoka 16:1 “Kisha wakasafiri kutoka Elimu, na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikilia bara ya Sini, iliyoko kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri; 2 Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani; 3 wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote".
Hili ni jaribu la tatu. Baada ya kumjaribu Bwana kwa maji ya Mara, sasa wanataka kumwangalia Bwana kama anaweza kuwafanyia muujiza wa NYAMA katikati ya jangwa, na Bwana akawapa nyama, kama walivyotaka lakini bado hawakuchoka kumjaribu.
Jaribu la 4: Kusaza kwa mana
Kutoka 16:19 “Musa akawaambia, Mtu awaye yote asikisaze hata asubuhi. 20 Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana”
Waisraeli walipewa maagizo wasisaze MANA (yaani wasibakishe chochote mpaka asubuhi), lakini wao wakafanya kinyume chake kwa kusudi la kuchunguza ni nini kitatokea.
Jaribu la 5: Ukusanyaji wa Mana siku ya Sabato
Kutoka 16:26 “Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.
27 Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.
28 Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini? “
Mungu aliwaambia wasitoke kwenda kuokota MANA siku ya Sabato, bali wapumzike, kwa sababu hiyo mana haitapatikana siku hiyo, lakini wenyewe wakatoka kwenda kuhakiki kama kweli haitapatikana? Hiyo ikawa ni dhambi kwao.
Jaribu la 6: Maji ya Refidimu
Kutoka 17:1 “Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. 2 Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe MAJI tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana? 3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?”
Baada ya kumjaribu Bwana kule Mara, kwa kutaka maji, sasa wanarudia makosa yale yale ya kutaka watokezewe maji ya kimiujiza. Kulikuwa hakuna haja ya kumjaribu Mungu mara ya pili kwa suala la maji, kwani tayari walishaona uweza wake mara ya kwanza, lakini wao walitaka kuona tena na tena.
Jaribu la 7: Sanamu ya ndama
Kutoka 32:7 “Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, 8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri”.
Wametoka kunywa maji kimiujiza katika mwamba, na kuhakiki kwamba Bwana yupo katikati yao, lakini hapa wanafanya makusudi, kutengeneza sanamu ya ndama, kama ishara ya kumsusia Mungu, ambaye wanajua kabisa kuwa yupo.
Jaribu la 8: Moto wa Tabera
Hesabu 11:1 “Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago. 2 Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba Bwana, na ule moto ukakoma. 3 Jina la mahali hapo likaitwa Tabera; kwa sababu huo moto wa Bwana ukawaka kati yao".
Manung’uniko haya ni yale ya kutafuta kuona kitu cha kimuujiza kutoka kwa Mungu, kwa sababu walikuwa wameshajua kuwa Mungu anaweza kufanya lolote.
Jaribu la 9: Tamaa ya nyama
Hesabu 11:4 “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? 5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; 6 lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu”.
Wana wa Israeli walitaka NYAMA, si kwa sababu walikuwa na njaa sana, bali kwa sababu walikuwa wanataka kuona kitu kipya kutoka kwa Bwana.
Jaribu la 10: Wapelelezi wa Kaanani
Hesabu 14:1 “Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.
2 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3 Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
4 Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri”.
Hilo ndilo lilikuwa jaribu la mwisho, wana wa Israeli walilomjaribu nalo Mungu. Nalo ndilo likawa muhuri wa wao kuipoteza ahadi ya kuiona ile nchi, isipokuwa watu wa WAWILI TU, AMBAO NI YOSHUA NA KALEBU.
Tunachojifunza kuhusu kumjaribu Mungu
Tunachojifunza katika habari hiyo kuwa ni kuwa kumjaribu Mungu ni dhambi kubwa.
1. Kama tumeshaujua uweza wake, kwa nini tumjaribu?
2. Kama tumeshajua kuwa Mungu anaweza kutuokoa kwenye hatari, kwa nini tujiweke katika hatari ya dhambi?
3. Kama tumeshajua kuwa Mungu anaweza kutuokoa na yule mwovu, kwa nini basi tujisogeze karibu na yule mwovu?
4. Kama tumeshajua kuwa “tutakapokula vitu vya kufisha, havitatudhuru, kwa nini basi tuvile makusudi”?
5. Kama umeshajua kuwa Mungu ni mponyaji, kwa nini basi tunywe sumu makusudi?
6. Kama umeshajua kuwa Bwana anakupenda, kwa nini ujiuze kwenye dhambi ili uujaribu upendo wake? Unadhani utabaki salama?
Ndicho wana wa Israeli walichokuwa wanakifanya, pasipo kujua kuwa wanafanya dhambi kubwa, ambayo itawagharimu kukosa kuingia Kaanani.
Kumbuka kuwa hili ndilo jaribu ambalo shetani anawaangusha nalo watu wengi, hata siku hizi za mwisho. Na ndilo hata alilolichagua kama moja kati ya majaribu yake matatu yenye nguvu kubwa, ili aweze kumwangusha Bwana Yesu, lakini alishindwa:
Mathayo 4:5 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.”
NINI KIFANYIKE
Tusimjaribu Bwana. Hatuwezi kumjaribu baba mzazi, iweje tumjaribu Mungu?
Tusimjaribu Muumba wetu.
Kufanya hivyo ni sawa na kuwa na mashaka na uumbaji wake na uweza wake.
Kufanya hivyo ni sawa na kusema Yesu hakufa msalabani, hivyo hakuna ukombozi uliofanyika.
Kumjaribu Bwana Mungu wako ni kutenda dhambi kubwa, ambayo ilizuia wana wa Israeli kuingia Kanaani. Nasi, kitendo hicho kitatuzuia kuingia mbinguni.