Majaribu makali anayopitia mwanadamu hapa duniani. (hii dunia ina majaribu sana)

Majaribu makali anayopitia mwanadamu hapa duniani. (hii dunia ina majaribu sana)

Hilo ni swali fikirishi sana ila swali ni kwamba nikifa naenda wapi hapo ndipo hofu inakuja hapo tu sio kingine, ila kuna wakati ile hofu hua inaondoka pale tu ninapokua nimetimiza mission fulani hua nasema hapa hata nikifa leo nitakua nimeacha alama hii hata nikirudi nitakuja kuiangalia hii alama niseme hapa niliwahi kuishi ingawa najua kwa kipindi sitoweza kujua niliwahi kuishi lini ni maisha baada ya kifo

ni aina ya maswali wengi kati yetu tunajiuliza je baada ya kifo ninaenda wapi?hayo ndiyo maswali ya msingi,unahisi utaenda wapi mkuu baada ya kifo?🤣🤣
 
ni aina ya maswali wengi kati yetu tunajiuliza je baada ya kifo ninaenda wapi?hayo ndiyo maswali ya msingi,unahisi utaenda wapi mkuu baada ya kifo?🤣🤣
Umeniuliza swali gumu sana, ila mimi nahisi nikifa nahitaji niende nikaonane na ndugu yangu kwa hio nitaenda kuonana na ndugu yangu ambae yeye pia ameshakufa kitambo tu, huyu ndugu yangu kabla hajafa alinipigia simu yaan km siku 4 kabla hajafa alinipigia simu tukaongea sana kuna changamoto alikua anazipitia akawa anahitaji msaada wangu wa mawazo nini afanye nimsaidie kimawazo, nakumbuka nikajitahidi kumshauri ila sikufanya kwa kile kiwango cha kuridhisha yaan nilimshauri kwa kiwango cha chini sana kitu ambacho niliposikia amefariki sikufurahi nikaona km sikumshauri kwa kiwango cha juu laiti km ningemshauri kwa kiwango cha juu sasa hivi angekua bado anaishi, kwa hio nikawa natarajia labda labda km ingewezekana muda ungerudi nyuma ila haikuwezekana sasa ukiniuliza nitaenda wapi basi mimi nitakwambia nitaenda alipo huyo ndugu yangu nikaonane tena
 
muda ukifika huwa hakuna mbadala mkuu labda Mungu mwenye akuepushe,kwenye biblia tunaona mfalme Ezekia aliumwa sanaa sanaa,zikabaki siku chache za yeye kufa akamjeukia Mungu akimlilia nakumuomba amuepushie kifo,mungu akamtuma nabii Isaya akampeleke habari njema kuwa Mungu kamuongezea siku za kuishi na maombi yake Mungu ameyasikia.Kwahiyo kifo ni fumbo lakini Mungu pia anauwezo wa kukubadilishia siku yako ya kufa ukimlilia,tumeona wagonjwa wangapi wanakaribua kufa wameumwa miaka lakini anakuja kupona,hapo usijilaumu rafiki yako muda ulifika
 
Unasema muda ulifika ni kweli ila chanzo ndio kinanifikirisha zaidi ingawa yote kwa yote ni kazi yake Maaulana; tusije tukakufuru hapa.
 
13
Yer 17:5 SUV
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mtumishi wa Mungu mmoja alianzisha huduma yake ya kiroho kanisa katika moja ya vijiji(Ukerewe)..eneo hilo lilikuwa na nguvu za giza kwa kiasi kikubwa na idadi kubwa ya washirikina.

Huduma yake ikafanikiwa kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwafungua wengi waliofungwa na vifungo vy kishirikina uchawi..akapata waumini wengi sana kanisa likaendelea kukua kila siku na idadi ya waumini kuongezeka kila uchwao.

Washirikina wa eneo hilo wakapata pigo kubwa maana wanakijiji wengi waliponywa.

washirikina hao hawakufurahi wakaweka kikao wakamtengenezea UGONJWA wa kansa...wakamtupia ukampata..

Na Mungu aliruhusu hilo jaribu limpate kama ilivyokuwa kwa AYUBU wa kwenye biblia (Jaribu ni mtaji wa kuongeza imani)
Mungu hataruhusu jaribu lililo nje au juu ya uwezo wa mwanadamu,majaribu tinayopata ni yale ambayo ni ya kawaida kwa mwanadamu,na Mungu huwa anaweka na njia za kutokapo,mlango wa kutokea kwenye hilo jaribu..

Sasa mtumishi wa Mungu yule alipopata huo uginjwa wa KANSA alipokwenda hospitali madokta wakamwambia huu ugonjwa hauponi hauna tiba hospitali..

Mtumishi wa Mungu akahuzunika sana akakata tamaa ,akamkasirikia Mungu...akasema yani Mungu umeruhusu huu ugonjwa wa kansa unipate mimi mtumishi wako pamoja na kikutumikia kwa kiasi hiki chote..kujitoa kwangu kote ..kufanya kazi yako ina maana huioni ..ndio ukaamua ukubali nipate huu ugonjwa...akamchukia sana Mungu..

Katika wale wachawi mmoja wapo ni mtu wake wa karibu kanisani..

Akamfuata mtumishi akamshauri...kama hospitali wamwshindwa kukutibu..jaribu nikupeleke kwa MTAALAMU anaweza kukuponya kama huko kwingine wameshindwa ...

Mtumishi akamkasirikia Yesu akasema ..Kama wewe Yesu umeruhusu niumwe basi ..acha nijarubu kwingine..

Akaenda kwa mtaalamu sangoma mganga wa kienyeji..ambaye naye ni mshirikina ..ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu kwakua ..kanisa lake na maombi ya kanisa lake yalikuwa yanaleta uharibifu mkubwa katika kuathiri nguvu zao na mambo yao ya kishirikina ..alikuwa maombi ya walokole yanavuruga na kuharibu kabisa kazi zao za kishirikina..

Siku ya nne tu toka aende kwa mtaalamu mtumishi akafariki..

Mungu ni Mwaminifu: 1 Wakorintho 10:13 inasisitiza kuwa Mungu hataacha ujaribiwe kupita uwezo wako, bali atafanya mlango wa kutokea.

Yakobo 1:2-18
Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote

1 Kor 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Mwanzo 22:1-2 ”Ikawa baada ya mambo hayo MUNGU alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

Mathayo 24:13 ” Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”

Zaburi 11:5 ‘’BWANA humjaribu mweyehaki Bali nafsi yake humchukia asiye haki na mwenye udhalimu’’
Jaribu la MUNGU ni kipimo tu cha MUNGU kama kweli unampenda.

AYUBU ALIJARIBIWA AYUBU NI MFANO BORA WA MWANADAMU ALIYESTAHIMILI MAJARIBU NANKUSHINDA ...soma kitabu cha AYUBU katika biblia.
Mungu atusaidie tusimame katika Imani thabiti bila kuyumbayumba.
 
Zaburi 11:3-5
3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

4 Bwana yu katika hekalu lake takatifu. Bwana ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu.

5 Bwana humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.

hilo andiko hapo juu,ni ufafanuzi kuwa, ukiona majaribu mengi yapo juu yako basi ujue Mungu anakupenda sana anasema hupenda kuwajaribu wenye haki,ni yeye amekujaribu na ni yeye atakuvusha✅
 
Kitu cha pekee ambacho biblia inajaribu kuangazia na naheshimu tofauti na vitabu vingine ni nadharia yake juu ya matatizo ya watu

Haichukulii kwamba mtu ukizaliwa ni nweupe bali inadodosa juu ya changamoto zako sio lazima ziwe zako

Watu wanazaliwa kwenye Malango ya damu yenye changamoto kubwa sana

Huu ni Ufahamu mkubwa sana ukiwa bado unapumua ili kusivive kwa saburi
 
Mathayo 11:28 SRUVDC
Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

1 Petro 5:7
Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.
 
Attachments

  • Screenshot_20260324-113242.jpg
    Screenshot_20260324-113242.jpg
    75.3 KB · Views: 11
Back
Top Bottom