Majaribu makali anayopitia mwanadamu hapa duniani. (hii dunia ina majaribu sana)


ni aina ya maswali wengi kati yetu tunajiuliza je baada ya kifo ninaenda wapi?hayo ndiyo maswali ya msingi,unahisi utaenda wapi mkuu baada ya kifo?๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
ni aina ya maswali wengi kati yetu tunajiuliza je baada ya kifo ninaenda wapi?hayo ndiyo maswali ya msingi,unahisi utaenda wapi mkuu baada ya kifo?๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Umeniuliza swali gumu sana, ila mimi nahisi nikifa nahitaji niende nikaonane na ndugu yangu kwa hio nitaenda kuonana na ndugu yangu ambae yeye pia ameshakufa kitambo tu, huyu ndugu yangu kabla hajafa alinipigia simu yaan km siku 4 kabla hajafa alinipigia simu tukaongea sana kuna changamoto alikua anazipitia akawa anahitaji msaada wangu wa mawazo nini afanye nimsaidie kimawazo, nakumbuka nikajitahidi kumshauri ila sikufanya kwa kile kiwango cha kuridhisha yaan nilimshauri kwa kiwango cha chini sana kitu ambacho niliposikia amefariki sikufurahi nikaona km sikumshauri kwa kiwango cha juu laiti km ningemshauri kwa kiwango cha juu sasa hivi angekua bado anaishi, kwa hio nikawa natarajia labda labda km ingewezekana muda ungerudi nyuma ila haikuwezekana sasa ukiniuliza nitaenda wapi basi mimi nitakwambia nitaenda alipo huyo ndugu yangu nikaonane tena
 
muda ukifika huwa hakuna mbadala mkuu labda Mungu mwenye akuepushe,kwenye biblia tunaona mfalme Ezekia aliumwa sanaa sanaa,zikabaki siku chache za yeye kufa akamjeukia Mungu akimlilia nakumuomba amuepushie kifo,mungu akamtuma nabii Isaya akampeleke habari njema kuwa Mungu kamuongezea siku za kuishi na maombi yake Mungu ameyasikia.Kwahiyo kifo ni fumbo lakini Mungu pia anauwezo wa kukubadilishia siku yako ya kufa ukimlilia,tumeona wagonjwa wangapi wanakaribua kufa wameumwa miaka lakini anakuja kupona,hapo usijilaumu rafiki yako muda ulifika
 
Unasema muda ulifika ni kweli ila chanzo ndio kinanifikirisha zaidi ingawa yote kwa yote ni kazi yake Maaulana; tusije tukakufuru hapa.
 
Mungu atusaidie tusimame katika Imani thabiti bila kuyumbayumba.
 
Zaburi 11:3-5
3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

4 Bwana yu katika hekalu lake takatifu. Bwana ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu.

5 Bwana humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.

hilo andiko hapo juu,ni ufafanuzi kuwa, ukiona majaribu mengi yapo juu yako basi ujue Mungu anakupenda sana anasema hupenda kuwajaribu wenye haki,ni yeye amekujaribu na ni yeye atakuvushaโœ…
 
Kitu cha pekee ambacho biblia inajaribu kuangazia na naheshimu tofauti na vitabu vingine ni nadharia yake juu ya matatizo ya watu

Haichukulii kwamba mtu ukizaliwa ni nweupe bali inadodosa juu ya changamoto zako sio lazima ziwe zako

Watu wanazaliwa kwenye Malango ya damu yenye changamoto kubwa sana

Huu ni Ufahamu mkubwa sana ukiwa bado unapumua ili kusivive kwa saburi
 
Mathayo 11:28 SRUVDC
Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

1 Petro 5:7
Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.
 

Attachments

  • Screenshot_20260324-113242.jpg
    75.3 KB · Views: 11
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ