Majaribu yapo kwaajili ya Binadamu, likikupata ujue ndio wakati wako ulikuwa umefika.

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
563
Reaction score
1,567

Maisha Ni Fumbo

Katika kutembelea mitandao, nimekumbana na video moja inayogusa moyo na maisha pia. Katika video hii kuna huyu mama akiwa na mwanae huyu anaonekana hana mikono yote, kwani imekatikia kwenye viwiko. Katika masaibu yaliyomkuta mimi na wewe msomaji hatujui, anafahamu yeye mwenyewe katika harakati zake, inaonyesha alizaliwa mzima kabisa ukiangalia kwa umakini. Hali hii kwa hakika inaleta huzuni sana, lakini kinachogusa zaidi ni jinsi anavyoishi kwa furaha, hajutii vile alivyo na yuko na smiles safi tu huku akimenya ndizi zake kwa ustadi mkubwa kwa kutumia sehemu ya mikono iliyobaki, na hata kumsaidia mwanawe kwa upendo mkubwa.

Ni picha yenye maumivu ndani yake, lakini pia ni somo kuu kuhusu ujasiri, shukrani na matumaini. Hii siyo hadithi ya kusimuliwa, bali ni kitu unachokiona kwa macho kupitia video hii, inazungumza mengi kuliko maneno.

Nimejikuta najiangalia na mimi:
Katika maisha yangu, nipende kushukuru jinsi nilivyo. Nipende kuthamini afya niliyonayo, nguvu nilizopewa, na hali yangu hata kama si kila kitu kiko sawa. Kwa kweli, najiona kama nimependelewa sana kuwa hivi nilivyo. Naamini kuna sababu kubwa juu ya hayo yote.

Wapo waliokuwa na viungo kamili, lakini baadaye maisha yakachukua mkondo tofauti si kwa sababu wameonewa, bali kwa sababu ambazo sisi hatuwezi kuelewa kwa sasa. Zimetimia juu yao, kwa namna yake Mungu anavyojua.

Hii imenifanya niseme: Asante kwa afya. Asante kwa uzima. Asante kwa uwezo wa kufanya hata yale madogo tunayoyadharau kila siku.

Ni muhimu tukumbuke kuwa maisha haya ni fumbo safari isiyoeleweka kikamilifu, lakini tunayoishi kwa neema. Kila siku ni zawadi, na kila pumzi ni baraka. Tusisahau kushukuru, tusisahau kuishi kwa moyo wa matumaini, na tusisahau kujifunza kutoka kwa wale wanaoendelea kupambana, hata katika hali ngumu kuliko zetu.
 
View attachment 3293192

muhimu tukumbuke kuwa maisha haya ni fumbo safari isiyoeleweka kikamilifu, lakini tunayoishi kwa neema. Kila siku ni zawadi, na kila pumzi ni baraka. Tusisahau kushukuru, tusisahau kuishi kwa moyo wa matumaini, na tusisahau kujifunza kutoka kwa wale wanaoendelea kupambana, hata katika hali ngumu kuliko zetu.💪🏿👌🏿
 
Back
Top Bottom