Ahyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2019
- 2,310
- 5,482
Tuseme kupata hitilafu kwa ndege hiyo kumetokana na sababu za kimawasiliano...Ww Hadi muda huu unadhani ni nani kahusika kwa nini Ndege yake tu ianguke! usihamishe magoli
Tujiulize je hiyo ndege inaweza kuongozwa na mtu tofauti na Rubani wake..?? Kama ndio, basi uwezekano huo wa kuuwawa upo...
Je walipoteza uelekeo na mawasiliano na watu wa chini mara baada ya kuwa angani..??
Basi tuseme imelipuliwa, je kuna ishara yoyote hadi sasa kuonyesha imelipuliwa..??
Je kuna movement yoyote ya kutiliwa shaka kabla/baada ama wakati wa hafla iliyomkutanIsha Raisi na rais wa Azerbaijan..??
Kama ataleta taarifa ambayo ina moja ya hayo mambo kutokea kabla ya tukio, nitaamini kwamba ameuwawa, vinginevyo ni hisia tu ambazo hata mm ninazo kutokana na
_Viongozi wengi wa Iran wamekufa kwenye ajali kama hiyo na ikasemwa wameuwawa
_Nilikutana na taarifa kwamba kuna ndege ya US airforce ilitua Azerbaijan muda wa tukio...
_Rais wa Marekani kuita kikao cha dharura baada kuthibitishwa kwa kifo cha rais wa Iran
_Urusi kafanya kikao cha dharura na balozi wa Iran nchini Urusi
Lakini pia kunahatari kubwa mbeleni, ambayo kila mtu anajaribu kuiepuka