Majenereta ya umeme ni ya nani haya jamani?

Tanzania kuna viwanda vya uongo. Njooni Iringa muone mto Ruaha kuanzia bonde la usangu kote kumekauka, mtera, pangani n.K maji yatatoka wapi?

Ni kosa kubwa kutegemea umeme wa maji badala ya vyanzo vingine kama gesi na upepo.
Usituaminishe ujinga we ,unazani si ni wapimbuvu
 
Kuna kampuni inayo majenereta kama hayo inauza kitambo sana, toka enzi za Jakaya, Magu mpaka sasa...
 
Si wa kuamua kwenye masanduku ya kupiga kura.
Wakiibiwa kura ambayo ni haki yao wanakaa kimya.
Si wa kupinga vitendo viovu!
Si wakuandamana wala kugoma.
Yaani kwa kifupi hatuna ujasiri, umoja wala mshikamamo.
Siku tikiungana kama wenzetu kule Uarabuni miaka ya nyuma au Iran kwa sasa naamini kabisa hawa wakoloni weusi ndio wangejua sasa wa Tz wameamka na wasingerudia tena haya wanayotufanyia!
 
Tanzania kuna viwanda vya uongo. Njooni Iringa muone mto Ruaha kuanzia bonde la usangu kote kumekauka, mtera, pangani n.K maji yatatoka wapi?

Ni kosa kubwa kutegemea umeme wa maji badala ya vyanzo vingine kama gesi na upepo.

Hususan kwa mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo hata rais mwenyewe alihudhuruia kikao huko Ulaya.
 
Umeongea kifalsafa MNO.

Utasikia hao wapuuzi wanauliza, "Mbona CHADEMA wako kimya?" utadhani wakati wa UKUTA hao wanaouliza leo kwa nini CHADEMA wapo kimya, waliwaunga mkono CHADEMA.
 
Yaani hizi maneno huwa tunaongea kukemea au kuwasemea viongozi huwa inawapa jazba sana na kuamua kukomoa kabisa
 
Naona Bakora za kuwachapia Wanzanzibara zimewasili.
Kata umeme,tununue jenereta,utaki unaacha!
"Hapo Wanzanzibara ni kuamua tu namna ya kumsitiri Marehemu;tuamue Kama tunazika hapahapa au tunasafirisha"
Dadeek!
 
hoja yako ningefikiria mara mbilimbili kama usingeweka picha hiyo, maana inaonyesha ushabiki na uchonganishi tu wala si uhalisia. picha hiyo imepigwa kama sio deport basi ni bandarini wakati yanapakuliwa. hatujui pengine yalikuwa on transit to burundi or congo drc, halafu pia hayo ni heavy duty ningekuelewa kidogo kama ungebandika majenereta ya kawaida kabisa na yametapakaa madukani kariakoo, magomeni, mwandiga, kirumba. hapo ningekuelewa kuwa kumbe mgao wa umeme unachochea biashara ya majenereta
 
Mwanzoni nlidhani ww ni great thinker kumbe ushakua na akili za JPM. Sasa lini majenereta hayajawahi kuagizwa nchi hii kiasi yakija ndio eti yauze kukiwa na mgao!! Are you serious?

Leo hii mnajiskiaje umeme unawaka non stop wakati mlisema ni uongo
 
Mbona mradi wa ziwa Victoria upo sana tu na Maji yameshavuka Hadi Nzega kuelekea Singida!! Hamfanyi tafiti kazi kuropoka tu. Mambo ya mabwawa kukauka yapo na ndio maana serikali imehamia kwenye gesi ila Kwa kuwa ni wakosoaji wa Kila kitu hamuoni kma ni progress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…