Majeneza getini mwa Hospitali ya Amana hayaleti taswira nzuri kwa Wagonjwa.

Tuliza mshono watu wapigwe hela
 
Ni kama fisi kwenye mzoga wa swala uliouliwa na simba sio?
 
Mbaya zaidi ukute ni biashara ya daktari unaenda kukutana naye mnafanya bagain uko uko🥴🥴🤣🤣
 
Mtoa mada Yuko sahihi,mwingine akiona tu pressure inapands Hata kama katoka hana shida hiyo.
 
Biashara yoyote inalenga potential customers hiyo ndo sehemu sahihi ya hiyo display ya biashara, huwezi kupeleka biashara ya vipuri vya magari karibu na hospitali sio mahara pake au upeleke jeneza jaribu na bar au guest house.
Bado hujashirikisha ubongo
 
Hujayaona pale Muhimbili?na sasa ni kama fasheni kila hospitali hapa nchini utakutana na mageneza mlangoni.
 
Petrol station kwa pembeni lazima kuna WAZIBA PANCHA
 
Yaani umesema kweli kabisa. Mimi nikipita pale hufumba macho. Inatia simanzi kwa mgonjwa inaleta hofu na mshituko. Wahusika toeni maelekezo kwa wauzaji wasi display namna ilivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…