Joanah
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 22,527
- 79,976
Looh!! 😃Kabisa na marketing pia, imagine unaenda na mgonjwa wako accidentally macho yamekutana na jeneza Zuri mpaka mwenyewe umelitamani, 😀 , M.Mungu atuepushie tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Looh!! 😃Kabisa na marketing pia, imagine unaenda na mgonjwa wako accidentally macho yamekutana na jeneza Zuri mpaka mwenyewe umelitamani, 😀 , M.Mungu atuepushie tu.
Basi sawaHii iko wazi
Hakuna kiumbe anaweza kubisha
....aaaaah kuna daktari aliwahi kuniambia kauli kama ya karibu tena...akajishitukia akaipoza...nilimuuliza hivi siku hizi mnatumia mashine hii kupima?! ...akasema mbona ya muda tu...hujawahi kuiona wakati wewe ni mteja wetu wa mara kwa mara!Sina uhakika mkuu kwenye majeneza
Lakini hospitali huwa hatuwaambii wagonjwa wakaribie tena
Sasa mkuu tusipokufa kupungua wengine wataishi wapi?sadly 2090 humu patakua na comments, reply na avatar za marehemu kibao
dah hakuna kitu kibaya kama kifo nachukia sana kifo mimi
Sio tu kwa mgonjwa ila hata wewe ambae unampeleka mgonjwa wako ambae yupo seriously ukiaona lazima ujisikie vibaya.Habari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.
Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.
Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.
Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.
NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.
Ahsante.
Kwanini?Jamiiforums haitakuwepo tena
NAunga mkono hoja kiukweli hii si sawa hata kidogo. Kisaikolojia imekaa vibaya sanaHabari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.
Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.
Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.
Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.
NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.
Ahsante.
Ni utabiri kutoka kwangu.Kwanini?
Oke oke mkuuNi utabiri kutoka kwangu.