Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

Hujui chochote, Wachina wamezagaa DRC wana migodi ya Cobalt, dhahabu n.k kila kona, wanavuna magogo pande zote za nchi na ndio wanaongoza kuchota rasilimali za hiyo nchi kwa kibali cha serikali ya DRC na njia haramu pia.
Kuzagaa wapi Sasa tofauti na eneo.la Eastern DRC North to South
 
Kuna Baadhi ya Watanzania walihusishwa na Kukamatwa kama.magaidi huko.

Hawakuomba Kwa sababu ya vibaraka waliojaa jeshini
Endelea kubaki na tope la akili za kijima za vibaraka wakati wenyewe wanasonga mbele. Kama unafikiri vibaraka ni tatizo anza kwanza kwa kuacha kutumia simu, tablets, flash na computer zao kwa sababu zinatumia madini ya DRC yanaouzwa na Wachina. Zikataeni pesa zao zinazochangia mtaji benki ya Africa unayoipamba inayokuja Dar kufanya mkutano wa nishati, vinginevyo wazalendo uchwara hamna tofauti na chichidodo.
Kalaghabao.
 
Endelea kubaki na tope la akili za kijima za vibaraka wakati wenyewe wanasonga mbele. Kama unafikiri vibaraka ni tatizo anza kwanza kwa kuacha kutumia simu, tablets, flash na computer zao kwa sababu zinatumia madini ya DRC yanaouzwa na Wachina.
Sasa vibaraka wataachaje kusonga mbele kama Wazalendo hawaungani? Najua wewe ni matusi unatetea ndugu zako kupora arhsi na Mali za DRC.
 
Yaani wakongo wako bize kujichumbua na kukatika sebene alafu sisi tutume vijana wetu waende kufia nchi yao.

Kiufupi kongo ni taifa lililo feli bora ligawanyike tu wenda wakongo wakaishi kwa amani.
 
Yaani wakongo wako bize kujichumbua na kukatika sebene alafu sisi tutume vijana wetu waende kufia nchi yao.

Kiufupi kongo ni taifa lililo feli bora ligawanyike tu wenda wakongo wakaishi kwa amani.
Maeneo yakikombolewa na kukabidhiwa wao baada ya miezi kadhaa mbeleni yanarudi kwa waasi.

Nashindwa kuwaelewa kabisa!

Suluhisho bora nchi yao imegwe vipande vipande ndipo watakuwa na akili na kujua walichokipoteza.

Kwa sababu hata serikali yao sioni cha maana wanachokifanya. Wanatumia mgogoro huu kama siasa njia ya kukwaa madaraka.

Hawa dawa ni kuwaacha hivyo hivyo na matatizo yao!
 
Pitieni na hapa mpate idea vyema..
 
Vijana wa kikongo wamejazana Dar na Ufaransa kazi kupaka wanja na hina alafu eti nchi nyingine zitume vijana wao wafie nchi iliyo jaa wapumbavu kama hao.
Nchi yenyewe kuanzia rais mpaka mwenyekiti ya kitongoji wananuka rushwa.
Hili nchi ligawanyike tu like pinching vidogo vidogo ili raia waishi kwa amani wanateseka sana mpaka huruma.
 
Nawashauri jwtz waache kujifanya kimbelembele katika vita na m23. Wakumbuke m23 wana kisasi kikubwa na jwtz. Jeshi letu wanapaswa kuwa wajanja na sio kujifanya wazalendo kufa kwa ajili ya wakongo wakati nchini mwao bandari zimeuzwa na hifadhi wala hawajafanya lolote.

Ushauli wangu, ukikuta wenzio wanapiga dili na wewe piga. Rwanda ni wajanja wanaiba mali za kongo wanajenga rwanda kwa nini jwtz wasiige kwa wenzo?

Wakishupaza shingo wengi hawatarudi. M23 ya sasa sio ile ya kipindi cha kikwete. Hata kipindi kile tuliwashinda kwa tabu sana sembuse wakati huu ambapo wamejipanga kikamilifu. Mali za kongo acha ziibwe ni nyingi sana na hawana uwezo wa kuzilinda wala kuzitumia hizo akili hawana acha wenye akili wazitumie. Mbona sisi tumeachia za kwetu?
 
JWTZ haiko kule kupigana na waasi Bali kulinda amani.
 
Kusema ni rahisi sana ila kumbuka kina P.Lumumba waliburuzwa mjini kwenye Barabara na hakuna hata kabuli lao.
Yako wapi makaburi ya watu zaidi ya 3,000 wa Bakwanga waliouwawa na majeshi yake yalipovamia eneo la South Kasai??
 
Yako wapi makaburi ya watu zaidi ya 3,000 wa Bakwanga waliouwawa na majeshi yake yalipovamia eneo la South Kasai??
Ukiwa kwenye ukombozi wa Nchi Yako vibaraka wowote ni Haki Yao kusagwa.
 
Wewe huna hoja kabisa na hata hujui hiyo M23 ilianza anzaje. Nyie ni wale wa vijiweni wanaoachwa hivyo hivyo walivyo.
 

JWTZ warudi nyumbani ili waje kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi yetu, waachane na hiyo Vita ya huko Goma Congo DR. Mambo ya ngoswe aachiwe mwenyewe ngoswe!

Hatma ya Congo DR ipo mikononi mwa WaCongoman wenyewe!
 
JWTZ warudi nyumbani ili waje kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi yetu, waachane na hiyo Vita ya huko Goma Congo DR. Mambo ya ngoswe aachiwe mwenyewe ngoswe!

Hatma ya Congo DR ipo mikononi mwa WaCongoman wenyewe!
Hawapigani na M23 Bali wanalinda amani chini ya MUNOSCO.
 
Wewe huna hoja kabisa na hata hujui hiyo M23 ilianza anzaje. Nyie ni wale wa vijiweni wanaoachwa hivyo hivyo walivyo.
Hujui kitu unachoongea kabisa wewe. Weka hoja zako mezani, tujadili. Hapa siyo sehemu ya kuja kuchamba
 
Wamefeli Kwa kupenda au Kwa kuzidiwa na vibaraka wa Mabeberu kina Rwanda na wengineo?

Hao wanatakiwa kusaidiwa acha upuuzi
Wakuu wa jeshi na intelijensia drc wananufaika na hivyo vita,kutwa kuuza siri za mchezo, colonel mamadou aliwadhibiti m 23,raia wakampenda,wakuu wakachukia,wakamlipua,akaungua kama ndavu ndani ya gari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…