Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

We ndio mpuuzi kushadadia upuuzi wa wakongomani waliofeli kulinda mipaka ya nchi yao.

Hata Tz kupeleka majeshi huko ni kujipendekeza tu na kutumia resources za nchi bure.

Wakongomani hawajielewi,acha kusuport wakata viuno walioshindwa kuiendesha nchi yao.
Mkuu kesho ukiwa manamba huko Rwanda unachuma kahawa usilalamike
 
Kama kagame ndie anae husika inabidi apumzishwe yeye kwanza ndio mengine yafuate. Ni kutumia kanuni ya kwenye biblia. Piga mchungaji ili kondoo waatawanyike
 
Hiyo habari ya MONUSCO hapana Kwa sababu wamekuwepo hapo hakuna Cha maana wamefanya
Umoja wa afrika na nchi zake waache kuutegemea umoja wa mataifa kwa mambo yanayogusa maslahi ya Africa. Umoja wa mataifa haukuundwa kwa lengo la kutetea maslahi ya Africa. Africa ndiyo inapaswa kuwa front kutetea maslahi yake. Lakini pia kuwe na faida katika kuteteana. Siyo kupigana kwa ajili ya nchi Fulani, halafu zikija deal viongozi wanakimbilia kwa wachina au wazungu kufunga mikataba
 
It's true kwamba hali ya usalama mashariki mwa DRC, hususan katika Mji wa Goma, ni ya kusikitisha na inahitaji hatua za haraka. Ni wazi kwamba kundi la M23 linaungwa mkono kwa njia moja au nyingine na maslahi ya kigeni, jambo linalosababisha changamoto kubwa kwa majeshi ya DRC na hata kwa vikosi vya kulinda amani kama JWTZ.

1. Ushirikiano wa Kikanda
Tatizo hili haliwezi kushughulikiwa na JWTZ pekee. Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinapaswa kushirikiana kwa dhati kuhakikisha amani na usalama vinapatikana. Ushirikiano wa kijeshi, kiintelijensia, na kifedha kati ya nchi hizi ni muhimu katika kuzuia juhudi za vibaraka wa kigeni kama M23 kuleta vurugu zaidi.

2. Mgogoro wa Kihistoria
Mgogoro wa M23 si jambo jipya, bali ni suala la muda mrefu linalotokana na changamoto za kikabila, rasilimali, na ushawishi wa kigeni. Hatupaswi kupuuza kwamba DRC ni nchi yenye rasilimali nyingi zinazotamaniwa na mataifa makubwa. Hili limefanya baadhi ya nchi jirani kushawishika kuunga mkono vikundi vya waasi kwa maslahi yao binafsi.

3. Udhibiti wa Rasilimali
DRC ina rasilimali za kutosha kuinufaisha Afrika nzima, lakini badala yake, rasilimali hizi zimekuwa chanzo cha migogoro na ushawishi wa nje. Kama Afrika, tunapaswa kuungana ili kulinda rasilimali hizi kwa manufaa ya watu wa DRC na bara lote. Vita vya M23 si vita vya ukombozi, bali ni juhudi za kulinda maslahi ya mabeberu kupitia vibaraka wao.

4. Mapendekezo ya Haraka

Umoja wa Mataifa unapaswa kuongeza msaada wake kwa MONUSCO ili kuhakikisha wanajeshi wa kulinda amani wanapata vifaa na msaada wa kutosha.

Vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia vinapaswa kuwekwa dhidi ya nchi yoyote inayothibitika kuhusika na kufadhili M23.

AU na EAC zinapaswa kuongeza juhudi za kidiplomasia kwa kushawishi mazungumzo ya amani kati ya DRC na nchi jirani zinazotuhumiwa.


5. Ushauri kwa JWTZ
JWTZ linapaswa kuendelea kushikilia wajibu wake wa kulinda amani bila kuvuka mipaka ya majukumu yake. Tukumbuke kwamba JWTZ liko DRC kulinda amani, si kushiriki moja kwa moja katika vita. Hili ni muhimu ili kulinda taswira ya jeshi letu kimataifa na kuepuka matokeo ya muda mrefu kwa Tanzania.

6. Umuhimu wa Diplomasia
Badala ya kupigana vita vya moja kwa moja, juhudi za kidiplomasia zinapaswa kuimarishwa. Rwanda na nchi nyingine zinapaswa kushauriwa kuachana na siasa za kuunga mkono vikundi vya waasi. Hili linaweza kufanikishwa kupitia shinikizo la kidiplomasia na kisiasa kutoka kwa AU na jumuiya ya kimataifa.

Mwisho wa yote::;
Mgogoro huu hauwezi kutatuliwa na jeshi moja pekee au nchi moja pekee. Tunahitaji mshikamano wa kikanda na wa bara zima kuzuia uchokozi huu wa M23 na kuhakikisha kwamba DRC inabaki kuwa nchi huru na salama.
Waigawie Rwanda tu hicho kisehemu ili amani irejee. DRC ni kubwa mno na imejaa misitu na Wakongoman wameshindwa kuitawala ipasavyo. Kuna ubaya gani kumgawia mwenzie kaeneo ili naye aongeze kidogo ka nchi kake ambako ni kadogo mno?
 
Inakera sana kuona Baadhi ya Nchi za Kiafrika zimejikausha na kuisusa DRC Kwa kuiacha inagukie kwenye mikono ya Jeshi la Vibaraka wa Wazungu M23 Kupitia Rwanda.

Ni kama Wameisusia Tanzania peke yake kiasi kwamba inaweza ikawa ngumu Kwa JWTZ Kuzuia hao Vibaka kuuteka Mji wa Goma ikizingatiwa kwamba watakuwa wanapewa vifaa vya Kisasa ,kusaidia inteligensia nk na Mabeberu. Soma JWTZ yatoa sababu 200 zilizoifanya Tanzania ipambane na waasi wa M23

Wananchi wa DRC wa Imani na JWTZ lakini Sina hakika kama wao yao wataweza kuwazuia M23 ikizingatiwa kwamba JWTZ Iko huko kulinda amnani na sio mstari wa mbele wa Vita,wanatakiwa kuwa mstari wa mbele NJ Jeshi la DRC lakini ndio Hilo limezidiwa.Inatia sana hasira.👇👇

View: https://youtu.be/Fs7jEBnCRJU?feature=shared

My Take
Nchi zingine za Kizalendo Ziungane kuzuia huu uhuni wa Rwanda.

Ikumbukwe Rwanda Kwa Sasa imepunguza sana biashara na Tanzania na bidhaa zao nyingi wanapitishia Bandari ya Mombasa.

View: https://youtu.be/yi8VlUZYe84?feature=shared

Mimi nionavyo ili amani iwepo hapo congo Kuna mawili, ama congo yote ipinduliwe ingozwe na M23,ama mamlaka zikubali kufanya mazungumzo na hao waasi.
 
Wezi wa hizo rasilimali ndio wenye soko pia, hata kama hao m23 wasipokuwepo watakuja wengine. Huyo Tshekedi alikuja moto hushangai amepoa kwa nini kashausoma mchezo nae anaucheza. Wewe unaedai kwa nini Tanzania tuu jitathmini sababu yeye pia anacheza part yake. Nyerere peke yake aliekataa kuchimba hizo mnazoita rasilimali mpaka tutakapokuwa tayari aliona mbali sema ndio hivo wakati ukuta.
 
Kama kagame ndie anae husika inabidi apumzishwe yeye kwanza ndio mengine yafuate. Ni kutumia kanuni ya kwenye biblia. Piga mchungaji ili kondoo waatawanyike
Zakaria 13:7
 
Kuna nchi afrika ambayo sio chawa wa mabeberu?

M23 wachukue goma na miji mingine,wajitangazie nchi mpya ya kivu.

Drc kongo ni failed state acha wenye nguvu waigawane.
Kibaraka mmoja wao Kenya kapeleka majeshi Haiti kwasababu mabeberu wamemtaka afanye hivyo. Kwenye nchi ya watu weusi na kupewa vihela vya chai wakati wao mabeberu waliipiga Libya,Iraq na Syria na kuiba rasilimali zao.

Sasa kwanini Kenya isipeleke jeshi Congo kama kweli anataka Amani tena kwa jirani yake. Lakini kama unavyosema anasubiri mabeberu wampe amri na ahadi ya hela ya chai.
 
Tatizo sio kagame pekee yeye ni moja ya tatizo, hata serikali yenyewe ni tatizo pia, haiko stable pia East Africa nayo ni tatizo vilevile beberu amefanikiwa kuivuruga system kingine jiografia ya DRC pamoja na mali walizonazo ni ngumu kujilinda na fisi beberu. Huu mgogoro DRC atumie akili sana kuusolve.

Kwa mawazo yangu mjumbe hauawi
1. Kwanza kabisa nchi ile waigawe katika zone kanda maalumu kama 5 au zaidi wherever kulingana na rasilimali zao yaani sehem ya madini flan, au sehem ya msitu fulani zile zinazoweza kuingiza kipato cha nchi
2. Waangalie ni zone gani inaingiza zaidi kuliko zote au yaani tajiri kuliko zote. Zone gani yenye vurugu je hio zone yenye vurugu iko location tofauti tofauti au iko location moja, kinachotakiwa kufanyika waasi wote wa nchi watengewe kwenye zone moja kwa namna yoyote ile hata kama hio zone ina utajiri wa nchi nzima
3.Changamoto ni kubwa sana kutokana na beberu katika kufanikisha hili lakini hapa hakuna kucheka na kima hio zone iliyotengwa serikali iiache kwa muda kwa kuweka ulinzi wa kiudhibiti kiasi kwamba waasi wahisi wameachwa kabisa lakini hizi zone zingine ziwa active sana kichumi na kimaendeleo wawekeze miundo mbinu pia sana tu.
4.Mkakati unaofuata ni kuhakikisha mji huo wana u depopulation Kwa Kwa namna yoyote ile kwa hakuna kupeleka dawa au zinaenda Kwa volume ndogo, hakuna uzalishaji wowote yaani ina kua abandoned city hakuna development yoyote iende kule na hakuna mtu kutoka kule unless akimbie nchi au awe cleared sana, watengenezewe zengwe la magonjwa bio weapons hapa ni pagumu hapa itaenda na aliyepo na asiye kuwemo kwa maslahi mapana ya nchi.
5. Zone hio population ikipungua sana wanaitisha sitisha zoezi la magonjwa hapo sasa kisha clean wanaigeuza kuwa military zone wanajeshi wa DRC n wazembe hivyo inasainiwa contract maalum na JWTZ au warusi basi hakuna zaidi ya hapo pana kuwa na kambi zaidi ya 300 na silaha za kila aina hapo beberu atasumbua mno.
6. Mwisho kabisa hakuna mtu atajenga nchi ya wakongo na wao wabadilike pia toka mioyoni mwao waache kutafuta madaraka kwaajili ya maisha yao wajihurumie na vizazi vyao wapiganie congo kweli na wajue wako vitani dunia nzima inapotolea macho wao wanaenda Ufaransa eti ndio dream yao kweli? Yaani uende nchi maskini akati utajiri unaokatika ardhi yako? Wajipamabanue waachane na kifaransa waongee kiswahili wapunguze starehe ile nchi ni tajiri dunia nzima. Waangalie ni namna gani utawanufaisha wanahitaji akili na maarifa na uzalendo wala si pesa
 
Back
Top Bottom