Hiyo habari ya MONUSCO hapana Kwa sababu wamekuwepo hapo hakuna Cha maana wamefanya.
Swala.la.kuweka wanajeshi wa kulinda kinachoitwa amani ila hawawezi kwenda msituni kuwafurusha waasi Haina maana.
Rwanda inadai hao wa Tutsi wa huko Mashariki mwa DRC sio raia wake ila wanalazimishwa kuwa WanyaRwanda so inajihami Kwa kuhakikisha vita havivuki Rwanda.
Kwa staili hii kuna siku Nchi Mpya itapatikana hapo na ndio utakuwa Mwanzo wa DRC yote kusambaratika.
Sioni Nchi tofauti na Tanzania ya kusaidia.
Binafsi napendelea DRC ikubali kupata usaidizi wa Nchi za Kigeni Kwa makubaliano ya malipo ya Rasilimali maana hawana hela ila tuu Waasi wafurushwe wote Hadi kuweka na usalama wa kutosha na Jeshi lao liwe na uwezo wa kudhibiti Kila kitu.