Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Status
Not open for further replies.
Haya ni mambo ya NGOSWE bora aachiwe ,nikianza kupima naona hapa kuna tactic flani inataka kutumika au inataka kutumiwa na Serikali ya Muungwana ,ni lipi hilo ,ok nitawachoma kidogo ili muamke.
Unajua serikali iliyopo madarakani imekwama na ina matatizo ambayo si madogo yanayoweza kusababisha kuanguka kifudifudi,hivyo imetafuta mbinu za kupindisha mawazo ya WaTanzania na kuyaelekeza Comoro kwa nguvu zote ,faida itakayopatikana hapa ni kuifunika hoja za ufisadi na uwizi huku wakiijadili mbio mbio tena chini chini na kuimaliza kinyemela nyemela wakati waTz wameshugulika na vita ,mapambano ndio yameanza akili za watZ zimeanza kuhamia Comoro kidogo kidogo na karibu zitashika kasi.
Uamuzi ni wenu tukirudi hali itakuwaje au mambo yashamalizika na kufungwa.
 
we are fighting a proxy war in comoro period. na yatatufikia yale yaliyowafikia wahabeshi hapo somalia.
 
......Comoro ina laana!!! Ku-solve issue za Comoro lazima mfaransa ausishwe, je hilo limefanyika?? kama la, basi ndugu zangu hili ni balaa!! thanx god, sina ndugu wala jamaa jeshini.
 
excuse me sire, excuse me sire! why the Minister of Foreign Affairs anazungumzia masuala ya operesheni za kijeshi na siyo mkuu wa Jeshi au Waziri wa Ulinzi...?
 
Quick question, majeshi yetu yameenda kule lini...? Kwa sababu nina taarifa zinazokinzana.
 
Quick question, majeshi yetu yameenda kule lini...? Kwa sababu nina taarifa zinazokinzana.

Kuna habariinasema majeshi yataanza uvamizi leo ama kesho .Tena si kulinda amani kama alivyosema Membe .Sasa hawa wamekufa kwa hali ya hewa ama kitu gani kimewaua ?
 
Kuna habariinasema majeshi yataanza uvamizi leo ama kesho .Tena si kulinda amani kama alivyosema Membe .Sasa hawa wamekufa kwa hali ya hewa ama kitu gani kimewaua ?

Swali zuri sana, ila serikali yetu haijawa wazi na wananchi unless ni operation ya siri. Wataalamu wa kijeshi mko wapi?
 
Ni kweli uvamizi utafanyika ila majeshi yetu hayatahusika kwenye uvamizi. Sisi tutahusika kwenye kulinda amani baada ya uvamizi kwisha. Mimi nimekuwa nikifuatilia swala hili kwa kina na ningependa kuwahujlisha kuwa hakuna aliyekufa ninavyojua mimi. Ofcourse siwezi kuweka vielelezo kuwa hakuna maiti.
 
Swali zuri sana, ila serikali yetu haijawa wazi na wananchi unless ni operation ya siri. Wataalamu wa kijeshi mko wapi?

serikali hii haiko wazi katika mambo mengi sana so hili nalo bila JF lilikuwa linaishia under the rug na kupewa bonge la spin.
 
Ni kweli uvamizi utafanyika ila majeshi yetu hayatahusika kwenye uvamizi. Sisi tutahusika kwenye kulinda amani baada ya uvamizi kwisha. Mimi nimekuwa nikifuatilia swala hili kwa kina na ningependa kuwahujlisha kuwa hakuna aliyekufa ninavyojua mimi. Ofcourse siwezi kuweka vielelezo kuwa hakuna maiti.

Whistling...........
 
excuse me sire, excuse me sire! why the Minister of Foreign Affairs anazungumzia masuala ya operesheni za kijeshi na siyo mkuu wa Jeshi au Waziri wa Ulinzi...?

"The African Union on Wednesday agreed to provide military and logistical aid to Sambi if necessary Tanzanian Foreign Minister Bernard Kamillius Membe said after talks in Addis Ababa.

Membe had co-chaired a session of the pan-African body's contact group on the Union of Comoros, with the commissioner of the AU Peace and Security Council"

Hii Ilikuwa baada ya mkutano wa AU early this year.
 
hilo sina tatizo nilikuwa na maana ya Operesheni yenyewe.. tangia wiki iliyopita ni membe anayezungumzia suala hili la Kijeshi..
 
Kwa taarifa zenu, kulingana na siasa za Mwalimu, Comoro ni koloni letu na viongozi wake walichaguliwa kama alivyofanya kwa Uganda enzi za kina Bina Issa, Obotte.
Ofisi nyingi za Comoro zinaendeshwa na Watanzania hasa ktk Ulinzi na hapa kwetu Wa Comoro wamejaa tele tena baadhi ni viongozi waheshimiwa wetu sawa na Myahudi Marekani. Sasa kama mtaweza tenganisha Myahudi na Marekani basi hata hili latazekana..
 
Swali zuri sana, ila serikali yetu haijawa wazi na wananchi unless ni operation ya siri. Wataalamu wa kijeshi mko wapi?

Majeshi yameanza kwenda last year kulinda amani wakati mjadala kati ya serikali na waasi unaendelea. Kwanza walienda 100. Baadaye wakawa wanaongezwa. Hizi habari zimetangazwa sana na haikuwa siri. Hadi wiki mbili zilizopita,mjadala umekuwa na umri wa miezi 8 na hakuna maendeleo, na Rais wa Comoro akaomba AU ivamie kisiwa kile na kumkamata jamaa, au la basi jeshi lake ingawa dogo lakini itabidi livamie.

Tanzania na South Afrika zimekuwa zikishughu;ikia suala la Comoro kwa muda mrefu sasa. Lakini nchi za Libya, Senegal Sudan na Tanzania ndo zimekubali wito wa AU kupeleka vikosi kwa ajili ya kumvamia Bacar. Jumla wanaweza kuwa 1900, na Tz imetoa kwenye 700 hivi, na kuifanya ndo kiongozi wa operesheni.

Hivyo basi, mejeshi yetu yamekwenda kule chini ya mandate ya AU, licha ya ukweli kuwa Rais wetu pia ni mwenyekiti wa AU. Vile vile, tuna uhusiano wa damu na Comoro, kwani watu wetu wengi hapa wametokea kule na vice versa, kitu kinachotufanya tuhitaji kuwasaidia.

Kama kweli kuna watu wamekufa, basi hizo ni hatari zinazohusishwa na mapigano. Kuna mwanajeshi ambaye hajui kuwa anaweza kufa vitani? wao wanaelewa vuziri zaidi dhana ya kufa wakati wowote. Kama tunafikiri hili ni jambo baya (kumsaidia jirani) basi ubaya wake tusiuone sasa, ilibidi tuuone wakati vikosi vinapelekwa. Vikosi vya kwanza vilikwenda kule miezi nane iliyopita.
 
Watanzania kwanza punguzeni woga! sasa hao maaskari wengine wa nchi zingine wanaokufa ktk mapambano je sii watu?

Ushupavu ktk jeshi ni kipimo cha uzalendo wetu!

Aluta Continua!
 
Watanzania kwanza punguzeni woga! sasa hao maaskari wengine wa nchi zingine wanaokufa ktk mapambano je sii watu?

Ushupavu ktk jeshi ni kipimo cha uzalendo wetu!

Aluta Continua!
Ndio watanzania ni waoga tena sana(mfano kuwaogopa Mafisadi) lakini saa nyingine wana haki ya kuuliza
Haiwezekani eti kwa sababu wanajeshi wa marekani wanakufa kila siku Iraq, basi hii iwe sawa na kwa wanajeshi wa Tanzania
Swala hapa sio kufa, ila wanakufa kwa sababu zipi haswa ambazo ni za kitaifa?
Ndo tunataka kujua hapa
 
excuse me sire, excuse me sire! why the Minister of Foreign Affairs anazungumzia masuala ya operesheni za kijeshi na siyo mkuu wa Jeshi au Waziri wa Ulinzi...?

Mkuu, ukisikiliza sana mambo ya Membe, utagundua kuwa ni mambo ya kisera na ushusiano katika bara hili, shughuli anayoifanya kama Foreign Minister. Kwenye mikutano hii na maamuzi mengine CDF anahudhuria (nadhani na waziri wa ulinzi pia, sina hakika).
Hapo ndiyo wizara hizi zinakuja kuungana paoja katika kutekeleza kazi moja, huku kila moja ikiwa na kona yake.

Kuna mambo Membe amesema wazi kuwa hawezi kuyaongelea kwa kuwa ni ya defence minister au CDF, mfano mambo yote ya kiutendaji kivita.
 
......Comoro ina laana!!! Ku-solve issue za Comoro lazima mfaransa ausishwe, je hilo limefanyika?? kama la, basi ndugu zangu hili ni balaa!! thanx god, sina ndugu wala jamaa jeshini.

France imehusishwa, na imepiga dole tu kwa kusaidia logistisc. Imeshatoa ndege kwa ajili ya kusafirisha askari. Don't worry, be happy.

Tanzania ni nchi yako, wote ni nduguzo, acha kujitenga, ndo maana umemshukuru god na siyo God! (Lol...!)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom