Baada ya kusoma na kufuatilia kwa makini baadhi ya maoni ya wanachma wenzangu, mimi nikaamua kufanza utafiti wa jambo hili na labda kutaka kuchambua zaidi kwanini majeshi ya AU yamepelekwa kisiwani humo.
Tangu kupata uhuru kisiwa hicho kimekoswakoswa na majaribio 19 ya kupindua serikali iliopo madarakani, huku ikiwa inaaminika kwamba kiongozi wa maghaidi bwana Fazul Abdullah Mohamed ni mzwaliwa wa kisiwani humo.
Katika duru za ujasusi inaaaminika kwamba bwana Mohamed ndie alikuwa kiranja mkuu wa mipango ya kulipua mabomu balozi za Marekani mjini Dar-es-Salaam nchini Tanzania na Nairobi nchini Kenya mwaka 1998. Mashambulizi hayo yaliua watu 224 na kikundi cha Al-Qaeda ambacho kilichoongozwa na Mohamed na ambacho kilikuwa na makao yake makuu nchini Somalia.
Lakini mara ghafla siku ya Jumanne tarehe 18 March, majeshi ya AU yaliyojumuisha kutoka Sudan, Libya,Senegal na Tanzania, yalivamia kisiwa cha Anjouan,na kuanza kusaidia vikosi va majeshi ya Comoro.
Lakini hatua hii inaleta maswali mengi sana.
1. Iweje majeshi hayo yote yavamie kisiwa hicho chenye watu si zaidi ya 240,000 ilhali njia ya kidiplomasia na vikwazo vingeendelea kutumika kama ambavo Afrika Kusini imekuwa ikishauri?
2.Ingawa operesheni hio ni fupi, lakini inaashiria kuleta gharama za uendeshaji likiwemo suala la watu kukimbia nyumba zao,na pia gharama za kujenga upya baadhi ya miundo mbinu au makazi ya watu ambayo yamebomolewa, je ni nani atagharamia hilo kati ya Umoja wa Afrika na Serikali ya Comoro?
3. Huku ikiwa inakabiliwa na majukumu mengine ya kusimamia amani huko Darfur na maeneo mengine yanye migogoro barani Afrika, je kwa sasa ni vema kujishughulisha na kusimamia amani kwa njia ya vita? badala ya kutumia njia ya mezani ambapo gharama za kupeleka majeshi katika maeneo yenye vurugu na migogoro zinakuwa kubwa na ni nani anawapa fwedha AU kuzichezea hivo?
Naomba kutoa hoja.