KERO Maji hayatoki Kimara karibu mwezi sasa. DAWASA shida nini?

KERO Maji hayatoki Kimara karibu mwezi sasa. DAWASA shida nini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
1,470
Reaction score
515
Hali ya maji katika eneo linalohudumiwa na kituo cha Kimara ni mbaya Sana.

Maji hayatoki katika baadhi ya maeneo karibu mwezi sasa.

Hakuna taarifa yeyote inayotolewa.

Viongozi wetu wa juu nao kwasasa naona kimya kabisa, zile amsha amsha hazipo.

Basi mtupe hata taarifa tatizo ni nini na maji yatarudi lini. Kipindi cha likizo, watoto wapo majumbani, mvua zimeanza kunyesha lazima tunakaribisha vipindupindu sasa.

Jamani huku mkwajuni, king'ongo, Kwa Mogela shida ni nini?
 
Sijui mikoani nako kuna kero za Maji hivi? Ila Dar sahivi hali imekua mbaya sana.
 
Watu WA kimara ombeni mhamishiwe mkoa WA pwani TU, dar imeshindwa kuwahudumia
 
Back
Top Bottom