Maji Ilemela Mwanza ni saa 24, miradi mikubwa ya maji yajengwa na kukamilika

Maji Ilemela Mwanza ni saa 24, miradi mikubwa ya maji yajengwa na kukamilika

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
166
Reaction score
182
Serikali imejenga miradi mikubwa ya maji safi na salama katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanikiwa kumaliza tatizo la ukosefu wa maji wilayani humo.

Miradi hiyo imejengwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula ambaye kwa sasa ameingia tena katika kinyang'anyiro cha kutetea nafasi hiyo.

Mbunge huyo ndani ya miaka mitano ameweza kuisimamia serikali ipasavyo na kufanikiwa kujenga miradi hiyo ya maji pamoja na miradi mingine.

Pia kazi hiyo ya ujenzi wa miradi ya maji imefanywa chini ya usimamizi makini wa Rais DK. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji safi.

Serikali ya awamu ya tano wakati inaingia madarakani mwaka 2015 ilijiwekea lengo la kuwatua ndoo akina mama na sasa imeweza kutekeleza ahadi hiyo kwa asilimia 95.

Miradi hiyo ya maji iliyokamilika katika wilaya ya Ilemela imejengwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo.

Maeneo ilipojengwa miradi hiyo na kukamilika ni pamoja na Kitangiri, Ibanda ambako tenki lenye lita laki tano limekamilika.

Pia serikali chini ya usimamizi wa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mwauwasa imesimamia ujenzi wa tenki eneo la Nyasaka lenye ujazo wa lita milioni 1.2.

Katika eneo la mji mwema nako limejengwa tenki kubwa litakalo sambaza maji kwa wakazi wa maeneo hayo likiwa na ujazo wa lita milioni 1.2.

Pia Serikali imejenga na kukamilisha ujenzi wa tenki la maji katika eneo la Nyamhongoro lenye ujazo wa lita laki tano litakalosambaza maji mpaka Kisesa wilayani Magu.

Kubwa kuliko, ni ujenzi wa tenki al Busweru jirani kabisa na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo ambalo lina ujazo wa lita milioni tatu na muda wowote kuanzia sasa litakamilika.

Miradi hiyo yote imegharimu zaidi ya bilioni 50 ambazo zimetolewa na Serikali kuu na wahisani wengine was maendeleo.

Miradi hiyo iliyotekelezwa na Serikali ndani ya Manispaa hiyo ikiwemo ya miundombinu ya barabara, usafirishaji wa majini, elimu ambayo imetolewa bure, afya, vituo vya afya vimejengwa na hospitali ya wilaya ambayo ipo hatua za mwisho kukamilika.

Kutokana na Serikali ya chama cha mapinduzi kufanya mambo makubwa ndani ya wilaya hiyo, wana Ilemela wana deni.

Wana Ilemela deni lenu kwenu ni kuwachagua kwa kuwapigia kura za ndiyo mbunge wa sasa aliyemaliza muda wake Angelina Mabula na Rais DK. John Magufuli ili waweze kuendelea kuwatumikia.

NB: Taarifa zinazosambazwa mitandaoni ilemela kuna ukosefu wa maji ni uzushi na zipuuzwe zinaletwa na watu wasiolitakia mema jimbo la Ilemela na watu hao wapuuzwe.
 
Wewe unakaa ilemela hipi ? Nyasaka, nsumba,ppf,busweru,lumala, kiseke,nsumba, nyamngoro na n.k, leo wiki ya pili maji yanakuja saa sita usiku na ikifika saa kumi na mbili asubuhi yamekatika. Uwe mkweli

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Mimi naishi Mwanza, namshangaa mtoa mada, labda anaongelea Capri point huko, asidhani sisi ni wajinga!
 
Ww ni muongo sana acha kufanya watu ni wajinga, maji bado ni tatizo kubwa sana wakati mwingine hapa kiseke ya ppf unaweza kukaa hadi siku 2 hakuna maji, Kuna siku tukawauliza watu wa idara ya maji kwann hatupati maji, akajibu wao mamlaka ya maji siyo reserve tank ya kuhifadhia maji watu kwa hiyo kila mtu anunue matank makubwa ya kuhifadhia maji, anashindwa kujua kwamba tank kubwa bei yake ni hadi milioni moja je watu wote wanamudu hiyo cost? Sisi wananchi tunaozunguka ziwa Victoria reserve tank yetu ni Ziwa jenyewe kinachotakiwa ni mamlaka ya maji kutupa maji na sisi wajibu wetu ni kulipa bills za maji basi
Halafu manispaa ya ilemela ndiyo ina miundo mbinu mibovu kabisa ya barabara kuliko manispaa zote nchini. Fanyeni kazi acheni siasa nyepesi miaka inavyoenda ufahamu wa wananchi unaongezeka
 
Unapafahamu alipojenga nyumba Angelina, buswelu majirani wake wote wanasema hawatoweza kumpigia kura maana walimuuliza kwenye mkutano wake kuhusu maji akashindwa kuwapa majibu mazuri na ndio sehemu mwaka 2015 alipata kura nyingi uko ila safari hii watu wa buswelu hawamtaki ata kumsikia
 
Nilikua Igoma last week nimekuta hawana maji week ya tatu na Igoma iko Ilemela, sasa hiyo mitambo mipya inahudumu Ilemela ipi?

Igoma ipo Nyamagana, ila Kuna mradi upo Lwanhima ambao nako tenki la maji linaendelea kujengwa lenye ujazo wa lita milioni mbili ambalo litasambaza maji mpaka igoma yote na kisesa
 
Kila siku napishana na ratiba ya maji hapa nyasaka. Yanakuja nikiwa nimelala na yanakatika nikiwa bado nimelala. Nikienda kibaruani ndo yanakuja, nikirudi yamekata
 
Back
Top Bottom