Maji kutoka kwenye bomba la kutolea moshi

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Habari wadau. Kila siku asubuhi nikiwaasha gari kunatoka maji kwenye bomba la kutolea moshi. Wengine wanasema ni ubora wa engine, wengine wanasema engine ina matatizo. Ukweli ni upi? Iwe ubora au matatizo ya engine, nikiufikiria mfumo wa engine yenyewe, maji hayo yanapatikanaje huko? Naomba msaada.
 
Maji mengi au ule mvuke? Hata mimi huwa yanatoka mvuke tena asubuhi kwani nilipo pana baridi. Nilimuuliza fundi, akasema sio tatizo.
Siyo maji mengi ila ni matone matone huwa yanadondoka wakati gari iko silent mode. Kama ni upya wa gari maji au mvuke huo unatokana na nini au unatengenezwa wapi kwenye mfumo mzima wa engine?
 
Maji hayatakiwa kutoka kwenye exhaust pipe. Ukiona hivyo fahamu kuna leakage kwenye mfumo wa maji....kuna gaskets zimeharibika au kuna tatizo mahali . Maji yanapenya kwenda kwenye exhaust system kupitia kwenye Ebgine block sejhemi...ipo shida mahali...mostly gaskets.
 
Mambo vp mkuu usiwe na hofu na hiyo si shida kabisa. Ushawahi kujiuliza kazi ya masega au catalyst converter? Ukipitia kwenye nyuzi zangu kazi yake ni kubadili hewa chafu ambazo zinatolewa kutokana na mlipuko wa kwenye engine na kubadili kuwa maji na carbon kama sikosei unaweza ku google importance of catalyst converter sasa hayo maji ndo ambayo unayaona kwenye exhayst pipe hasa wakati wa asubuhi. Karibu
 
Maji hayatakiwa kutoka kwenye exhaust pipe. Ukiona hivyo fahamu kuna leakage kwenye mfumo wa maji....kuna gaskets zimeharibika au kuna tatizo mahali . Maji yanapenya kwenda kwenye exhaust system kupitia kwenye Ebgine block sejhemi...ipo shida mahali...mostly gaskets.
Mkuu effect ya hiki kitu haihusiani na maji kutoka kwnye exhaust
 
Kama vipi jipige ngumi kifuani. Maana injini ya hiyo gari yako bado iko kwenye ubora wake.

Lakini pia nichukue nafasi hii ya kipekee kukupongeza kwa kununua usafiri. Hatimaye na wewe umeanza kutembea huku ukiwa umekaa.
Nashukuru mkuu umenishushia presha, maana kuna mmoja humu kaniambia eti kuna shida ya gasket hivyo kuna leakage ya maji yanaingia kwenye mfumo wa engine. Nilianza kulowa jasho. Lakini wewe umenisaidia, na inabidi nikuamini tu. Aidha, nakushukuru kwa kunipongeza. Ahsante sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Maji yapo kwenye closed circulation....radiator-wwterpump-Engine block/oil cooler-Radiator.
Ukiona maji yanatoka kwenye Muffler lazima kuna tatizo.
 
Gari yako inatoa Maji kwenye Exhaust, Usipuuzie hali hiiWatu wengi sana wamekua wakijiuliza kitendo cha Gari kutoa maji kwenye Exhaust ina sababishwa na nini, na je ni tatizo katika gari yangu au ni kitu cha kutokuhofia. sasa soma nakala hii leo niweze kukujuza.guides11. Mar 2023 213 views
Gari yako inatoa Maji kwenye Exhaust, Usipuuzie hali hii
Katika hali ya kawaida, sio rahisi kuona maji yanayotoka kwenye mfumo wa Exhaust wa gari. Lakini ukigundua kuwa bomba lako la nyuma linavuja au linadondosha maji kutoka humo, basi ina maana kwamba mfumo wako wa kutolea moshi lazima uwe na maji ndani yake.Hii sio sababu ya kuwa na wasiwasi sana kwa sababu kwa kawaida hali hii sio jambo kubwa. Hata hivyo, imekuwa ni jambo zuri kufanya uchunguzi wa hali hii na ukatenga muda kusoma nakala hii. Vinginevyo, inaweza kuunda matokeo mabaya zaidi ambayo yatakugharimu pesa nyingi kama usipojua tatizo nini.zifuatazo ni baadhi ya sababu Kwanini Gari hutoa Maji kwenye Exhaust.Kwanini Gari yangu inatoa maji kwenye Exhaust1. Injini yako inafanya kazi vizurimoja ya viashiria kua injini yako ipo vizuri hasa katika utendaji wake wa kazi ni kuona maji yanatoka kwenye Exhaust ingawa sio magari yote yanayotoa maji basi inaashiria hivi lakini magari mengi. Injini yako inapo unguza mafuta iwe petrol au diesel kinachofuata kama matokeo ni Gas aina ya Kaboni dioksidi na maji. hii pia husaidia kupunguza kiwango cha hewa chafu kitakachotelewa na gari yako.Pia sababu nyingine ya Gari kutoa maji kwenye Exhaust, kama unaishi kwenye maeneo yenye baridi kama Iringa, mbeya arusha na singida basi vitu kama hivi ni rahisi kuona kwani injini yako inapopata joto ile hewa ya baridi inayo ingia kwenye Exhaust. Kwa sababu hii, mvuke wa maji hutolewa wakati joto linapounganishwa na hewa baridi. Kisha utaona matone madogo ya maji yakianguka kutoka kwenye bomba la nyuma pamoja na kile kinachoonekana kuwa moshi mweupe. hata hivyo hali hii hutoweka baada ya muda mchache tu.2. Piston yako ni mbovusababu nyingine ambayo husababisha maji kutoka kwenye mfumo wa kutolea hewa chafu yani Exhaust ni ubovu wa piston ya gari yako. lakini hii hua ina viashiria vyake kutambua kwamba kuna kitu hakipo sawa utaona vitu vifuatavyo.Exhaust yako inatoa maji pamoja na moshi muda huo, ikiambatana na harufu isiyo ya kawaida, na maranyingi harufu hii hua ni nzuri na yenye kuvutia.utakapo ona hali hii haraka sana usiendeshe gari yako na muite fundi wa mechanic aje akague piston yako kuthibitisha uwepo wa tatizo hilo.
 
Attachments

  • 21.png
    21.png
    129.5 KB · Views: 20
Habari wadau. Kila siku asubuhi nikiwaasha gari kunatoka maji kwenye bomba la kutolea moshi. Wengine wanasema ni ubora wa engine, wengine wanasema engine ina matatizo. Ukweli ni upi? Iwe ubora au matatizo ya engine, nikiufikiria mfumo wa engine yenyewe, maji hayo yanapatikanaje huko? Naomba msaada.
Kama inadondosha matone hiyo ni kawaida tu, ila kama ni kinyume cha hapo na inafanya hivyo muda wote hayo ni majanga.
 
Siyo maji mengi ila ni matone matone huwa yanadondoka wakati gari iko silent mode. Kama ni upya wa gari maji au mvuke huo unatokana na nini au unatengenezwa wapi kwenye mfumo mzima wa engine?
Hiyo ni condensation tu kwenye exhaust ndio maana inatokea tu kwenye cold start ila ukiendesha gari nayo inapotea.

Wala siyo tatizo
 
Maji hayatakiwa kutoka kwenye exhaust pipe. Ukiona hivyo fahamu kuna leakage kwenye mfumo wa maji....kuna gaskets zimeharibika au kuna tatizo mahali . Maji yanapenya kwenda kwenye exhaust system kupitia kwenye Ebgine block sejhemi...ipo shida mahali...mostly gaskets.
Tofautisha kati ya maji na mvuke. . . .
 
Kama vipi jipige ngumi kifuani. Maana injini ya hiyo gari yako bado iko kwenye ubora wake.

Lakini pia nichukue nafasi hii ya kipekee kukupongeza kwa kununua usafiri. Hatimaye na wewe umeanza kutembea huku ukiwa umekaa.
Wala hata siyo ubora wa engine mkuu, hata engine mbovu inaweza kufanya hivyo. . . .
 
Gari yako inatoa Maji kwenye Exhaust, Usipuuzie hali hiiWatu wengi sana wamekua wakijiuliza kitendo cha Gari kutoa maji kwenye Exhaust ina sababishwa na nini, na je ni tatizo katika gari yangu au ni kitu cha kutokuhofia. sasa soma nakala hii leo niweze kukujuza.guides11. Mar 2023 213 views
Gari yako inatoa Maji kwenye Exhaust, Usipuuzie hali hii
Katika hali ya kawaida, sio rahisi kuona maji yanayotoka kwenye mfumo wa Exhaust wa gari. Lakini ukigundua kuwa bomba lako la nyuma linavuja au linadondosha maji kutoka humo, basi ina maana kwamba mfumo wako wa kutolea moshi lazima uwe na maji ndani yake.Hii sio sababu ya kuwa na wasiwasi sana kwa sababu kwa kawaida hali hii sio jambo kubwa. Hata hivyo, imekuwa ni jambo zuri kufanya uchunguzi wa hali hii na ukatenga muda kusoma nakala hii. Vinginevyo, inaweza kuunda matokeo mabaya zaidi ambayo yatakugharimu pesa nyingi kama usipojua tatizo nini.zifuatazo ni baadhi ya sababu Kwanini Gari hutoa Maji kwenye Exhaust.Kwanini Gari yangu inatoa maji kwenye Exhaust1. Injini yako inafanya kazi vizurimoja ya viashiria kua injini yako ipo vizuri hasa katika utendaji wake wa kazi ni kuona maji yanatoka kwenye Exhaust ingawa sio magari yote yanayotoa maji basi inaashiria hivi lakini magari mengi. Injini yako inapo unguza mafuta iwe petrol au diesel kinachofuata kama matokeo ni Gas aina ya Kaboni dioksidi na maji. hii pia husaidia kupunguza kiwango cha hewa chafu kitakachotelewa na gari yako.Pia sababu nyingine ya Gari kutoa maji kwenye Exhaust, kama unaishi kwenye maeneo yenye baridi kama Iringa, mbeya arusha na singida basi vitu kama hivi ni rahisi kuona kwani injini yako inapopata joto ile hewa ya baridi inayo ingia kwenye Exhaust. Kwa sababu hii, mvuke wa maji hutolewa wakati joto linapounganishwa na hewa baridi. Kisha utaona matone madogo ya maji yakianguka kutoka kwenye bomba la nyuma pamoja na kile kinachoonekana kuwa moshi mweupe. hata hivyo hali hii hutoweka baada ya muda mchache tu.2. Piston yako ni mbovusababu nyingine ambayo husababisha maji kutoka kwenye mfumo wa kutolea hewa chafu yani Exhaust ni ubovu wa piston ya gari yako. lakini hii hua ina viashiria vyake kutambua kwamba kuna kitu hakipo sawa utaona vitu vifuatavyo.Exhaust yako inatoa maji pamoja na moshi muda huo, ikiambatana na harufu isiyo ya kawaida, na maranyingi harufu hii hua ni nzuri na yenye kuvutia.utakapo ona hali hii haraka sana usiendeshe gari yako na muite fundi wa mechanic aje akague piston yako kuthibitisha uwepo wa tatizo hilo.
Acheni kumtisha mwenzenu
 
Tena ushukuru engine yako inachoma vizur hiyo n physics tu acha wasi wasi ingekuwa n piston haichomi vizur ungenyooka mapema sana gerej
 
Maji yapo kwenye closed circulation....radiator-wwterpump-Engine block/oil cooler-Radiator.
Ukiona maji yanatoka kwenye Muffler lazima kuna tatizo.
Umeshawahi kumiliki mchuma mpya au w
 
Maji yanayotoka huwa yabaridi kweli....Sidhani kama ni leakage kutoka kwenye engine
 
Back
Top Bottom