KERO Maji machafu toka machinjio ya Vingunguti

KERO Maji machafu toka machinjio ya Vingunguti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Natumaini n mzima wa afya , wananchi wa wilaya ya ilala kata ya vingunguti tuna kero ambayo inaenda miaka miwili na nusu sasa ya maji machafu ambayo yanakuja mitaani kutoka kwenye mabucha mapya ya Vingunguti na kuwa kero kubwa kwa wananchi.

Tumejaribu kufuatilia pamoja na kuwasiliana na viongozi wetu lkn jitihada zetu zmeshindikana. Tunaomba msaada wako ikiwezekana ifike kwa NEMC ili itusaidie maana watoto wadogo wanachezea lkn pia sio salama kiafya.

Mazalia ya mbu yameongezeka mtaani homa za matumbo. Kwa kweli Hali sio nzuri na ukizingatia miundombinu ya maji ya kunywa DAWASA imepita sehemu ambazo maji hayo machafu ambayo yamechanganyika na kemikali lkn pia kuna wakati mpaka huwa yanachanganyika na damu yanapita.

Hali ni ngumu na changamoto mno. Kiafya watoto wanachubuka miguu. Hali sio nzuri kabisa.

Tunaomba msaada ili tuondokane na changamoto hii inayotusumbua kwa muda mrefu. Sasa inaenda miaka miwili na nusu bila ufumbuzi wowote na ilihali maji yanapotoka panajulikana.

BeautyPlus_20240524135458132_save.jpg
BeautyPlus_20240524135450331_save.jpg
BeautyPlus_20240524135444520_save.jpg
BeautyPlus_20240524135439361_save.jpg
BeautyPlus_20240524135411696_save.jpg


 
Back
Top Bottom