SoC02 Maji: Ushiriki wa jamii, uendeshaji na uibuaji wa miradi ya maji, utoaji taarifa na changamoto za utendaji na utatuzi

SoC02 Maji: Ushiriki wa jamii, uendeshaji na uibuaji wa miradi ya maji, utoaji taarifa na changamoto za utendaji na utatuzi

Stories of Change - 2022 Competition

CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2017
Posts
2,031
Reaction score
1,514
Utangulizi.

Tangu uwepo wa ulimwengu huu maji ni kimiminika ambacho kimekuwepo na kusaidia shughuli mbalimbali za uendeshaji na ujenzi wa ulimwengu tangu ikiwa tupu hadi sasa katika zama za sayansi na teknolojia iliyokubuhu (Post-science and technology society).Maji hayana mbadala,na wengine waliofikiri zaidi walisema maji ni uhai.

Tangu nchi ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ijitwalie uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa mwisho ambaye alikuwa muangalizi wetu kabla ya uhuru mnamo mwaka 1961 kumekuwepo na jitihada nyingi za kuhakikisha kuwa huduma hii ya maji inawafikia wananchi wote wa mijini na vijijini.

Kumekuwepo sera mbalimbali za maji tangu uhuru,hususani sera ya maji ya mwaka 1991 iliyokuwa na malengo kuwa ifikapo mwaka 2000 kila mwananchi awe amepata maji safi na salama lakini ni dhahiri imeshindikana kutokana na jamii kutokushirikishwa(WAVUTI YA WIZARA YA MAJI)

TAFSIRI YA MANENO DHAHIRI KATIKA MADA.

Maji:Ni kimiminika amabacho ni kiini cha uhai wowote duniani na utamaduni wa mwanadamu sababu ni asilimia 71.11 ya sehemu ya ulimwengu (wikiwand.com)

Jumuiya za wtumiaji wa maji :
Ni vyombo vinavyoundwa katika ngazi ya jamii kwa dhumuni la kuendesha na kughaaramia miradi ya maji katika ngzi ya chini kabisa ya jamii.jumuiya hizi hapo kabla zilikuwa chini ya halmashauri pamoja na wahandisi wa wilaya au mikoa.kutokana na mabadiliko ya sheria namba tano ya mwaka 2019 kifungu nzmba 32 jumuiya za watumia maji hutambulika.

Jumuiya za watumiaji maji zimefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa kwani zimepelekea uendelevu wa miradi ya maji ambapo haikuwa hivyo hapo awali.

Jumuiya za watumiaji maji zimehuishwa kutoka kamati na vyombo vya watumiaji maji ngazi ya jamii na kuwa jumuiya za watumiaji maji zikiwa chini ya wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA).

USHIRIKI WA JAMII (UIBUAJI MIRADI).

Kwa
hakika na dhahiri jamii imekuwa na ushiriki mdogo kabisa wa uibuaji miradi na kupewa kipaumbele katika katika maoni yao ya vyanzo vya maji vya kihistoria.Jambo hili ni baya sana kwa ukuaji na uendelevu wa miradi ya maji inayojengwa.

Hii inajidhihirisha pale ambapo kuna maeneo amabayo hipimwa kitaalamu (pump test) na wataalamu hujiridhisha na kuamua kuchimba kwa madai kuwa ni matokeo ya kitaalamu hivyo kupuuza maoni ya wananchi kuhusu vyanzxo vya uhakika vya maji vya kihistoria,kutokana na hali maji hukosekana au kupungua ndani ya muda mfupi tangu kuchimbwa kwa visima hivyo jambo linalopelekea kufifisha jitihada za kuwaondolea mzigo wananchi juu ya kero ya maji.

Ukitembelea mikoa ya kusini katika vyanzo vya maji vya kata ya chilaile,kiparamnero,Ngangambo vyanzo vyake vya maji vimekuwa na changamoto kubwa kutokana na kutokuwepo kwa maji ya kutosha ukilinganisha na vyanzo vya maji vya kihistoria.

Kama wataalamu wa maji kupitia taasisi zao wataamua kuishirikisha jamii kabla ya uanzishaji wa miradi inawezekana kukawepo uendelevu wa miradi ya kwa muda mrefu.

Ukitembea kote nchini utashuhudia upotevu mkubwa wa fedha za serikali kutokana na miradi ya maji kutokuwa na usanifu unaotazama mbali zaidi ya miaka hamsini ijayo.Hasara itokanayo na kushindwa kuishirikisha jamii ni kupelekea mamia kwa mamia ya miradi kupoteza ufanisi ndani ya muda mfupi sana,hivyo kufanya jamii ileile iliyopewa mradi wa maelfu ya fedha kuanza kudai mradi mwingine ndani ya miaka kadhaa kutokana na labda ongezeko la watu au upungufu wa maji.

Ili kuweza kuiendesha miradi ya maji ni muhimu kuwepo kwa mita za kisasa au kuweza kuipa kipaumbele teknolojia mpya ya uuzaji wa maji itakayotokana na kufanana na pampu za kuuzia mafuta katika vituo mbalimbali vya kujazia mafuta.

Suala la teknolojia hiyo ni muhimu kwa sababu jamii ya kitanzania ni ngumu kuweza kujaza maji kwa ujazo bali hujaza maji kwa chombo husika kwa mfano,pale mnunuzi wa maji anapokwenda na dumu la lita ishirini mnunuzi hupenda kujaza dumu na si ujazo wa lita ishirini jambo ambalo dhahiri shughuli za maji zitapata hasara ukilinganisha na kama ikiwepo teknolojia inayoruhusu mtu kupata kutokana na anachokilipia.

Kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa kuwepo na mita za kisasa ambazo huruhusu maji pale unapolipia au kwa kimombo huitwa (pre-paid water meter) japo bado changamoto ya upotevu wa maji yanayomwagika ni mkubwa,hivyo suluhisho pekee katika hili ni kuwa na mfumo wa uuzaji maji vijijini kama ule wanaotumia katika vituo vya uuzaji wa mafuta.

1661365553833.png

Picha kwa hisani ya earthview.co.ke​
1661365477552.png

Picha kwa hisani ya stronsmart.com

Hii ni pampu ya maji ifananayo na pampu za kujazia mafuta ambapo hakuna hata tone moja la mafuta linalopotea.Hivyo pia ziwekwe ktk maji.
UTOAJI TAARIFA.

Miradi ya maji kwa ukaribu kabisa huwa chini ya jamii kwa sababu wao ndio huishi na kupakana na vyanzo vya maji hivyo kuwa rahisi kwao kuweza kutoa taarifa mbalimbali zikiwemo zakuharibika kwa vyanzo vya maji,kupasuka kwa mabomba au uharibifu wa namna ayeyote ile.

Taarifa hizo huenda pamoja na kushindwa kutatuliwa kwa wakati kutokana na uhaba wa wataalamu,raslimali fedha na hata kupuuzwa kwa taarifa hizo na wataalamu.

CHANGAMOTO ZA UENDESHAJI.

Kwanza kabisa ni kutokuwepo kwa uelewa wa viongozi juu ya masuala mbalimbali ikiwemo katiba za jumuiya za watumiaji maji,uingiliaji wa wanasiasa ktk shughuli za maji,ukosefu wa mapato hasa wakati wa mvua,kukosekana kwa wataalamu wa jamii ndani ya sekta ya maji.

Vilevile,kumekuwepo na changamoto ya uwasilishaji wa taarifa za mapato na matumizi na mihustasari mbalimbali ya vikao,na mapendekezo ktk hili ili kuleta mabadiliko ni kuhimiza mafunzo na kuhimiza matumizi ya teknolojia haswa barua pepe ili kuondoa gharama za usafiri na kuimarisha hali ya utunzaji wa kumbukumbu.

Naomba kuwasilisha.​
 
Upvote 0
Back
Top Bottom