Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Unaposema ni mwili kweli na damu kweli wakati tunaviona ni mkate na divai.Hapa ndipo wakatoliki napowaona hawana tofauti na mashabiki wengine wa kiimaani.
Ila utasikia padri kasoma miaka 3 filosofi alafu kasoma miaka 4 theology alafu kasomea digrii ya kawaida miaka 3.
Any way mtu ukimueleza mambo ya systematic theology na dogmatic theology na advantages na disadvantages zake hata haelewi.Yy anachokazania tu ni kasoma theology miaka 3.
 
No situmiii PM Kwa Sababu maalum. Tumia codes utaeleweka.
Kama ni kuona wakinitetea basi ...

Nimewahi kuona Kuhani Musa akinitetea ktk vita zangu zote ..

Pia namuona Kuhani Musa akiwa ktk mavazi meupe sana...

Na nimeona madhabahu ya Kuhani Musa ikiwa inajengwa hata kabla hajaanza kujenga...

Pia nimewahi kumuona Askofu wa Anglican Dar akinitetea..

Mwamposa naona tu akiwa anahubiri neno..
 
Kuhani Musa ana Yule msaidizi wake, kila kitu anajibu NDIYO!
 
Basi sawa kama umeona hivyo. Huyo kuhani sijamfuatilia,

Bt Bulldozer ni Agent wa kule chini.
 
Maji yetu Katoliki, tatizo linakuja pale Mtu anapoacha kumwabudu Mungu anabaki na Maria
Maria ni mwanadamu tu na baada ya kumzaa Yesu aliendelea na masiha kawaida na bwana ake.

Kuna mahali kanisa linakwama kwa kupunguza mafundisho ya imani kwa watoto, nashindwa kuelewa inakuwaje unajiita Mkatoliki na bado hauelewi ukuu wa Mama Bikira Maria katika historia ya Ukombozi, na jukumu alilokabidhiwa na Yesu Kristo pale msalabani na baada ya kufufuka kabla hajapaa.

Unashindwa hata kuelewa kwanini Mama Bikira Maria ndie Sanduku la agano lililoptea pale mlimani, likaja kuonekana kwa ishara mawinguni baada ya kupalizwa?

Bado huyo unamuita ni mwanadamu wa kawaida? Ungesema wewe si Mkatoliki kidogo ningekuelewa, japo kuwa Mkristo tu kunakufanya ufahamu vitu kama hivi.
 
Ngoja niendelee kuomba mpaka nimjue...

Nikijua lazima niseme ili watu wasipoteee..
Ok fuatilia,

Bt kumsema lazima uwe level yake, Nabii anasemwa na Nabii, Askofu Kwa Askofu nk nk.

Sababu kuu ni kulinda wafuasi wanaomwamini wasojua lolote. Pia hutumika BUSARA sababu anaweza kutubu na kurudi Kwa Mungu, na Mungu ni WA Rehema.

Pia, kuwasema manabii wa UONGO Waliowekeza ktk viwango vya juu ktk makafara ya damu uwe na misuli, maana mziki wake Si wa kitoto.
 
Asante mkuu...

Mungu atusaidie
 
Newton alijua Quantum Physics?

Unaeleea unafanya logical fallacy inaitwa "appeal to authority"?

Google that.
 
Mkuu, wewe unasemaje kuhusu utata huu? Vitu vilijitokeza vyenyewe tu bila kuwa na mwezeshaji? Kuna theory yoyote inayoelezea vitu kujizalisha pasipo chanzo? Na kama hakuna kitu kinachoweza kujizalisha chenyewe, basi utuambie chanzo chake ni nini?
Unaelewa kwamba hata kama vitu havikujitokeza vyenyewe tu, chanzo chake si lazima kiwe Mungu?

Yani hapo unachosema ni kama vile wewe Mmatumbi wa Kibiti, halafu unadai baba yako mzazi ni rais wa zamani wa Marekani George W. Bush, eti kwa sababu hujajizaa mwenyewe, lazima una baba.

Sasa, ikiwa lazima uwe na baba ndiyo baba yako lazima awe George W. Bush?

Pia unaelewa kwamba dhana nzima ya chanzo katika fizikia haiko rahisi kama unavyofikiria?

Unaelewa kuwa katika Quantum Causal Loop, chanzo kinaweza kuwa ni matokeo ya matokeo yake?

Yani ni hivi, unaweza kuwa na kitu 1, kilichosababisha kitu 2, halafu hapo hapo, hicho kitu 2 nacho kikawa ndicho chanzo kilichosababisha kitu 1?

Sasa hapo chanzo ni kipi? Kitu 1 au kitu 2?

Unaelewa hilo?
 
"Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu". Hii ndiyo iliyoandikwa pale SICHO ulichoandika
Biblia inatafsiri nyingi. Kwani unaelewa maana ya mashonde? Weka hata ya kingereza KJV na NIV kwenye biblia za kiswahili zimetumia maneno tofauti.

 
Hii inafanya kazi hata kwenye zile lucid beats,ukitaka kuingia ktk ulimwengu wa roho
 
Nimeisoma.Waisrael walifanya makosa mbele za MUNGU.Mungu akawaletea njaa kali,chakula hakuna,kiasi kwamba watu ilibidi wale mavi ya njiwa.Nayo yakawa dili hadi yakawa yanauzwa.Badala ya ngano Watu wakawa wananunua mavi ya njiwa wanatengeneza mikate wanakula.Sasa hii inaingilianaje na mikate inayotengezezwa kwa ngano!?Unieleze hapo sasa
 
Umepuyanga kabisa maji ya Mwamposa ni maji ya kawaida yanayouzwa dukani yeye mwenyewe kwenye TV anasema beba maji uliyokuja nayo niyaombee ,Kila nikiangalia TV sijawahi kusiki akiwalzimisha watu LAZIMA wanunue maji yanayouzwa dukani kwake shs 1000
 
Umepuyanga kabisa maji ya Mwamposa ni maji ya kawaida yanayouzwa dukani yeye mwenyewe kwenye TV anasema beba maji uliyokuja nayo niyaombee ,Kila nikiangalia TV sijawahi kusiki akiwalzimisha watu LAZIMA wanunue maji yanayouzwa dukani kwake shs 1000
Alipoenda mza, kijiko Cha mchanga kiliuzwa 9,000/=

Huduma zote za kibenki zilikuwa pale.
 
Wapi wameandika mavi ya njiwa? Hii tabia ya kujitungia maneno kwenye biblia mtaacha lini?
Hapo ni mavi ya mwanadamu kwa mujibu wa hilo andiko. We endelea kula hiyo mikate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…