Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,322
- 3,648
- Tatizo hili linaendelea hata baada ya kukamilika mradi wa maji wa tanki la bangulo uliogharimu bilioni 36.8 na maji hamna Kinyerezi.
Wakazi wa Kinyerezi wapo katika wakati mgumu maji ya Dawasa yanatoka dakika 30 mara moja kwa mwezi,magari ya maji boza yanauza maji ya chumvi sh 24,000 lita 2000 ambayo kila nyumba inatumia kwa siku tatu,kwa wiki itahitaji uite gari la maji mara mbili na kulipa 48,000 lita 4000 ili uweze kuyatumia maji kwa siku sita,adha ya kukosa majisafi inaendekea kuwakumba wakazi wa Kinyerezi hata sasa baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kutangaza kuanza kusambaza Majisafi katika maeneo ya Kinyerezi toka mwezi Februari 2025 lakini ajabu hamna maji!!?
Ilielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasa Mhandisi Bwire kuwa baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Bangulo uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 36.8 utahudumia wakazi zaidi ya 450,000 na akaendelea kusema utekelezaji wake ulijumuisha ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi maji lita Milioni 9 na ulioenda sambamba na ulazaji wa mtandao wa bomba wenye Kilomita 108 kwa hiyo kuanzia mwezi February 2025 wakazi wa Kinyerezi watapata maji ila leo ni mwezi July 2025, Kinyerezi hakuna maji,je kuna siasa hata kwenye utendaji wa huduma muhimu kwa Wananchi?
-Je tunahujumiwa wakazi wa Kinyerezi Ili biashara ya kuuza maji iendelee milele hapa Kinyerezi!!??
Mh Rais,tumewalilia watendaji wa ukanda huu bila mafanikio,inavyoonekana upande huu unachangamoto na inakinzana na mamlaka,Mh Rais hii inavyoonekana hata Waziri ameshindwa badala yake amekemea jambo bila kujua tatizo,tunapokea maji mara Moja kwa mwezi yanatoka dakika 30 halafu yanakatika,Mimi nipo mtaa wa Msingwa kwa Babu Ali,mwisho wa mwezi Mita yangu inasomeka,umetumia Unit 3, Ndugu Xxxx, Akaunti: B10400005078, Meter: 18054378, Dira yako ya maji imesomwa tarehe 2025-07-11 17:58:23 kwa usomaji wa sasa 244, uliopita ulikuwa 241
Matumizi yako ni unit 3. Hakiki usomaji huu kwenye dira yako kabla ya ankara yako kuandaliwa au piga bure huduma kwa wateja No: 0800110064,
Matumizi ya maji kwa wiki ni lita 4000@ nyumba 1,tukinunua 48,000 kwa wiki 1 na 192,000 kwa wiki 4,sasa unaishi kwa kusubiri huruma dawasa wafungue maji kwa dakika 30 mara Moja kwa mwezi ndipo tupate,watendaji wanasingizia msukumo, kila siku wanadai msukumo, yapata mwezi wa nne sasa toka tanki la bangulo lizinduliwe na kuambiwa na Mtendaji mkuu wa Dawasa kuwa adha ya maji Kinyerezi imeisha!!? Bustani zetu zinakufa kwa sababu tunamwagilia maji ya chumvi ambayo ni bei rahisi sh 24,000 huku maji ya Dawasa yakiuzwa na boza 36,000 kwa lita 2000,uwezo wetu wa kununua maji chumvi unasababisha majani yanakauka,miti ya matunda inakauka,ukijani unaondoka,je mnataka Kinyerezi iwe Jangwa!!!??Mh Rais tusaidie kuondoa adha hii.
Nakala kwako@mbunge Bonna
RC
DC
Waziri Jumaa.