DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aliyeandika nahisi sio mwenyeji wa lake zone maana kanda yote iyo samaki wengi wanaoliwa ni fresh from the lake tofauti na pwani ambapo samaki uwa sio fresh hadi kupelekea kukaangwa kabla ya kupikwa,
Wewe kweli wa mikoani, pwani tunapenda Samaki wa kukaanga.

Samaki wa kukaanga ndio mpango mzima, ni kolekole tu ndio anakubali ukimchesha supu na kukatia karoti, hoho na kitunguu
 
Amekurupuka period!

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
Kuna kipindi Lissu alikuwa anawatetea waathirika wa kemikali za mgodini kule nyamongo Tarime, wale watu walikuwa wameathirika ngozi zimebabuka hatari.......sasa badala ya kutatua tatizo la migodi kutiririsha kemikali kwenye mazingira na kwenye vyanzo vya maji kwa matumizi ya watu na wanyama wao wanakuja na vitu ambavyo ni simulizi ambazo hazina scientific basis yoyote, mara maji ya kuoshea maiti, sijui kemikali za kuhifadhi samaki ambazo hata hazijulikani ni zipi......​
 
Naheshimu mawazo Yako.

Naomba unitofautishie kati ya
1. Maono. 2. Ndoto na chanzo chake na 3. Ulimwengu wa ROHO.
Mkuu, Ukiwaza kwa kina jambo linalokuhusu wewe mwenyewe au jamii yako kwa ujumla na huoni hatima yake itakuwaje na huku anamwomba Mungu, Mungu kwa uweza wake anaweza kukuonesha majibu kwa njia ya Maono. Lengo la Maono ni kukutanabahisha ukae uwe umejiandaa kwa hali hiyo itakapowadia.
Akili ya binadamu(Tofauti na akili ya mnyama) inauwezo mkubwa sana wa kuhifadhi kumbukumbu na kuzihuisha (Update) mara kwa mara ili ziendane na wakati. Mtindo mmojawapo wa ku-update memory ni pale mtu ametulia kabisa (iwe mchana au usiku) akili kwa namna ilivyoumbwa huzivuta taswira za mambo uliyopitia(au mapito yako) na kuweka a Basket of alternative options yaani ni kama unavyojiuliza mwenyewe jee, kama ingekuwa hivi ingelikuwaje n.k. hizo ni Ndoto na wakati mwingine Mungu kwa upendo wake anaweza kukupa majibu sahihi ya jambo linalokuhusu au pia hata Ibilisi anaweza kukulaghai kwa kutumia Ndoto zako.
Kumbuka na zingatia kwamba Binadamu ni mwili na Roho. Mwili ni huu tunaouona na ndio ninatumia vidole vyake kukuandikia hapa. Lakini pungufu kubwa la mwili ni kwamba mwili hauwezi kuiona Roho. Roho ipo kana kwamba imejificha. Ndo maana huwezi kujua kilicho ndani ya Roho ya binadamu mwenzako hata kama ni mkeo au mtoto wako. Mungu kwa kuweka Pungufu hilo ndani ya mwili imesaidia sana watu waishi kwa amani.Lakini pia Mungu amewafunulia baadhi ya watu aina fulani ya Hekima inayowawezesha watu hao kutambua mambo yaliyojificha (Yaliyo rohoni) i.e Mambo ya Kiroho. Sasa Ukichukulia mambo ya kiroho kwa mapana yake utaupata Ulimwengu wa Roho. Ni katika ulimwengu wa Roho utaweza kuona na kupata maana halisi ya Ulimwengu wa Roho pale watu wanaposema Mungu muumba wa mbingu na nchi na Vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.Visivyonekana ni vipo katika ulimwengu wa Roho. (Naomba niishie)
 
Kwa nini hili usingecomment kwenye thread husika badala ya wewe kufunguwa thread nyingine? Au huwa ni fasheni kufunguwa Uzi?
 
Hili wameibika naro wapi Tena?
Haya maji yamekua yakitumiwa na baadhi ya wanawake kwa ,wa ume zao kama limbwata, Ali maarufu "Mnyoshe"
Hii ya mvuto nipya kabisa na hayawezi kutumika kiasi kikubwa Haina budi huo utafiti urudiwe.
 
Sasa tule nn walaji samaki Kaz mnayo ss Wala nguruwe na ngombe tuna Jambo letu
 
Huu ndio ukweli
 
Sasa hivi nimemaliza kula apple 🍎 itabidi niache kula tena !
 
Nadhani Majibu(scientific Findings) yatakayotokana na UTAFITI WA KINA ndio itakuwa hitimisho la malumbano haya.
 
Nadhani Majibu(scientific Findings) yatakayotokana na UTAFITI WA KINA ndio itakuwa hitimisho la malumbano haya.
Ili kuepuka mgongano wa kimaslahi Scientific findings nani atazitoa na zitakuwa zimefanywa na akina nani ?
 
Umeongea yote mkuu, hii kitu haingii akilini ata kidogo, akili na uwezo wako ni mkubwa mnoo.
Kama kweli maji ya kuoshea maiti yanatumika kuhifadhi samaki tatizo lingekua kubwa nje ya Mwanza kuliko Mwanza maana Mwanza kunapatikana samaki fresh na samaki wanaotoka nje ndo wanatakiwa kuhifadhiwa.
Natamani comment yako iwe [emoji419] juu kabisa ili kila mtu aisome tuachane na hii cheep propaganda.
 
Ili kuepuka mgongano wa kimaslahi Scientific findings nani atazitoa na zitakuwa zimefanywa na akina nani ?
Enhe! Hapo tena..... Mkuu, tumewaamini na kuwapa kazi ya Utafiti baadhi ya Watanzania wenzetu na kuwaweka katika Taasisi zitakazohusika na shughuli hizo. Endapo itabainika au hata kuhisiwa kwamba Utafiti na Majibu ya Utafiti huo Vitachakachuliwa basi ni bora ku-outsource shughuli hiyo na mchakato wa kumpata mtafiti au Consultant iwe ni kwa njia ya Tenda.( Lakini bro. ujue ni gharama kubwa).
 
Kila kukicha afadhali ya jana

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 

Hivyo ndio inavyotakiwa iwe, ila kuna ilivyo. Ww ndio unapata tabu kupata hiyo chemical lakini wenzako wanaipata kama kawaida, na wanaitumia vile vile.
 
Ukioa samaki mbichi hata nzi awasogei usinunue sumu hio
 
"Hili nalo la vijimaji vya kuoshea maiti Kuhifadhia samaki, Mwanangu Mashimba na Mtaalamu wetu wa Mchongo Mwanangu Profesa Manyele muende mkalitizame kwa kina"
 
Pia kuna haja ya kuangalia migodi na hizo elution plants kwa namna wanao Dhibiti taka zitokanazo na uchenjuaji wa madini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…