Katika baadhi ya nyakati, wakazi wa maeneo ya kanda ya Ziwa, hususan wilaya ya Ukerewe, wameripoti kushuhudia maji ya Ziwa Victoria yakibadilika rangi na kuonekana ya buluu kijani kibichi chenye mchanganyiko wa bluu Hali hii huwavutia na kuwashangaza wengi kutokana na kutokuwa ya kawaida.
Kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa maeneo hayo, tukio hili hujitokeza zaidi katika mwezi wa sita (Juni), hasa kuanzia majira ya asubuhi (karibu saa moja) hadi mchana, na kisha huonekana tena kwa kiwango kikubwa zaidi nyakati za jioni.
Uchunguzi uliofanywa kwa kutumia nyenzo mbalimbali umebaini kuwa mabadiliko hayo ya rangi husababishwa na kuongezeka kwa maua hatari ya mwani (Harmful Algal Blooms – HABs), hasa jamii ya cyanobacteria. Ukuaji huu huchochewa na kuongezeka kwa virutubishi kama vile nitrojeni na fosforasi vinavyoingia majini kutokana na uchafuzi wa mazingira, pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa kawaida, maua haya ya mwani huonekana kama matabaka ya kijani kibichi juu ya maji, lakini pia yanaweza kuathiri namna mwanga unavyorudishwa majini na hivyo kufanya maji yaonekane na rangi ya bluu au mng’ao wa pekee.
Hali hii ni hatari kwa viumbe vya majini, shughuli za uvuvi, na afya ya binadamu kwa sababu ya uwepo wa sumu zinazojulikana kama cyanotoxins.
Kwa kurejelea utafiti uliofanywa na Jofrey J. Mchau mwaka 2019, wenye kichwa kinachosema “Harmful algal bloom and associated health risks among users of Lake Victoria freshwater: Ukerewe Island, Tanzania,” imeelezwa kuwa ongezeko la maua haya linaweza kusababisha madhara makubwa kwa viumbe wa majini, hususan samaki, pamoja na kuathiri mfumo mzima wa ikolojia ya ziwa.
Aidha, utafiti huo unaonya kuwa matumizi ya maji yenye hali hiyo si salama kwa binadamu madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na:Kuwasha au muwasho kwenye ngozi,Kuharisha na Kutapika
Kwa kuzingatia maelekezo ya Shirika la Afya Duniani(WHO ) matumizi ya maji yasiyotibiwa kutoka ziwani, hasa wakati wa uwepo wa maua haya ya mwani, yanaweza kusababisha hatari kubwa za kiafya. Tafiti zinaonyesha kuwa kutumia maji hayo bila kuyatibu kunaweza kuhusishwa na athari mbalimbali mbaya kwa afya ya binadamu.

- Tunachokijua
- Katika baadhi ya nyakati, wakazi wa maeneo ya kanda ya Ziwa, hususan wilaya ya Ukerewe, wameripoti kushuhudia maji ya Ziwa Victoria yakibadilika rangi na kuonekana ya buluu kijani kibichi chenye mchanganyiko wa bluu Hali hii huwavutia na kuwashangaza wengi kutokana na kutokuwa ya kawaida.