Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #21
hakuna atakayekwenda mahakamani, unless wakubaliane kuwa JK, Lowassa, Mkapa, watakuwa tayari kusimama kama mashahidi...
FMES.. CCM wana njia ya kutokea.. natamani niwasaidie... lakini haya majibu yao ya kihuni ni kujiongezea shimo...
mhm, huu moto sasa ! kumbe hapa pana maongezi mengine, subiri nitundike kambi hapa kidogo !
...njaa itakuua mnafiki wewe!
[size]Dua.. mahakama yetu haina njia ya kuhakikisha maamuzi yake yanatelekezwa. Period.[/size]
FMES.. CCM wana njia ya kutokea.. natamani niwasaidie... lakini haya majibu yao ya kihuni ni kujiongezea shimo...
Wahuni hupewa majibu ya kihuni. Naishangaa serikali kupoteza muda na hawa wahuni. Wengi ni hypocrites, wanasimama kwenye majukwaa kuongea kuhusu ufisadi wakati wao wenyewe wanapocket fedha za vyama vyao.
Ni yale yale.
Hivi unafikiri Nyerere angedeal nao vipi hawa wahuni...eeh wapinzani?
COMMENT YA DR. SLAA: Nadhani ili serikali nayo isiwapotoshe wananchi inatakiwa kutoa majibu ya kina na kuridhisha. Taarifa niliyoitoa kupitia Maelezo ya Hoja yangu iliyokuwa iwasilishwe Bungeni yalikuwa na maswali ya msingi ambayo hayawezi kujibika tu kwa kutamka kuwa ni ya uzushi. Kila mtu anaweza kutamka hivyo. Serikali inatakiwa kujibu maswali ya msingi yaliyokuwepo kwenye maelezo niliyotaja mathalan:JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU SHUTUMA ZA RUSHWA DHIDI YA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI
1.0 UTANGULIZI:
1.1 Tarehe 15 Septemba, 2007 katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Mheshimiwa Dkt. Wilbrod Peter Slaa, Mbunge wa Karatu (CHADEMA), akishirikana na wanasiasa wenzake wa vyama vya upinzani, alitoa tamko hadharani akiwatuhumu viongozi kadhaa wa Umma kwamba wameshiriki katika vitendo vya rushwa.
1.2 Kufuatia shutuma hizo, gazeti la kila wiki la Mwana Halisi limekuwa likisambaza habari za tuhuma hizo za Mhe. Dkt Slaa, bila kutafuta ukweli wa tuhuma zilizotolewa.
2.0 MTAZAMO WA SERIKALI KUHUSU RUSHWA:
2.1 Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa nchini ikiwemo Mkakati wa Kupambana na Rushwa Awamu ya Kwanza wa mwaka 1997-2004 na Mkakati wa Kupambana na Rushwa Awamu ya Pili wa mwaka 2005-2010. Serikali ya Awamu ya Nne imeendelea kutekeleza mkakati wa kudhibiti tatizo la rushwa nchini ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi (2005) ya Chama cha Mapinduzi. Katika Ibara ya 110, Ilani ya Uchaguzi inaelekeza ifuatavyo:-
(a) Kuendelea kuchukua hatua za kisheria, kiutawala na kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa.
(b) Kujenga mazingira mazuri zaidi yatakayowapa wananchi uwezo, ari na ujasiri zaidi katika kupambana na rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.
(c) Kufuatilia malalamiko ya baadhi ya wananchi kwamba kuna watu wengi wanaolimbikiza mali nyingi kama majumba, mashamba n.k. kuliko uwezo wa mapato halali wanayoyapata.
(d) Kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika utendaji wa Serikali.
(e) Kushughulikia kwa nguvu zaidi malalamiko ya wananchi ya kero ya rushwa ndani ya vyombo vya dola kama vile Polisi na vyombo vya huduma za jamii kama hospitali, shule na mahakama.
(f) Katika mafunzo ya elimu ya uraia, wananchi watachochewa kuichukia rushwa katika siasa na kuwadharau viongozi watoa na wapokea rushwa.
2.2 Pamoja na maelekezo haya ya Ilani ya Uchaguzi, azma ya kupambana na rushwa ilifafanuliwa vyema na Mheshimiwa Rais wakati alipozindua Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma tarehe 29 Desemba, 2005.
2.3 Katika kutekeleza ahadi zilizotokana na Ilani ya Uchaguzi na hotuba hiyo ya Mhe. Rais, Serikali imeandaa na kupitisha Sheria mpya ya TAKUKURU kwa lengo la kuiongezea mamlaka ya kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa wa rushwa. Vile vile, sheria mpya imeongeza wigo zaidi wa vitendo vitakavyochukuliwa kisheria kuwa ni makosa ya rushwa. Sambamba na hatua hizo Serikali imeanzisha Ofisi za TAKUKURU kwenye Wilaya zote nchini na kuzipatia vifaa bora vya kazi pamoja na mafunzo kwa watumishi.
2.4 Aidha, azma ya Serikali inathibitishwa na jinsi ambavyo imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2005/2006. Kufuatia kuchapishwa na kusambazwa kwa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais aliitisha Mkutano wa viongozi na Watendaji Wakuu wote wanaohusika ambapo taarifa hiyo ilijadijiliwa kwa kina na maelekezo ya kutatua upungufu uliodhihirika. Hivi sasa Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa, Halmashauri za Serikali za Mitaa na Taasisi zote za Umma zinaendelea na utekelezaji wa maelekezo hayo.
2.5 Ili kushirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, Serikali imebuni na kuanzisha njia rahisi za mawasiliano zinazowawezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo na matukio ya rushwa. Njia hizo ni pamoja na kutangazwa hadharani kwa namba za simu za Viongozi na kuanzishwa kwa tovuti maalum kwa ajili ya kupokea taarifa za rushwa na malalamiko mengine ya wananchi. Vile vile, Serikali ikishirikiana na wadau wengine inatekeleza mpango wa kuongeza uwezo wa Waandishi Habari kuchunguza kwa kina tuhuma nzito za Rushwa na maovu mengine katika jamii (Investigative Journalism).
2.6 Ni dhahiri kuwa Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa nchini. Matarajio ya Serikali katika kuchukua hatua hizi ni kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine katika jamii. Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongoni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili.
3.0 TUHUMA KUHUSU BENKI KUU YA TANZANIA
3.1 Tamko la Mheshimiwa Dk. Slaa na wanasiasa wenzake lilijumuisha tuhuma kadhaa nzito kuhusu uendeshaji wa Benki Kuu. Tuhuma hizo zilihusu gharama za ujenzi wa majengo mapya ya Benki Kuu ya Dar es Salaam na Zanzibar, madai ya malipo hewa, pamoja na ushiriki wa Benki Kuu katika makampuni binafsi kinyume na maslahi ya umma.
3.2 Baada ya kufuatilia kwa kina kuhusu tuhuma hizi, Serikali inatoa Tamko kuwa ni za uzushi na upotoshaji wa makusudi wa ukweli. Aidha, tuhuma kuhusu majina ya wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini na baadaye kulipwa na Benki Kuu, ni vyema ieleweke kuwa wadai wanaozungumziwa hawakuingiza fedha za kigeni nchini bali walilipa fedha za Kitanzania kwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kama malipo ya kuagiza bidhaa kutoka nje katika miaka ya 80, lakini Benki Kuu ikashindwa kufanya malipo hayo baada ya kupokea fedha kutoka NBC kutokana na kutokuwa na fedha za kigeni enzi hizo.
COMMENT YA DR.SLAA: a) Uchunguzi unaofanywa na anayeitwa International Auditing Firm ni tone la Mchanga katika Bahari. Ukaguzi huo hauhusishi maeneo niliyoyaeleza ambako fedha za Walipa kodi zimetumika katika Meremeta, Tanagold, Mwananchi Gold Company Ltd, na kadhalika. Inahusu tu eneo la EPA, Isipokuwa kama Terms of Reference zimeongezeka tofauti na zilizotolewa Bungeni. Iwapo hivyo ndivyo, Audit inayofanyika ni sehemu ndogo sana na Hoja yangu haiwezi kupata majibu kutokana na Ukaguzi huo.Dr.Slaa.3.3 Baada ya tuhuma za uwezekano wa kuwepo kwa malipo yasiyo sahihi kupitia Akaunti hii kujitokeza, Serikali ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuteua mkaguzi wa kimataifa (International Auditing Firm) kwa utaratibu wa wazi wa zabuni ili kufanya uchunguzi maalum na kuwasilisha taarifa yake Serikalini. Uchunguzi huo unaendelea na Serikali inasubiri ukamilike ili kuamua hatua muafaka. Mhe. Dk. Slaa na wenzake wanafahamu vizuri hatua zilizochukuliwa na Serikali katika suala hili kwani Serikali ilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari na imetoa maelezo ya hatua za utekelezaji wake Bungeni mara kadhaa.
COMMENT ZA DR.SLAA: Maelezo ya Serikali inayoonyesha aliyeyatoa hajui msingi wa hoja au hajafanya utafiti wa kina:-3.4 Hoja nyingi za Mheshimiwa Dk. Slaa kuhusu Benki Kuu zinadaiwa kutokana na Hoja za Ukaguzi zilizotolewa na CAG baada ya kukagua hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/06. Serikali imepitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu hizo, lakini haikuona hoja za ukaguzi zinazodaiwa kutolewa na CAG. Isitoshe Taarifa ya Hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/2006 ziliwasilishwa katika Kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge mapema mwaka huu na kukubaliwa na Kamati hiyo. Aidha, Kamati hiyo iliwasilisha taarifa yake Bungeni na Bunge likairidhia. Vile vile, kwa nyakati tofauti, Kamati ya Fedha ya Uchumi ya Bunge pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) zimepata nafasi ya kutembelea miradi ya ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Dar es Salaam na Zanzibar ili kupatiwa maelezo ya kutosheleza kuhusu utekelezaji na gharama za miradi hiyo. Hivyo haieleweki kuwa Mheshimiwa Dk. Slaa amepata wapi hoja hizi; yawezekana ni za kubuni.
COMMENT YA DR. SLAA: Inawezekana Mhusika anafanya kazi na Documents zisizo sahihi. Nadhani ni vema asome hoja yangu ilieleza nini kuhusu thamani ya Tshs 522,459,255,000. Hoja hiyo inahitaji majibu, na yatapatikana kimsingi wakati Serikali itakapoweka hadharani mkataba wa ujenzi, na Hati mbalimbali zilizopitisha Variations husika.Dr.Slaa.3.5 Nia mbaya ya Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake katika kutoa tuhuma hizi inadhihirishwa na upotoshaji wa makusudi wa takwimu zilizo katika hesabu hizi ili kupindisha ukweli. Kwa mfano, anaituhumu Benki Kuu kutumia Shilingi 522,459,255,000 (Bilioni 522.5) kwa ujenzi wa Twin Towers mjini Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kiasi hicho ni thamani ya mali zote za kudumu za Benki Kuu hadi tarehe 30 Juni, 2006. Taarifa hizi ziko wazi katika nyaraka zilizowasilishwa Bungeni na zinaweza kuthibitishwa na mtu yeyote kutokana na Taarifa ya Benki Kuu ya Mwaka 2005/06 iliyosambazwa kwa umma.
COMMENT YA DR.SLAA:4.0 TUHUMA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KATIKA KAMPUNI BINAFSI
Mheshimiwa Dk. Slaa vile vile ametoa tuhuma kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi ya kigeni na kwamba maafisa wa Umma kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo kunaashiria mgongano wa kimaslahi. Maelezo juu ya tuhuma hii ni kama ifuatavyo:-
(a) Tangold ni kampuni ya Serikali, inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kupitia Mfuko wa Udhamini wa Maendeleo (Tanzania Development Trust).
(b) Wakurugenzi wa Tangold wameteuliwa na Serikali ya Tanzania, wote ni watumishi wa Umma ambao ni pamoja na wale ambao Mheshimiwa Slaa anawatuhumu katika tamko lake. Watumishi hao wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Tangold kutokana na nafasi zao katika Utumishi wa Umma. Kuwa Mkurugenzi katika Chombo cha Umma hakusababishi mgongano wa kimaslahi kwani ni sehemu ya Utumishi wa Umma.
(c) Aidha, Wakurugenzi hawa wa Tangold hawana hisa katika kampuni hiyo kwa sababu hisa zake zote zinamilikiwa na Tanzania Development Trust kwa niaba ya Watanzania wote. Kwa maana hiyo Wakurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Tangold hawana maslahi yoyote binafsi zaidi ya kusimamia maslahi ya Watanzania.
COMMENT YA DR. SLAA:5.0 TUHUMA KUHUSU KAMPUNI YA ALEX STEWART (ASSAYERS):
5.1 Tuhuma kwamba kulikuwepo na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu hazina ukweli wowote, kwani Kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma na hakukuwa na shinikizo lolote. Hivyo shutuma hizi ni za uongo na upotoshaji.
5.2 Aidha, tuhuma ya rushwa katika mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart, jambo hili tayari liko mahakamani, hivyo si vyema kulielezea hapa.
COMMENT YA DR.SLAA:6.0 TUHUMA KUHUSU MADINI
Sekta ya madini ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu. Kutokana na unyeti wa sekta hii na tuhuma nzito zilizotolewa dhidi ya Serikali juu ya sekta hii, Serikali inaona ni vyema kutoa maelezo ya ufafanuzi zaidi. Hivyo, Serikali itatoa taarifa maalum na ya kina kuelezea wananchi juu ya sekta hili.
COMMENT YA DR.SLAA:7.0 TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA UNUNUZI NA UBINAFSISHAJI:
Tuhuma kuhusu uuzaji wa rasilimali za Taifa, ununuzi wa ndege ya Rais, ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB) hazina msingi wala ushahidi wowote na zinajaribu kujenga mazingira ya kujipatia umaarufu usiostahili. Taratibu za ununuzi na ubinafsishaji wa mali za umma zinazingatia uwazi na kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria. Kwa mfano, itakumbukwa kwamba mkakati mzima wa ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ulijadiliwa kwa kina na Bunge, ambalo pia lilitunga Sheria kadhaa zenye miongozo iliyozingatiwa katika kutekeleza zoezi hilo.
COMMENT YA DR.SLAA:8.0 HITIMISHO:
8.1 Kwa ujumla, tuhuma za Mheshimiwa Dk. Slaa dhidi ya Viongozi wa Umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya Serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa Taifa letu. Tafsiri pekee ya mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa programu iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2005) na kama ilivyotafsiriwa katika Bajeti ya mwaka 2007/08.
Comment ya dr. Slaa:8.2 Serikali inawahakikishia wananchi kuwa inapinga vitendo vya rushwa nchini kwa nguvu zake zote na msimamo wake ni thabiti kuhusiana na suala hili. Kama lengo la Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake ni kushiriki kupiga vita vitendo vya rushwa, wanashauriwa kuwasilisha tuhuma zao kwenye vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.
COMMENT YA DR. SLAA:8.3 Aidha, Serikali inawathibitishia wananchi kwamba haitavunjika moyo na itaendelea kuelekeza nguvu zote za kitaifa katika utekelezaji wa mipango yake ili kuondoa umaskini na kufikia lengo la maisha bora kwa kila mtanzania.
8.4 Maelezo haya ya Serikali yanadhihirisha kwamba Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake hawana hoja za msingi katika lengo lao la kutaka kuichafulia jina Serikali ya awamu ya nne. Lakini Serikali inaelewa kwamba hawa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda, lakini walishindwa vibaya na wananchi wakaichagua CCM ambayo iko madarakani na inachapa kazi kwa kasi kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Wananchi wanayaona mafanikio mengi. Kutokana na hali hiyo, inaelekea wanachokitafuta ni kile walichokikosa katika uchaguzi wa mwaka 2005 kwa kujaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi. Serikali inatoa tahadhari kuwa wananchi wasikubali upotoshaji huo.
8.5 Serikali ya awamu ya nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani. Hivyo, wananchi wawapuuze hao wanaotapatapa na kutaka kutuondoa katika lengo letu la kuimarisha uchumi na kuondoa kero za wananchi ili kuleta maisha bora kwa Watanzania.
Imetolewa na:
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO
DAR ES SALAAM
28 SEPTEMBA, 2007
Nilijua tu kuna siku ita-backfire!"Kwa ujumla, tuhuma za Dk. Slaa dhidi ya viongozi wa umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa taifa letu," ilieleza sehemu ya tamko hilo.
Tuhuma kwamba kulikuwa na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington, Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu, serikali ilisema si kweli.
Ilieleza kuwa kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma na hakukuwa na shinikizo lolote.
Nazikumbuka sana kauli hizi za serikali... Kila anachoongea raia YEYOTE ambaye hayumo kwenye 'list yao' basi huitwa 'Mzushi'!Katika tamko lake hilo, serikali, inaziita tuhuma zote za Slaa, kuhusu Benki Kuu (BoT), Kampuni ya Tangold na nyinginezo kuwa ni za kizushi na ambazo zimetolewa pasipo kufanyika kwa utafiti wa kutosha.
Na wao wenye 'nia njema' wakamshikilia Liyumba na mpaka sasa anahenya Keko!"Nia mbaya ya Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake katika kutoa tuhuma hizi, inadhihirishwa na upotoshaji wa makusudi wa takwimu zilizo katika hesabu hizi, ili kupindisha ukweli. Kwa mfano, anaituhumu Benki Kuu kutumia shilingi 522,459,255,000 (Bilioni 522.5) kwa ujenzi wa "Twin Towers" mjini Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kiasi hicho ni thamani ya mali zote za kudumu za Benki Kuu hadi tarehe 30 Juni, 2006. Taarifa hizi ziko wazi katika nyaraka zilizowasilishwa bungeni na zinaweza kuthibitishwa na mtu yeyote kutokana na Taarifa ya Benki Kuu ya Mwaka 2005/06 iliyosambazwa kwa umma," inasema taarifa hiyo ya serikali.
Kuna upuuzi mwingine watanzania hamtakiwi kunyweshwa mkanywa kama unavyokuja...SERIKALI imesema mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa masilahi ya taifa ikilinganisha na mikataba ya zamani ya madini, na kutaja faida za mradi huo wa uchimbaji dhahabu. Kutokana na hali hiyo, Serikali imesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwa katika kusaini mkataba wa Buzwagi, sheria na taratibu za nchi zilikiukwa, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma.
Taarifa ya Serikali iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wa hapa nchini na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini. Serikali ilieleza kuwa wataalamu waliohusika katika mchakato wa majadiliano ya mkataba huo na Kamati ya Ushauri ya madini iliyoupitisha, wote ni wazalendo na wakati wote walihakikisha masilahi ya nchi yanawekwa mbele.
"Kulinganisha na mikataba mingine iliyotangulia, mkataba huo wa Buzwagi unavyo vipengele vilivyoboreshwa zaidi," ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Vipengele ambavyo vimetajwa na serikali kuwa vimeboreshwa ni kupungua kwa asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na asilimia 50 miaka inayofuata; Kodi za zuio kwa kazi za kitaalamu kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi kufikia asilimia tano.