Majibu haya ya serikali ni ya Kihuni!!

Majibu haya ya serikali ni ya Kihuni!!

Dua.. mahakama yetu haina njia ya kuhakikisha maamuzi yake yanatelekezwa. Period.
 
hakuna atakayekwenda mahakamani, unless wakubaliane kuwa JK, Lowassa, Mkapa, watakuwa tayari kusimama kama mashahidi...

Kwenye hili inaonekana kuwa startegy inawapa taabu what to do, kwanza walinyamaza kimya, meaning walikuwa wanasubiri rais aseme something, he did not, kwa hiyo wakaamua kwenda solo wakitanguliwa na Mkono, then mabalozi wakubwa waliopo bongo wakaanza kuingilia kati, noma!

Sasa wako kwenye panick strategy, kila mmoja anasema lake, serikali inasema yake, hakuna kati yao anayejibu exactly tuhuma za Dr. Slaa, ambazo zinatakiwa kupelekwa mahakamani na sio kujibiwa kwenye majukwaa ya siasa,

Hiii kitu ni lazima iende mahakamani, ama sivyo CCM will never recover na hii sooo, hii ni bonge la soo, kwa sababu ni kwa mara ya kwanza Tanzania a politician is accussing other politicians with "facts" na sio hadithi, sasa ni mahakama tu inyoweza kuwasafisha CCM unless hawana imani na mahakama yao,

Binafsi sioni sababu ya kutokwenda mahakamani, yes kwenda huko itakuwa ni aibu ya mwaka maana yatafumuka tusiyoyataka wananchi kusikia, sasa what to do? Lakini ndio the only way iliyobaki kwa CCM kujisafisha, hawa kina Warioba wangenyamaza tu maana the more they talk wanaonekana wametumwa tu na kuna kitu wanaficha,

CCM na serikali, the minute wakuu wa nje walipoingilia that was it, sasa ni mahakamani tu kwenye sheria, otherwise mtatuulia chama chetu CCM, kuna ambao tuna imani nacho, sasa msiweke ubinafsi wenu mbele na chama nyuma, CCM ni kubwa kuliko nyinyi wote, na tunaweza kuwaweka pembeni wote mlioshutumiwa na kuanza na safu mpya, chini ya mwenyekiti wetu rais Kikwete, kwa hiyo msituletee hizi nyepesi nyepesi, at stake hapa ni taifa letu, sasa nendeni mahamakamani mkajisafishe, na sisi tunawasubiri kwenye uchaguzi wa wabunge tuwape dozier safi, kama mlivyoona kwenye uchaguzi wa NEC,

Tena ingewezekana mjiuzulu kwenye nafasi zenu mpaka mtakapojisafisha mahakamani, kwa nchi yoyote yenye kujali demokrasia hufanya hivyo viongozi watuhumiwa hukaa pembeni kwanza mpaka wajisafishe kwenye sheria, lakini bongo watakufa njaa maana hela nyingi wanazotuibia huishia kujengea nyumba mahawara tu, na kusomesha watoto wao nje, na pia kusubiri kampeni za uchaguzi wanunue pilau za kuwadanganya wananchi,

CCM na serikali acheni maneno mengi, twendeni mahakamani tukaongee legal facts!
 
FMES.. CCM wana njia ya kutokea.. natamani niwasaidie... lakini haya majibu yao ya kihuni ni kujiongezea shimo...
 
FMES.. CCM wana njia ya kutokea.. natamani niwasaidie... lakini haya majibu yao ya kihuni ni kujiongezea shimo...

Wahuni hupewa majibu ya kihuni. Naishangaa serikali kupoteza muda na hawa wahuni. Wengi ni hypocrites, wanasimama kwenye majukwaa kuongea kuhusu ufisadi wakati wao wenyewe wanapocket fedha za vyama vyao.

Ni yale yale.

Hivi unafikiri Nyerere angedeal nao vipi hawa wahuni...eeh wapinzani?
 
mhm, huu moto sasa ! kumbe hapa pana maongezi mengine, subiri nitundike kambi hapa kidogo !
 
there is no truth where there is money.....

yetu macho.
 
FMES.. CCM wana njia ya kutokea.. natamani niwasaidie... lakini haya majibu yao ya kihuni ni kujiongezea shimo...

Hapana mkuu, hii iende mahakamani tu either tunaishi kwa the rule of law au we are Banana Republic,

njia ya CCm kutoka inapaswa kuwa mahakama tu, anything less than mkondo wa sheria tunakuwa Banana Republic we are not there yet!,

Dr. Slaa atoe ushahidi wake watuhumiwa wajibu, let the legal dual process proceed, and let the chips fall where they may enough na blah! blah! Mimi sasa nasubiri tu mahakamani! kwenye hili wamechelewa, I mean it is too late kuleta ujanja wowote zaidi ya kwenda mahakamani!
 
Inawezekana kabisa hakuna anayejua hoja ya Dr Slaa ina uzito gani kutokana na kulewa madaraka mno na kuiba sana. Hata wameshindwa kufikiri sawa sawa hawa wenzetu...

Wameshindwa waanzie wapi kutoa ufafanuzi...completely off target... jibu hili linathibitisha competence ya serikali yetu jinsi ilivyo!
 
Kama kweli kuna atayekwenda mahakamani, basi huyo ni capable wa kuonyesha kuwa si mfisadi...otherwise wanazuga kinga sana, ni vigumu kuamini kama hiyo ndiyo level ya competence kweli au wanafanya makusudi hawa
 
Wahuni hupewa majibu ya kihuni. Naishangaa serikali kupoteza muda na hawa wahuni. Wengi ni hypocrites, wanasimama kwenye majukwaa kuongea kuhusu ufisadi wakati wao wenyewe wanapocket fedha za vyama vyao.

Ni yale yale.

Hivi unafikiri Nyerere angedeal nao vipi hawa wahuni...eeh wapinzani?

Naomba uweke ushahidi hapa mkuuu maana hizi ni tuhuma nzito kuwa wanakula pesa za vyama vyao, hebu fafanua na weka ushahidi .
 
Serikali sasa yaweka wazi faida ya Buzwagi

Mwandishi Wetu
HabariLeo; Tuesday,October 02, 2007


SERIKALI imesema mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa masilahi ya taifa ikilinganisha na mikataba ya zamani ya madini, na kutaja faida za mradi huo wa uchimbaji dhahabu. Kutokana na hali hiyo, Serikali imesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwa katika kusaini mkataba wa Buzwagi, sheria na taratibu za nchi zilikiukwa, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma.

Taarifa ya Serikali iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wa hapa nchini na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini. Serikali ilieleza kuwa wataalamu waliohusika katika mchakato wa majadiliano ya mkataba huo na Kamati ya Ushauri ya madini iliyoupitisha, wote ni wazalendo na wakati wote walihakikisha masilahi ya nchi yanawekwa mbele.

“Kulinganisha na mikataba mingine iliyotangulia, mkataba huo wa Buzwagi unavyo vipengele vilivyoboreshwa zaidi,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Vipengele ambavyo vimetajwa na serikali kuwa vimeboreshwa ni kupungua kwa asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na asilimia 50 miaka inayofuata; Kodi za zuio kwa kazi za kitaalamu kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi kufikia asilimia tano.

Eneo jingine ni kodi za zuio kwa gharama za utawala kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi asilimia 15; Masharti ya kununua bidhaa na huduma mbalimbali nchini; na kuchangia mfuko wa uwezeshaji dola za Marekani 125,000 kwa mwaka.

Serikali pia imesema ujenzi wa mgodi utakapokamilika na uzalishaji kuanza rasmi inatarajiwa kwamba miaka 10 ya kwanza ya uendeshaji wa mradi huo utakuwa na faida nyingi, ikiwamo mrahaba na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia dola za Marekani milioni 198.8. Faida nyingine zilizotajwa na serikali ni ajira kwa Watanzania 696 wa fani mbalimbali; kodi zinazotokana na mishahara ya wafanyakazi (PAYE) dola za Marekani milioni 50.3 na ujenzi wa laini ya umeme utakaogharimu dola za Marekani milioni 30.

“Laini hii itawezesha upatikanaji wa nishati ya umeme ambayo ni pamoja na maeneo ya mji wa Kahama, vijiji vya Mwine, Chapulwa, Mwendakulima, Sangiwa,” ilisema taarifa hiyo na kutaja faida nyingine kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya uchumi na jamii kama vile shule na zahanati katika maeneo yanayozunguka mgodi.

“Hivi karibuni pamejitokeza baadhi ya wanasiasa hususan kutoka vyama vya upinzani kutoa matamshi hadharani, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma walioko madarakani sasa au awamu zilizopita kuwa walikiuka taratibu au kuvunja sheria kwa kusaini mikataba ya madini,” ilisema taarifa hiyo. Serikali ilisema viongozi hao wamejaribu kupotosha umma juu ya tafsiri sahihi za sheria inayoongoza mikataba hii.

Vile vile kuna jitihada za makusudi za kuuhadaa umma kwamba kusainiwa mkataba wa Buzwagi kulikiuka taratibu na sheria za nchi, ilisema taarifa hiyo. Katika kuwaelimisha wananchi, serikali imeelezea mchakato wa mkataba huo kwa kueleza kuwa mikataba ya uendelezaji wa madini ya mwaka 1998 inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya madini kuingia makubaliano na mmiliki au muombaji wa leseni kubwa ya uchimbaji madini.

Taarifa ilisema kwa mujibu wa kifungu hicho, Waziri hutakiwa kupata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kabla ya kusaini mkataba. Kampuni tanzu ya Barrick iitwayo Pangea Minerals ilipatiwa leseni ya utafutaji wa madini katika eneo la Buzwagi wilayani Kahama, Shinyanga kuanzia mwaka 2003.

Baada ya utafiti wa miaka takriban mitatu, kampuni ya Pangea Minerals iliwasilisha maombi yake serikalini ili kuingia mkataba wa uendelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini katika eneo hilo. Maombi hayo yaliambatanishwa na upembuzi yakinifu wa mradi huo. Timu ya wataalamu wa serikali ilianza majadiliano na kampuni ya Pangea Minerals kuanzia Mei mwaka jana kwa nia ya kuingia katika mkataba. Kufikia Februari 16 mwaka huu, taratibu zote za kisheria kwa ajili ya kusaini mkataba huo zilikuwa zimekwisha kukamilika na hatimaye mkataba huo kutiwa saini Februari 17 mwaka huu.

Katika hatua nyingine, malumbano juu ya suala la ufisadi na rushwa yanaweza yakafikia kiwango cha kuleta mafarakano na uhasama katika jamii yakizidi kiasi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Mstaafu Mark Bomani alisema kutokana na malumbano ya ufisadi yanayotokea kwa sasa, vitendo vya rushwa na ufisadi ni lazima vipigwe vita kwa nguvu zote, lakini sheria za kutuwezesha kufanya hivyo na sababu za kufanya hivyo vipo, kinachotakiwa ni utashi wa kufanya jambo hilo.
 
Nilikwisha ainisha kwamba uongo haufanani hata siku moja. Ona sasa!

Matamko yote ya serikali ni ya Kiimla hayalengi kujibu hoja bali yanalenga kuwachafua watoa hoja bila kujali uzito wa hoja.

Wasemapo kuna jitihada za makusudi za kuuhadaa umma wanatakiwa waziseme moja moja na kuzipa maelezo ya kutosha.

Serikali haiwezi kutoa matamko ya kubuni na kijumla kwamba kuna njama bila kusisema njama zenyewe.

Hawa wamelewa mvinyo wa madaraka.

Nakubali juu ya kodi za mishahara ya wafanyakazi na kazi zenyewe lakini changio lao ni Secondary.
Primary contributor ni Tax ya Dhahabu yenyewe na shughuli nzima ya kuchimba dhahabu.
Kuhusu kodi ya ardhi?

Mtumia ardhi yeyote ni lazima ailipie kodi serikalini hilo si ombi ni sheria.
Kodi ya Mapato ya dhahabu yenyewe?
Ukitengeneza Marimba Chair unatozwa kodi ya bidhaa yaani marimba chair, iweje dhahabu haitozwi kodi?
Kodi ya ushuru wa Barabara? Hii ni lazima walipe
Kodi uchafuzi wa Mazingira????
Siku wakiondoka mashimo yao atafukia nani?
Je kama ni open mining wapo tayari kupanda mimea ya kuzuia mmonyoko wa ardhi?

Huu ndo mkataba Mswano kuliko ile ya mwanzo?
Haya maneno kama ni ya kweli kuna haja ya kuipata mikataba yote na kuiweka hadharani watu wote tuisome.
Inaelekea watendaji wa serikali yetu pengine wanashindwa
tofautisha Maslahi ya taifa na Maslahi yao Binfsi.

Kwa sababu wamefanya kazi serikali muda mrefu hawajui serikali inaanzia wapi na kuishia wapi vile vile hawajitofautishi wao na serikali.

Tamko la serikali linadhihirisha kitu kimoja kwamba ili mradi Rushwa imetolewa na kupokelewa na Watanzania kadhaa, taifa limenufaika kwani watumishi wa serikali na serikali ni kitu kimoja!!!!!

Kuwabughudhi watumishi wa vyeo vya juu wa serikali waliopokea rushwa ni Kuhatarisha Usalama wa Taifa kwani wakiamua Kutumia Polisi, USalama wa Taifa, FFU, na JWTZ kuwanyamazisha watoa tuhuma kuna hatari ya;

Watu kuwekwa Selo kwa muda mrefu na Polisi bila kufunguliwa mashtaka.

Kupigwa virungu na FFU na kuumuzwa vibaya kunakoweza sababisha ulemavu wa maisha au hata kifo.

Kufunguliwa Kesi za uongo mahakamani na mahakimu na majaji kusimama upande wa serikali na hivyo haki kushindwa kutetendeka .

Kufuatwa na maofisa wa Usalama wa Taifa kila siku na kuulizwa maswali ya Kunya( Kama anavyoulizwa yule kijana aliyemlamba Swali zito MH sana Edward lowassa.)

Vile vile Usalama wa nchi na Amani unaweza hatarishwa na hasira kuu ya mmoja wa watuhumiwa,Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamua kuwaweka ndani Dr Slaa na Zitto kwa kutumia mamlaka anayopewa na katiba.

Kwa misingi yao Serikali ya SISIEMU Hoja nzima ya Buswazi ni kuhatarisha AMANI NA UTULIVU Kama si Usalama wa nchi.


Tunaijua serikali ya SISIEMU ni hodari wa kuandika na kujieleza iweje Suala la Buzwagi linakuwa gumu kulijibu hoja kwa hoja?

Wana JF na wananchi kwa ujumla, subirini kidogoo SIRIKALI wataleta tamko jingine la serikali.
 
Haya ndio majibu ya serikali , yanatia aibu sana ,



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU SHUTUMA ZA RUSHWA DHIDI YA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI


1.0 UTANGULIZI:

1.1 Tarehe 15 Septemba, 2007 katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Mheshimiwa Dkt. Wilbrod Peter Slaa, Mbunge wa Karatu (CHADEMA), akishirikana na wanasiasa wenzake wa vyama vya upinzani, alitoa tamko hadharani akiwatuhumu viongozi kadhaa wa Umma kwamba wameshiriki katika vitendo vya rushwa.

1.2 Kufuatia shutuma hizo, gazeti la kila wiki la Mwana Halisi limekuwa likisambaza habari za tuhuma hizo za Mhe. Dkt Slaa, bila kutafuta ukweli wa tuhuma zilizotolewa.

2.0 MTAZAMO WA SERIKALI KUHUSU RUSHWA:

2.1 Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa nchini ikiwemo Mkakati wa Kupambana na Rushwa Awamu ya Kwanza wa mwaka 1997-2004 na Mkakati wa Kupambana na Rushwa Awamu ya Pili wa mwaka 2005-2010. Serikali ya Awamu ya Nne imeendelea kutekeleza mkakati wa kudhibiti tatizo la rushwa nchini ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi (2005) ya Chama cha Mapinduzi. Katika Ibara ya 110, Ilani ya Uchaguzi inaelekeza ifuatavyo:-

(a) Kuendelea kuchukua hatua za kisheria, kiutawala na kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa.

(b) Kujenga mazingira mazuri zaidi yatakayowapa wananchi uwezo, ari na ujasiri zaidi katika kupambana na rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.

(c) Kufuatilia malalamiko ya baadhi ya wananchi kwamba kuna watu wengi wanaolimbikiza mali nyingi kama majumba, mashamba n.k. kuliko uwezo wa mapato halali wanayoyapata.

(d) Kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika utendaji wa Serikali.

(e) Kushughulikia kwa nguvu zaidi malalamiko ya wananchi ya kero ya rushwa ndani ya vyombo vya dola kama vile Polisi na vyombo vya huduma za jamii kama hospitali, shule na mahakama.

(f) Katika mafunzo ya elimu ya uraia, wananchi watachochewa kuichukia rushwa katika siasa na kuwadharau viongozi watoa na wapokea rushwa.

2.2 Pamoja na maelekezo haya ya Ilani ya Uchaguzi, azma ya kupambana na rushwa ilifafanuliwa vyema na Mheshimiwa Rais wakati alipozindua Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma tarehe 29 Desemba, 2005.

2.3 Katika kutekeleza ahadi zilizotokana na Ilani ya Uchaguzi na hotuba hiyo ya Mhe. Rais, Serikali imeandaa na kupitisha Sheria mpya ya TAKUKURU kwa lengo la kuiongezea mamlaka ya kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa wa rushwa. Vile vile, sheria mpya imeongeza wigo zaidi wa vitendo vitakavyochukuliwa kisheria kuwa ni makosa ya rushwa. Sambamba na hatua hizo Serikali imeanzisha Ofisi za TAKUKURU kwenye Wilaya zote nchini na kuzipatia vifaa bora vya kazi pamoja na mafunzo kwa watumishi.

2.4 Aidha, azma ya Serikali inathibitishwa na jinsi ambavyo imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2005/2006. Kufuatia kuchapishwa na kusambazwa kwa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais aliitisha Mkutano wa viongozi na Watendaji Wakuu wote wanaohusika ambapo taarifa hiyo ilijadijiliwa kwa kina na maelekezo ya kutatua upungufu uliodhihirika. Hivi sasa Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa, Halmashauri za Serikali za Mitaa na Taasisi zote za Umma zinaendelea na utekelezaji wa maelekezo hayo.

2.5 Ili kushirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, Serikali imebuni na kuanzisha njia rahisi za mawasiliano zinazowawezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo na matukio ya rushwa. Njia hizo ni pamoja na kutangazwa hadharani kwa namba za simu za Viongozi na kuanzishwa kwa tovuti maalum kwa ajili ya kupokea taarifa za rushwa na malalamiko mengine ya wananchi. Vile vile, Serikali ikishirikiana na wadau wengine inatekeleza mpango wa kuongeza uwezo wa Waandishi Habari kuchunguza kwa kina tuhuma nzito za Rushwa na maovu mengine katika jamii (Investigative Journalism).

2.6 Ni dhahiri kuwa Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa nchini. Matarajio ya Serikali katika kuchukua hatua hizi ni kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine katika jamii. Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongoni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili.

3.0 TUHUMA KUHUSU BENKI KUU YA TANZANIA
3.1 Tamko la Mheshimiwa Dk. Slaa na wanasiasa wenzake lilijumuisha tuhuma kadhaa nzito kuhusu uendeshaji wa Benki Kuu. Tuhuma hizo zilihusu gharama za ujenzi wa majengo mapya ya Benki Kuu ya Dar es Salaam na Zanzibar, madai ya malipo hewa, pamoja na ushiriki wa Benki Kuu katika makampuni binafsi kinyume na maslahi ya umma.


3.2 Baada ya kufuatilia kwa kina kuhusu tuhuma hizi, Serikali inatoa Tamko kuwa ni za uzushi na upotoshaji wa makusudi wa ukweli. Aidha, tuhuma kuhusu majina ya wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini na baadaye kulipwa na Benki Kuu, ni vyema ieleweke kuwa wadai wanaozungumziwa hawakuingiza fedha za kigeni nchini bali walilipa fedha za Kitanzania kwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kama malipo ya kuagiza bidhaa kutoka nje katika miaka ya 80, lakini Benki Kuu ikashindwa kufanya malipo hayo baada ya kupokea fedha kutoka NBC kutokana na kutokuwa na fedha za kigeni enzi hizo.
COMMENT YA DR. SLAA: Nadhani ili serikali nayo isiwapotoshe wananchi inatakiwa kutoa majibu ya kina na kuridhisha. Taarifa niliyoitoa kupitia “Maelezo ya Hoja yangu iliyokuwa iwasilishwe Bungeni yalikuwa na maswali ya msingi ambayo hayawezi kujibika tu kwa kutamka kuwa ‘ni ya uzushi’. Kila mtu anaweza kutamka hivyo. Serikali inatakiwa kujibu maswali ya msingi yaliyokuwepo kwenye maelezo niliyotaja mathalan:
a) Mkataba wa ujenzi wa Twin Towers utolewe hadharani ili wananchi wajue kuwa tuhuma ni uzushi au la.
b) Tenderers walikuwa nani, Tender ilitolewa lini na mchakato wake ulikuwaje,
c) Mshindi wa Tender ni nani na wakurugenzi wa Kampuni hiyo na sifa zao.
d) Gharama ilivyokuwa kwenye Mkataba na variations zote, na jinsi zilivyoidhinishwa( miniti za vikao vilivyoidhinisha)
Vinginevyo: Majibu ya Serikali hayakidhi haja, na hayajawasaida watanzania ambao ndio wenye mali na ndio wanaotaka kujua ukweli. Ukweli haupatikani kwa Tamko uchi bila vielelezo vyovyote.Dr.Slaa


3.3 Baada ya tuhuma za uwezekano wa kuwepo kwa malipo yasiyo sahihi kupitia Akaunti hii kujitokeza, Serikali ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuteua mkaguzi wa kimataifa (International Auditing Firm) kwa utaratibu wa wazi wa zabuni ili kufanya uchunguzi maalum na kuwasilisha taarifa yake Serikalini. Uchunguzi huo unaendelea na Serikali inasubiri ukamilike ili kuamua hatua muafaka. Mhe. Dk. Slaa na wenzake wanafahamu vizuri hatua zilizochukuliwa na Serikali katika suala hili kwani Serikali ilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari na imetoa maelezo ya hatua za utekelezaji wake Bungeni mara kadhaa.
COMMENT YA DR.SLAA: a) Uchunguzi unaofanywa na anayeitwa ‘International Auditing Firm” ni tone la Mchanga katika Bahari. Ukaguzi huo hauhusishi maeneo niliyoyaeleza ambako fedha za Walipa kodi zimetumika katika Meremeta, Tanagold, Mwananchi Gold Company Ltd, na kadhalika. Inahusu tu eneo la EPA, Isipokuwa kama “Terms of Reference” zimeongezeka tofauti na zilizotolewa Bungeni. Iwapo hivyo ndivyo, Audit inayofanyika ni sehemu ndogo sana na Hoja yangu haiwezi kupata majibu kutokana na Ukaguzi huo.Dr.Slaa.

3.4 Hoja nyingi za Mheshimiwa Dk. Slaa kuhusu Benki Kuu zinadaiwa kutokana na Hoja za Ukaguzi zilizotolewa na CAG baada ya kukagua hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/06. Serikali imepitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu hizo, lakini haikuona hoja za ukaguzi zinazodaiwa kutolewa na CAG. Isitoshe Taarifa ya Hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/2006 ziliwasilishwa katika Kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge mapema mwaka huu na kukubaliwa na Kamati hiyo. Aidha, Kamati hiyo iliwasilisha taarifa yake Bungeni na Bunge likairidhia. Vile vile, kwa nyakati tofauti, Kamati ya Fedha ya Uchumi ya Bunge pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) zimepata nafasi ya kutembelea miradi ya ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Dar es Salaam na Zanzibar ili kupatiwa maelezo ya kutosheleza kuhusu utekelezaji na gharama za miradi hiyo. Hivyo haieleweki kuwa Mheshimiwa Dk. Slaa amepata wapi hoja hizi; yawezekana ni za kubuni.
COMMENT ZA DR.SLAA: Maelezo ya Serikali inayoonyesha aliyeyatoa hajui msingi wa hoja au hajafanya utafiti wa kina:-
a) Taarifa ya ukaguzi ya BOT inayosemekana ilipelekwa kwa Kamati ya Fedha hazijafika Bungeni. Hadi leo hii, karibu ya mwaka mzima kinyume na Sheria ya BOT Taarifa hiyo haijawasilishwa Bungeni. Naomba Mhusika atazame sheria inayohusika. Huu ni uvunjaji wa Sheria usioweza kuvumilika kwa Taasisi kubwa kama BOT.
b) Inawezekana mhusika hajachunguza Maelezo ya Hoja yangu na Taarifa ya Ukaguzi ya CAG iliyowasilishwa kwa Kamati ya Fedha. Hoja zote nilizozieleza hazijajibiwa. Nadhani ni vema akachukua muda wake kufanya utafiti wa kina, asome maelezo ya hoja yangu ya msingi, na yapatiwe majibu. Lugha inawezekana imerekebishwa kidogo lakini hoja za msingi ziko pale pale. Watanzania tunataka kufahamu kilichojiri, na maelezo ya kina.
c) Mhusika anasema hoja za Dokta Slaa hazina ushahidi. Ni wazi, Ushahidi wa kamili ni sillaha yangu.Serikali ingelikubali Kuunda Kamati Teule, ushahidi wote ungelitolewa katika Kamati hiyo. Hivyo ushahidi wangu nitautoa siku itakapokuwa lazima kuutoa yaani Mahakamani. Iwapo Serikali inania ya kuuputa siyo kwa kutoa Matamko uchi bali kwa taratibu za kawaida za kisheria.


3.5 Nia mbaya ya Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake katika kutoa tuhuma hizi inadhihirishwa na upotoshaji wa makusudi wa takwimu zilizo katika hesabu hizi ili kupindisha ukweli. Kwa mfano, anaituhumu Benki Kuu kutumia Shilingi 522,459,255,000 (Bilioni 522.5) kwa ujenzi wa “Twin Towers” mjini Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kiasi hicho ni thamani ya mali zote za kudumu za Benki Kuu hadi tarehe 30 Juni, 2006. Taarifa hizi ziko wazi katika nyaraka zilizowasilishwa Bungeni na zinaweza kuthibitishwa na mtu yeyote kutokana na Taarifa ya Benki Kuu ya Mwaka 2005/06 iliyosambazwa kwa umma.
COMMENT YA DR. SLAA: Inawezekana Mhusika anafanya kazi na Documents zisizo sahihi. Nadhani ni vema asome hoja yangu ilieleza nini kuhusu thamani ya Tshs 522,459,255,000. Hoja hiyo inahitaji majibu, na yatapatikana kimsingi wakati Serikali itakapoweka hadharani mkataba wa ujenzi, na Hati mbalimbali zilizopitisha Variations husika.Dr.Slaa.

4.0 TUHUMA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KATIKA KAMPUNI BINAFSI
Mheshimiwa Dk. Slaa vile vile ametoa tuhuma kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi ya kigeni na kwamba maafisa wa Umma kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo kunaashiria mgongano wa kimaslahi. Maelezo juu ya tuhuma hii ni kama ifuatavyo:-

(a) Tangold ni kampuni ya Serikali, inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kupitia Mfuko wa Udhamini wa Maendeleo (Tanzania Development Trust).

(b) Wakurugenzi wa Tangold wameteuliwa na Serikali ya Tanzania, wote ni watumishi wa Umma ambao ni pamoja na wale ambao Mheshimiwa Slaa anawatuhumu katika tamko lake. Watumishi hao wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Tangold kutokana na nafasi zao katika Utumishi wa Umma. Kuwa Mkurugenzi katika Chombo cha Umma hakusababishi mgongano wa kimaslahi kwani ni sehemu ya Utumishi wa Umma.

(c) Aidha, Wakurugenzi hawa wa Tangold hawana hisa katika kampuni hiyo kwa sababu hisa zake zote zinamilikiwa na Tanzania Development Trust kwa niaba ya Watanzania wote. Kwa maana hiyo Wakurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Tangold hawana maslahi yoyote binafsi zaidi ya kusimamia maslahi ya Watanzania.
COMMENT YA DR.SLAA:
a) Nashukuru kwa serikali kuthibitisha tena kuwa TANGOLD ni kampuni ya Serikali na inamilikiwa na Serikali asilimia mia 100%. Iwapo hii ni kweli:-
b) Serikali haijaeleza kwanini Kampuni hii ya Serikali ya Tanzania ilisajiliwa Mauritius na kupata tu Tanzania Certificate of Compliance? Ilifanya Biashara gani kule Mauritius wakati Sheria ya Mauritius na hati ya usajili ilifakataza isifanye Biashara Marititus?
c) Serikali iwatangaze wahusika wote, ili jamii ya Watanzania iweze kupekua vitabu vya Sheria kama kuna “conflict of interest” popote?
d) Serikali inaitaja tu na kueleza ni ya Hoja yangu inataka kujua “Tanzania tumenufaika nini na Kampuni hiyo” na kwanini taarifa ya Tangold haiko kwenye Taarif ya Ukaguzi, angalau kutaja tu kuwa Benki kuu inahisa katika Kampuni hiyo? Haya Maswali yasipopata majibu ya kuridhisha Serikali bado itakuwa imetoa majibu ya kubabaisha.

5.0 TUHUMA KUHUSU KAMPUNI YA ALEX STEWART (ASSAYERS):
5.1 Tuhuma kwamba kulikuwepo na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu hazina ukweli wowote, kwani Kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma na hakukuwa na shinikizo lolote. Hivyo shutuma hizi ni za uongo na upotoshaji.

5.2 Aidha, tuhuma ya rushwa katika mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart, jambo hili tayari liko mahakamani, hivyo si vyema kulielezea hapa.
COMMENT YA DR. SLAA:
a)Serikali haijaeleza Kesi iliyofunguliwa mahakamani inahusu nini yaani ‘Grounds za kesi” . Ni vema Mhusika akasoma hoja yangu akaomba na file ya mahakamani ili aweze kuona grounds zilizoko mahakamani na uhusiano ukoje.
b) Hoja yangu iko wazi, kuna taarifa kuwa “Waziri anatuhumiwa kuwa anamiliki asilimia 12.5 ya Hisa ya Kampuni ya Alex Stewart. Serikali ingelituambia kuwa ilifanya utatifi ningelielewa.
d) Serikali itoe hadharani mkataba kati ya Benki Kuu (kwa niaba ya serikali) ili kubaini kuna hujuma/ufisadi au la. Kujitetea peke yake hakutoshi. Kinachotakiwa ni majibu ya Serikali siyo “TAMKO”, hii mtu yeyote anaweza kuitoa na akajifichamo.

6.0 TUHUMA KUHUSU MADINI
Sekta ya madini ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu. Kutokana na unyeti wa sekta hii na tuhuma nzito zilizotolewa dhidi ya Serikali juu ya sekta hii, Serikali inaona ni vyema kutoa maelezo ya ufafanuzi zaidi. Hivyo, Serikali itatoa taarifa maalum na ya kina kuelezea wananchi juu ya sekta hili.
COMMENT YA DR.SLAA:
a) Tunasubiri Ufafanuzi wa kina wa serikali kuhusu tuhuma hizi baada ya Mkataba kupatikana hadharana. Watanzania wanaendelea kuuchambua kwa nafsi zao. Hivyo tunasubiri kwa hamu kubwa ufafanuzi wa Serikali.Dr.Slaa.


7.0 TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA UNUNUZI NA UBINAFSISHAJI:
Tuhuma kuhusu uuzaji wa rasilimali za Taifa, ununuzi wa ndege ya Rais, ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB) hazina msingi wala ushahidi wowote na zinajaribu kujenga mazingira ya kujipatia umaarufu usiostahili. Taratibu za ununuzi na ubinafsishaji wa mali za umma zinazingatia uwazi na kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria. Kwa mfano, itakumbukwa kwamba mkakati mzima wa ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ulijadiliwa kwa kina na Bunge, ambalo pia lilitunga Sheria kadhaa zenye miongozo iliyozingatiwa katika kutekeleza zoezi hilo
.
COMMENT YA DR.SLAA:
a) Tuhuma tulizotoa katika eneo hili ni mahususi. Tulitaja majina na sababu ya kuwataja. Serikali imejibu utumbo na kuwapotosha watanzania. Kipindi cha majibu ya mafumbo kimesha, nadhani Serikali hii bado haijagundua hili. Tunahitaji majibu moja moja kwa kila tuhuma kama tulivyoyatoa. Vinginevyo Watanzania tunahaki bado ya kusema kuwa ufisadi mkubwa umejaa katika eneo hilo.
b) Tumeeleza kwa mfano ni kweli kuwa Plot no 15 Luthuli Street ilitumika kama Ofisi ya Biashara badala ya kuwa Ofisi ya Ikulu, inayolipiwa Kodi na watanzania wote?
c) Kama ni kweli Ofisi yetu ya Plot na 15 Luthuli Street kwa kipindi hicho chote Serikali imekusanya kodi ya pango kiasi gani?
d) Na masuali yote yaliyohusiana na tuhuma hizo zinahitaji kujibiwa kikamilifu. Serikali haijajibu, na imepoteza fedha za watanzania bure kuchapa Barua, kuzitawanya na kadhalika jambo ambalo linaongezea matumizi mabaya ya fedha za umma.


8.0 HITIMISHO:
8.1 Kwa ujumla, tuhuma za Mheshimiwa Dk. Slaa dhidi ya Viongozi wa Umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya Serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa Taifa letu. Tafsiri pekee ya mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa programu iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2005) na kama ilivyotafsiriwa katika Bajeti ya mwaka 2007/08.
COMMENT YA DR.SLAA:
a) Nashukuru kuwa Serikali imetumia Ilani ya Uchaguzi wa CCM kuwa kigezo chake. Nadhani hoja hii haihitaji kuelezwa kwa Watanzania kwani sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya Habari Matendo ya rushwa yalivyojaa ndani ya CCM yenyewe. Cha ajabu nini kama wanafanyiana hiyana wenyewe? Majibu yatapatikana tutakapotakiwa kutoa ushahidi mahali panapostahili kisheria.
b) Kujenga chuki. Ni nani kati yetu tunaotumia haki zetu za kikatiba kujua rasilimali na mali zetu au yeye anayezificha. Serikali ni lini ikawa mmiliki wa rasilimali za Taifa? Immesahau kuwa wana ‘hold in Trust” kwa niaba ya Wananchi, na hivyo, inapotakiwa ni lazima waje na majibu. Nadhani Watanzanania watatambua sasa nani anajenga chuki, nani anatafuta umaarufu wa kisiasa kati ya CCM na vyama vya Upinzani. Serikali ifahamu kuwa umaarufu hautafutwi. Utakuja tu mtu akitimiza wajibu wake. Kambi ya Upinzani tunatekeleza tu wajibu wetu, wananchi wakituamini watatuona maarufu. Hatuhitaji Serikali kututangazia hilo. Hata hivyo, tunashukuru kwa serikali kuendelea kutujengea umaarufu, kwani “Matendo ya Serikali ndiyo yametufikisha hapa tulipofika”.

8.2 Serikali inawahakikishia wananchi kuwa inapinga vitendo vya rushwa nchini kwa nguvu zake zote na msimamo wake ni thabiti kuhusiana na suala hili. Kama lengo la Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake ni kushiriki kupiga vita vitendo vya rushwa, wanashauriwa kuwasilisha tuhuma zao kwenye vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.
Comment ya dr. Slaa:
a) Sitegemei kuwasilisha Taarifa yeyote kwa vyombo vinavyohusika. Vyombo hivyo vinawataalam, wanalipwa kwa kazi hiyo, walitakiwa kuwa wamefanya upelelezi huo muda mrefu si leo. Taarifa nyingine zimesambaa zaidi ya mwaka sasa. Hakuna hatua iliyochukuliwa wala na Serikali wala na vyombo hivyo.
b) Ilishatangazwa hadharani kuwa Taarifa na vielelezo vya Dr.Slaa vimefikishwa kwa Polisi na ikasemekana kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nadhani hiyo inatosha. Serikali ziko ngapi haiwasiliani na vyombo vyake/
c) Iwapo hoja ilifanyiwa mizengwe izuiwe isiingie Bungeni kwa vile ikiingia Bungeni ina athari mbaya kwa Serikali, na kwamba inachunguzwa ‘Leakage hiyo ilifikaje kwa wapinzani” kama Serikali inatumia fedha za Walipa kodi kuchunguza “leakage” badala ya kuchunguza ubadhirifu kuna sababu gani ya kupeleka taarifa kwa vyombo hivyo?


8.3 Aidha, Serikali inawathibitishia wananchi kwamba haitavunjika moyo na itaendelea kuelekeza nguvu zote za kitaifa katika utekelezaji wa mipango yake ili kuondoa umaskini na kufikia lengo la maisha bora kwa kila mtanzania.

8.4 Maelezo haya ya Serikali yanadhihirisha kwamba Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake hawana hoja za msingi katika lengo lao la kutaka kuichafulia jina Serikali ya awamu ya nne. Lakini Serikali inaelewa kwamba hawa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda, lakini walishindwa vibaya na wananchi wakaichagua CCM ambayo iko madarakani na inachapa kazi kwa kasi kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Wananchi wanayaona mafanikio mengi. Kutokana na hali hiyo, inaelekea wanachokitafuta ni kile walichokikosa katika uchaguzi wa mwaka 2005 kwa kujaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi. Serikali inatoa tahadhari kuwa wananchi wasikubali upotoshaji huo.
COMMENT YA DR. SLAA:
a) Hoja hii ni ya watu walioshiwa na wamebaki na fikra mgando. Nani kati yetu kipindi chote hiki amezungumzia masuala ya uchaguzi. Ni kazi yetu ya kikatiba kuelezea watanzania pale ambapo Serikali imefanya makosa. Si kazi ya Upinzani kuipigia makofi Serikali. Kazi ya Kambi ya Upinzani duniani kote inajulikana. Na Ndiyo maana tuko kikatiba.
b) Serikali ijieleze kwa wananchi ieleweke isitafute mchawi. Leo wananchi wanalalamika kila kona ya nchi maisha Bora hayajaonekana inatuhusuje sisi? Chuki haitokani na Vyama vya Upinzani kutaka kujua rasilimali zao bali wananchi kuonja joto la jiwe baada ya ahadi isiyotekelezeka ya CCM mwaka 2005, na maneno matamu yanayoendeleo kutolewa na Serikali. Kama ni shule wananchi ndiyo wanaojua adha ya michango. Kama ni zahanati vivyo hivyo. Maisha bora yako wapo? Ajira ziko wapi? Mbona Bungeni waziri husika alipata kigugumizi kujibu ajira ngapi hadi leo zimepatikana miaka karibu miwili tangu uchaguzi. CCM ichunguze sababu ya chuki ya Wananchi isitafute mchawi mbali na korridor zake. Dr.Slaa

8.5 Serikali ya awamu ya nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani. Hivyo, wananchi wawapuuze hao wanaotapatapa na kutaka kutuondoa katika lengo letu la kuimarisha uchumi na kuondoa kero za wananchi ili kuleta maisha bora kwa Watanzania.



Imetolewa na:
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO
DAR ES SALAAM
28 SEPTEMBA, 2007
 
Ukisoma kwa makini utajua ni jinsi gani slaa amewabana kwani wamemtaja zaidi ya mara mia....,

Haya kazi kwenu kwenye kujibu nimeliweka tamko lote ili muweze kuijibu serikali kipengele kwa kipengele
 
Kaazi kweli kweli,kama utafiti uliofanyika wa kina ndo umeleta hayo majibu,wadanganyika tuna kazi!Kule mkoani Kagera mkimkamata mtu anaiba ndizi,mkamtwisha mkungu wake huo wa ndizi aliouiba mumpeleke polisi,watu hata polisi wakimuuliza njiani nini kimetokea hasemi nimekamatwa naiba ndizi bali husema,"ETI NIMEIBA NDIZI''

Hata tuwakabe vipi hawatasema kama ni mafisadi,wataendelea tu kusema,''ETI SISI NI MAFISADI''

Tuna sehemu moja tu ya kusemea kama ni mafisadi,''UCHAGUZI 2010''
 
"Kwa ujumla, tuhuma za Dk. Slaa dhidi ya viongozi wa umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa taifa letu," ilieleza sehemu ya tamko hilo.

Tuhuma kwamba kulikuwa na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington, Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu, serikali ilisema si kweli.

Ilieleza kuwa kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma na hakukuwa na shinikizo lolote.
Nilijua tu kuna siku ita-backfire!
Katika tamko lake hilo, serikali, inaziita tuhuma zote za Slaa, kuhusu Benki Kuu (BoT), Kampuni ya Tangold na nyinginezo kuwa ni za kizushi na ambazo zimetolewa pasipo kufanyika kwa utafiti wa kutosha.
Nazikumbuka sana kauli hizi za serikali... Kila anachoongea raia YEYOTE ambaye hayumo kwenye 'list yao' basi huitwa 'Mzushi'!

"Nia mbaya ya Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake katika kutoa tuhuma hizi, inadhihirishwa na upotoshaji wa makusudi wa takwimu zilizo katika hesabu hizi, ili kupindisha ukweli. Kwa mfano, anaituhumu Benki Kuu kutumia shilingi 522,459,255,000 (Bilioni 522.5) kwa ujenzi wa "Twin Towers" mjini Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kiasi hicho ni thamani ya mali zote za kudumu za Benki Kuu hadi tarehe 30 Juni, 2006. Taarifa hizi ziko wazi katika nyaraka zilizowasilishwa bungeni na zinaweza kuthibitishwa na mtu yeyote kutokana na Taarifa ya Benki Kuu ya Mwaka 2005/06 iliyosambazwa kwa umma," inasema taarifa hiyo ya serikali.
Na wao wenye 'nia njema' wakamshikilia Liyumba na mpaka sasa anahenya Keko!

SERIKALI imesema mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa masilahi ya taifa ikilinganisha na mikataba ya zamani ya madini, na kutaja faida za mradi huo wa uchimbaji dhahabu. Kutokana na hali hiyo, Serikali imesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwa katika kusaini mkataba wa Buzwagi, sheria na taratibu za nchi zilikiukwa, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma.

Taarifa ya Serikali iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wa hapa nchini na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini. Serikali ilieleza kuwa wataalamu waliohusika katika mchakato wa majadiliano ya mkataba huo na Kamati ya Ushauri ya madini iliyoupitisha, wote ni wazalendo na wakati wote walihakikisha masilahi ya nchi yanawekwa mbele.

"Kulinganisha na mikataba mingine iliyotangulia, mkataba huo wa Buzwagi unavyo vipengele vilivyoboreshwa zaidi," ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Vipengele ambavyo vimetajwa na serikali kuwa vimeboreshwa ni kupungua kwa asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na asilimia 50 miaka inayofuata; Kodi za zuio kwa kazi za kitaalamu kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi kufikia asilimia tano.
Kuna upuuzi mwingine watanzania hamtakiwi kunyweshwa mkanywa kama unavyokuja...

Hebu pata nakala ya mkataba wa Buzwagi hapa JF na uone ambacho serikali yetu 'tukufu' ambayo 'haijaishiwa' tena 'yenye nia njema' inachokitetea:

 
duh! hii ndiyo Serikali ya Mhe. Kikwete! nchi hii bwana, tunashinda sana, integrity ya Serikali zero.
 
Back
Top Bottom