Majibu kwa Lord Denning kuhusu tamko la TEC juu ya mkataba wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai

Majibu kwa Lord Denning kuhusu tamko la TEC juu ya mkataba wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai

View: https://youtu.be/R1zyTINo6kQ

Rafiki yetu Lord Denning ameuliza maswali kadhaa kuhusu tamko la TEC kwenye uzi unaopatikana HAPA. Nasi kwa hapa chini tumeamua kumjibu point counter point.

1. Lord Denning ameuliza: Wanadai Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo. Je, ni jambo lipi nchi hii limewahi kukubaliwa na asilimia 100 ya wananchi wote? Kwenye Mfumo wa vyama vingi, Mbona asilimia kubwa ya Wananchi walikataa mfumo huo ila Serikali wakauunga mkono? Je kwa nini hawakutoa tamko kipindi hicho kutaka nchi iendelee kuwa ya Chama kimoja? Kwa tamko lao walilosema maamuzi ya wananchi yaheshimiwe basi wanataka Serikali ifute maamuzi yake ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja?

Jawabu: Kaulimbiu ya tamko la TEC ni "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kwamba "Sauti ya watu (wote wakiwemo vichaa) ni sauti ya Mungu." Kanuni ya "mental reservation" iko kazini hapa pia. Tulia sindano ikuingie.

2. Lord Denning ameuliza: Kwenye tamko lao TEC wanadai Mihimili ya dola iheshimiwe. Juzi Mahakama Kuu wametoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya watu walioshtaki mkataba wa Bandari. Sasa kwa nini wanataka mihimili ya dola iheshimiwe na wao hawataki kuheshimu maamuzi ya Mahakama? Kama Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hasa ibara ya 107A, inasema Mahakama ndio Mhimili wa mwisho katika kutoa haki sasa kwa nini hawaheshimu maamuzi ya Mahakama halafu wanatoa tamko kusema Mihimili ya dola iheshimiwe?

Jawabu: Walichosema TEC ni kwamba Bunge na Mahakama ni mihimili inayofanya kazi chini ya shinikizo la Ikulu. Rais amekuwa mfalme anayedhalilisha Bunge na Mahakama. Uhuni uliofanywa na Bunge wakati wa kuidhinisha mkataba wa bandari ni uthibitisho. Hukummu ya Kesi ya Mahakama Kuu Mbeya ni ushahidi tosha. "Ukipinga mkataba wa bandari unampinga Mama," ndio kaulibiu iliyo ushahidi tosha.

3. Lord Denning ameuliza: Wao TEC ya Wakristo wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari; kesho BAKWATA ya Waislamu wanaweza kutoa tamko; na Kesho kutwa Mabuda wanaweza kutoa tamko. Je, wanataka Serikali imsikilize nani katika suala la mkataba wa Bandari?

Jawabu: Kaulimbiu ya tamko la TEC ni "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu (wa watu wote)." Hawajasema kwamba "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu (wa watu ambao ni Wakristo)." Kanuni ya "mental reservation" iko kazini hapa pia. Tulia sindano ikuingie.

4. Lord Denning ameuliza: Kwa hali hii tukiaamini kwamba ilikuwa sawa kwa mapadre wa kanisa katoliki waliohamasisha mauaji ya kimbari Rwanda kushitakiwa tutakuwa tuekosea?

Jawabu: Ni kichaa pekee anayeweza kuamini na kukubali hoja ya Lord Denning ifuatayo: Baadhi ya mapadre katoliki walihamasisha mauaji huko Rwanda. MMapadre Katoliki ni Wakristo. Kwa hiyo, Wakristo wote sio waadilifu.

Kwa ufupi, TEC wamekataa Watanzania kuendelea kusokomezwa chini ya utumwa wa wawekezaji wa kigeni, na hasa Waarabu wa Dubai ambao ni makuwadi wa ukoloni wa kilowezi!

Dawati la Mama Amon,
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga.

View attachment 2720874

Umetusaidia sana kumjibu kesho tukutaane hapa kahama kanisani
 
Attachments

  • Screenshot_20230819-225817_Chrome.jpg
    Screenshot_20230819-225817_Chrome.jpg
    172.4 KB · Views: 2
Unajua kwanini walitaka kubaki kwenye Chama kimoja! Eniwei Tanzania enzi hizo haukuwa na wasomi wengi hasa katika elimu ya uraia na waliamini sana kwamba kama itatokea Kukawa nna vyama vingi hasa vyama vya mageuzi (Kama Walivyoviita enzi hizo) Zitaleta Uvunjifu wa Amani na kutatokea Vita kwani Kutakuwa na ubishani kati ya vyam na vyama (KWA HYO LILIKUWA NI MATTER OF FEAR NA ELIMU TU) So ilibdi kuelimishwa kwa kupitisha ili wauone mfumo mzima unavyofanya kazi na KWA TAARIFA WALIUPENDA NA ndio maana uliamuliwaa kuwa mfumo wa uchaguzi mwaka 95' kama unayo elimu ya uraia lakini
Kwani kwenye hili jambo issue sio suala la ELIMU tu?

Wewe unaamini kama maaskofu wanaweza kutafsiri kipengele kilichosema land rights in accordance with the law kuwa tunawamilikisha au tunawapa ardhi yetu?? Sheria zetu zinaruhusu mgeni kumilikishwa ardhi? Au kupewa ardhi kwa shughuli za uwekezaji tu??

Kama hoja kipindi hicho ilikuwa elimu kwa nini hoja hiyo isiwepo saivi? Au wanapotosha kwa makusudi?
 
Hadi hapo umeshakosea!

Kwenye tamko lao hawajasema sauti ya watu wengi wenye akili. Wamesema sauti ya watu ni sauti ya Mungu!

Hivyo ni sawa tukirudi kwenye mfumo wa Chama kimoja kwa kuwa mwaka 1992 watu wengi walitaka tubaki na chama kimoja na Maaskofu wamesema Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.

Pia how comes hawakutoa tamko mwaka 1992 wakati Serikali imefanya uamuzi against matakwa ya watu wengi waliotaka tubaki kwenye mfumo wa chama kimoja? Tena kwa takwimu kabisa?
Hahaaaaa... Lord Denning

Mama Amon amekusaidia tu ili ulinde heshma yako ndogo iliyobaki. Maake wewe walau unaweza hata kuuliza maswali.

Pitia tena Hoja 8 za mapungufu ya mkataba zilizoko kwenye Tamko la Maaskofu.
 
Mama Amon aka Rabon hajaweza kujibu hoja zangu hata moja. Nimemuuliza swali kakimbia kabisa
 
Mama Amon aka Rabon hajaweza kujibu hoja zangu hata moja. Nimemuuliza swali kakimbia kabisa
Hudhuria tu Ibada ya kanisa lolote kesho la Katoliki na Muulize muumini yeyote baada ya hili Tangazo kusomwa, halafu jioni ulete mrejesho. Dini yetu adhini inasema itafute ilmu hata uchina
 
Hudhuria tu Ibada ya kanisa lolote kesho la Katoliki na Muulize muumini yeyote baada ya hili Tangazo kusomwa, halafu jioni ulete mrejesho. Dini yetu adhini inasema itafute ilmu hata uchina
Nakwambiaje huo waraka hata usomwe kwa miaka 5 mfululizo. Serikali haitoacha kamwe kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuangalia taasisi za kidini. Hilo haliwezi kutokea kamwe
 
Wewe unaamini kama maaskofu wanaweza kutafsiri kipengele kilichosema land rights in accordance with the law kuwa tunawamilikisha au tunawapa ardhi yetu?? Sheria zetu zinaruhusu mgeni kumilikishwa ardhi? Au kupewa ardhi kwa shughuli za uwekezaji tu??

Kama hoja kipindi hicho ilikuwa elimu kwa nini hoja hiyo isiwepo saivi? Au wanapotosha kwa makusudi?

Mi nafikiri Ndugu yangu cha kwanza kabisa Unahitaji kupata Muda kuusoma vizuri kabisa huu mkataba wa IGA ili upate vizur Mwanga Ni Mkataba mzuri sana ila una vipengele vichache ambavyo ukivitilia mkazo kisheria vina maana kubwa sana....

Na kuhusu kuwatilia Shaka Maaskofu Japo sio mkatoliki ila nawajua sana hao watu wamesoma proffesional mbalimbali na wengi wao ni Ma PhD holder na Maproffesor akiwemo katibu wa baraza hilo ambaye ni Mhadhiri aliwahi pia kufundisha SAUT mwanza na ni MBOBEZI WA Sheria hivyo kuhusu taaluma yao kama ulivyouliza sina shaka nao..

Ila shaka kubwa ni kwako kuwa umeusoma kweli mkataba huu?

Nia ya Serikali ni Nia nzuri sana ya kutafuta Wawekezaji ili tuapate nafuu ya kiuchumi na nilifurahi walipokaribisha maoni mbalimbali Na yawasilishwe kwa staha kama walivyosema (Ili lilitupa moyo wengi angalau kuchangia bila kuvunjaa sheria)

Sasa nirudi kwenye mada uliyouliza umeuliza kuhusu Ardhi me ntakuongeza na na swali jingine unalopenda kusema kuwa mahakama imeshaamua vipi anasema waheshimu Miamala?

Naanza kujibu kuwa unahitaji kusoma baadh ya sheria chache tu kama

Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, 2017 (No. 5 of 2017) na angalau katiba ya nchi soma pia Sheria ya Ardhi halafu soma pamoja na Mkataba wa IGA UTAPATA MWANGA FULANI...
Kuhusu mahakama maana umeliruudia zaidi ya mara kumi...naomba upitia pia hukumu hiyo Ya kesi ya 5 ya mwaka 2023 utaelewa zaidi...

Kimantiki WALIOSHINDA ni WALALAMIKAJI kwani Mahakama Kuu imekiri Mkataba wa IGA una mapungufu kadhaa;

1. Umevunja Sheria za Natural Wealth and Resources, Sura za 449 na 450 za 2017 ambazo zimekataza Migogoro juu ya uwekezaji kwenye rasilimali isipelekwe Nje ya Nchi na isitumie sheria za nje kutatua Migogoro hiyo.
IGA imesema Migogoro itatatuliwa Afrika Kusini na sheria za Uingereza ndizo zitatumika.,

2. Mahakama imekiri Tangazo la Bunge la saa 23 kualika maoni ya Wananchi ulikuwa ni muda mfupi sana na kwamba inaondoa mantiki ya Public Constitution.[consultation]

3. Mahakama imekiri pia Dubai haina Legal Personality katika Sheria za Kimataifa (Montevideo Convention na Vienna Convention) kwani inakosa Sovereignty

4.Mahakama ilishangaa inakuwaje Mkataba wa IGA umekosa ukomo wa muda wake.

5. Pia Mahakama imekiri kwamba kitendo cha IGA kusema haitawezekana kujitoa hata kama kuna Uvunjifu mkubwa wa Masharti yake, kwamba ni dosari kubwa na kwamba inakiuka hata Vienna Convention ambayo Serikali ilijikita sana kuutumia kama rejea kujenga hoja kwamba IGA ni International agreement.

Sasa

naomba uende kwenye Utangulizi wa Natural Wealth and Resources, Sura 5 ya 2017 katika paragraph ya 1 na 2 Paragraph ya 1: inahusu msingi mkuu wa malengo na maelekezo ya kisera katika ibara ndogo ya 1 ya sura 5 na ibara ya 9(f) ya Katiba ya Tanzania inatambua mamlaka ya umma. Na kupitia umma huo, serikali itapata nguvu na mamlaka kutoka kwa watu na huku msingi mkuu ikiwa ustawi wa watu. Na paragraph ya 2 inaeleza kwamba; sheria za kimataifa zinatambua haki yetu ya jamhuri katika permanent sovereignty ya kufaidi, kutumia maliasili yake.

Sasa DP WORD ITAINYIMA SIO TU SERKALI KUTUMIA SOVEREIGNTY BALI HATA KUPUNGUZA PRESIDENTIAL POWER

Hayo ni maoni machache yangu naomba tusijengeane chuki kwenye kutofautiana..
Sometimes its bettr to Agree to be disagreed to each other "Wakati mwingine Ni boraa kukubali kutokukubaliana...." Inakuza democrasia na undugu...
 
Nakwambiaje huo waraka hata usomwe kwa miaka 5 mfululizo. Serikali haitoacha kamwe kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuangalia taasisi za kidini. Hilo haliwezi kutokea kamwe
Sawa, waraka hauizuii serikali kuendeleea na jambo lake. Lakini pia kanisa kama kanisa limeonesha msimamo wake, msimamo huu utahulumiwa mbele. Masuala ya kiimani sio ya muda mfupi, na nimesema asbh, WARAKA WA MAASKOFU NI AGIZO LA KIROHO KWA WAUMINI WAKE. wako watakao pokea na wako watakaolikataa, lkn haya yote lazima yakae pamoja. Kwenye panasemwa viache MAGUGU NA NGANO VIENDELEE KUWEPO HADI WAKATI WA MAVUNO.
tutaona mbeleni. Sambaza waraka, usiwe na roho mbaya
 
Waweke msimamo kwenye namna maaskofu wanavyokula fedha za wizi kama zile za escrow.
 
Waweke msimamo kwenye namna maaskofu wanavyokula fedha za wizi kama zile za escro
Mtskatifu Lord Dening, tumalize hili la Bandari, mbona unahama hama ? Kwani mnaiiuza wapi Tz kiasi cha kuwa na haraka hivi
 
Mtskatifu Lord Dening, tumalize hili la Bandari, mbona unahama hama ? Kwani mnaiiuza wapi Tz kiasi cha kuwa na haraka hivi
Tanzania imeuzwaje? Nipe uthibitisho wa huo uuzwaji ndugu?
 
Kwenye tamko lao hawajasema sauti ya watu wengi wenye akili. Wamesema sauti ya watu ni sauti ya Mungu!

Hata hUjaelewa jawabu langu. Neno "watu" lina maana nyingi. Laweza maanisha watu wengi, watu wachache, watu wote, watu wenye akili timamu, watu vichaa, watu wala rushwa. Nimekuonyesha maana iliyokusudiwa na TEC. Huu utaratibu wa kuwasiliana kwa kuweka akiba ya mawazo unaitwa MENTAL RESERVATION. Hilo nalo gumu kueleweka?
 
Hata hUjaelewa jawabu langu. Neno "watu" lina maana nyingi. Laweza maani watu wengi, watu wachache, watu wote, watu wenye akili timamu, watu vichaa, watu wala rushwa. Nimekuonyesha maana iliyokusudiwa na TEC. Huu utaratibu wa kuwasiliana unaitwa MENTAL RESERVATION. Hilo nalo gumu kueleweka?
Kwa maana hiyo hata sisi tunaounga mkono uwekezaji sauti yetu ni sauti ya Mungu sio?
 
Kwa maana hiyo hata sisi tunaounga mkono uwekezaji sauti yetu ni sauti ya Mungu sio?

TEC wanaongelea watu wengi wenye akili timamu.
Nyie na wahariri waliokwenda Dubai mmepokea milioni 20 kila mtu ili kuharibu ukweli
Nyie wala rushwa.
Sauti yenu haiwezi kuwakilisha sauti ya Mungu
 
TEC wanaongelea watu wengi wenye akili timamu.
Nyie na wahariri waliokwenda Dubai mmepokea milioni 20 kila mtu ili kuharibu ukweli
Nyie wala rushwa.
Sauti yenu haiwezi kuwakilisha sauti ya Mungu
Wangesema basi kwenye waraka wao kuwa sauti ya watu wenye akili
 
Back
Top Bottom