Majibu kwa Lord Denning kuhusu tamko la TEC juu ya mkataba wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai

Umetusaidia sana kumjibu kesho tukutaane hapa kahama kanisani
 

Attachments

  • Screenshot_20230819-225817_Chrome.jpg
    172.4 KB · Views: 2
Kwani kwenye hili jambo issue sio suala la ELIMU tu?

Wewe unaamini kama maaskofu wanaweza kutafsiri kipengele kilichosema land rights in accordance with the law kuwa tunawamilikisha au tunawapa ardhi yetu?? Sheria zetu zinaruhusu mgeni kumilikishwa ardhi? Au kupewa ardhi kwa shughuli za uwekezaji tu??

Kama hoja kipindi hicho ilikuwa elimu kwa nini hoja hiyo isiwepo saivi? Au wanapotosha kwa makusudi?
 
Hahaaaaa... Lord Denning

Mama Amon amekusaidia tu ili ulinde heshma yako ndogo iliyobaki. Maake wewe walau unaweza hata kuuliza maswali.

Pitia tena Hoja 8 za mapungufu ya mkataba zilizoko kwenye Tamko la Maaskofu.
 
Hahaaaaa... Lord Denning

Mama Amon amekusaidia tu ili ulinde heshma yako ndogo iliyobaki. Maake wewe walau unaweza hata kuuliza maswali.

Pitia tena Hoja 8 za mapungufu ya mkataba zilizoko kwenye Tamko la Maaskofu.
Mama Amon aka Rabon hajaweza kujibu hoja zangu hata moja. Nimemuuliza swali kakimbia kabisa
 
Mama Amon aka Rabon hajaweza kujibu hoja zangu hata moja. Nimemuuliza swali kakimbia kabisa
Hudhuria tu Ibada ya kanisa lolote kesho la Katoliki na Muulize muumini yeyote baada ya hili Tangazo kusomwa, halafu jioni ulete mrejesho. Dini yetu adhini inasema itafute ilmu hata uchina
 
Hudhuria tu Ibada ya kanisa lolote kesho la Katoliki na Muulize muumini yeyote baada ya hili Tangazo kusomwa, halafu jioni ulete mrejesho. Dini yetu adhini inasema itafute ilmu hata uchina
Nakwambiaje huo waraka hata usomwe kwa miaka 5 mfululizo. Serikali haitoacha kamwe kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuangalia taasisi za kidini. Hilo haliwezi kutokea kamwe
 

Mi nafikiri Ndugu yangu cha kwanza kabisa Unahitaji kupata Muda kuusoma vizuri kabisa huu mkataba wa IGA ili upate vizur Mwanga Ni Mkataba mzuri sana ila una vipengele vichache ambavyo ukivitilia mkazo kisheria vina maana kubwa sana....

Na kuhusu kuwatilia Shaka Maaskofu Japo sio mkatoliki ila nawajua sana hao watu wamesoma proffesional mbalimbali na wengi wao ni Ma PhD holder na Maproffesor akiwemo katibu wa baraza hilo ambaye ni Mhadhiri aliwahi pia kufundisha SAUT mwanza na ni MBOBEZI WA Sheria hivyo kuhusu taaluma yao kama ulivyouliza sina shaka nao..

Ila shaka kubwa ni kwako kuwa umeusoma kweli mkataba huu?

Nia ya Serikali ni Nia nzuri sana ya kutafuta Wawekezaji ili tuapate nafuu ya kiuchumi na nilifurahi walipokaribisha maoni mbalimbali Na yawasilishwe kwa staha kama walivyosema (Ili lilitupa moyo wengi angalau kuchangia bila kuvunjaa sheria)

Sasa nirudi kwenye mada uliyouliza umeuliza kuhusu Ardhi me ntakuongeza na na swali jingine unalopenda kusema kuwa mahakama imeshaamua vipi anasema waheshimu Miamala?

Naanza kujibu kuwa unahitaji kusoma baadh ya sheria chache tu kama

Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, 2017 (No. 5 of 2017) na angalau katiba ya nchi soma pia Sheria ya Ardhi halafu soma pamoja na Mkataba wa IGA UTAPATA MWANGA FULANI...
Kuhusu mahakama maana umeliruudia zaidi ya mara kumi...naomba upitia pia hukumu hiyo Ya kesi ya 5 ya mwaka 2023 utaelewa zaidi...

Kimantiki WALIOSHINDA ni WALALAMIKAJI kwani Mahakama Kuu imekiri Mkataba wa IGA una mapungufu kadhaa;

1. Umevunja Sheria za Natural Wealth and Resources, Sura za 449 na 450 za 2017 ambazo zimekataza Migogoro juu ya uwekezaji kwenye rasilimali isipelekwe Nje ya Nchi na isitumie sheria za nje kutatua Migogoro hiyo.
IGA imesema Migogoro itatatuliwa Afrika Kusini na sheria za Uingereza ndizo zitatumika.,

2. Mahakama imekiri Tangazo la Bunge la saa 23 kualika maoni ya Wananchi ulikuwa ni muda mfupi sana na kwamba inaondoa mantiki ya Public Constitution.[consultation]

3. Mahakama imekiri pia Dubai haina Legal Personality katika Sheria za Kimataifa (Montevideo Convention na Vienna Convention) kwani inakosa Sovereignty

4.Mahakama ilishangaa inakuwaje Mkataba wa IGA umekosa ukomo wa muda wake.

5. Pia Mahakama imekiri kwamba kitendo cha IGA kusema haitawezekana kujitoa hata kama kuna Uvunjifu mkubwa wa Masharti yake, kwamba ni dosari kubwa na kwamba inakiuka hata Vienna Convention ambayo Serikali ilijikita sana kuutumia kama rejea kujenga hoja kwamba IGA ni International agreement.

Sasa

naomba uende kwenye Utangulizi wa Natural Wealth and Resources, Sura 5 ya 2017 katika paragraph ya 1 na 2 Paragraph ya 1: inahusu msingi mkuu wa malengo na maelekezo ya kisera katika ibara ndogo ya 1 ya sura 5 na ibara ya 9(f) ya Katiba ya Tanzania inatambua mamlaka ya umma. Na kupitia umma huo, serikali itapata nguvu na mamlaka kutoka kwa watu na huku msingi mkuu ikiwa ustawi wa watu. Na paragraph ya 2 inaeleza kwamba; sheria za kimataifa zinatambua haki yetu ya jamhuri katika permanent sovereignty ya kufaidi, kutumia maliasili yake.

Sasa DP WORD ITAINYIMA SIO TU SERKALI KUTUMIA SOVEREIGNTY BALI HATA KUPUNGUZA PRESIDENTIAL POWER

Hayo ni maoni machache yangu naomba tusijengeane chuki kwenye kutofautiana..
Sometimes its bettr to Agree to be disagreed to each other "Wakati mwingine Ni boraa kukubali kutokukubaliana...." Inakuza democrasia na undugu...
 
Nakwambiaje huo waraka hata usomwe kwa miaka 5 mfululizo. Serikali haitoacha kamwe kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuangalia taasisi za kidini. Hilo haliwezi kutokea kamwe
Sawa, waraka hauizuii serikali kuendeleea na jambo lake. Lakini pia kanisa kama kanisa limeonesha msimamo wake, msimamo huu utahulumiwa mbele. Masuala ya kiimani sio ya muda mfupi, na nimesema asbh, WARAKA WA MAASKOFU NI AGIZO LA KIROHO KWA WAUMINI WAKE. wako watakao pokea na wako watakaolikataa, lkn haya yote lazima yakae pamoja. Kwenye panasemwa viache MAGUGU NA NGANO VIENDELEE KUWEPO HADI WAKATI WA MAVUNO.
tutaona mbeleni. Sambaza waraka, usiwe na roho mbaya
 
Waweke msimamo kwenye namna maaskofu wanavyokula fedha za wizi kama zile za escrow.
 
Waweke msimamo kwenye namna maaskofu wanavyokula fedha za wizi kama zile za escro
Mtskatifu Lord Dening, tumalize hili la Bandari, mbona unahama hama ? Kwani mnaiiuza wapi Tz kiasi cha kuwa na haraka hivi
 
Mtskatifu Lord Dening, tumalize hili la Bandari, mbona unahama hama ? Kwani mnaiiuza wapi Tz kiasi cha kuwa na haraka hivi
Tanzania imeuzwaje? Nipe uthibitisho wa huo uuzwaji ndugu?
 
Kwenye tamko lao hawajasema sauti ya watu wengi wenye akili. Wamesema sauti ya watu ni sauti ya Mungu!

Hata hUjaelewa jawabu langu. Neno "watu" lina maana nyingi. Laweza maanisha watu wengi, watu wachache, watu wote, watu wenye akili timamu, watu vichaa, watu wala rushwa. Nimekuonyesha maana iliyokusudiwa na TEC. Huu utaratibu wa kuwasiliana kwa kuweka akiba ya mawazo unaitwa MENTAL RESERVATION. Hilo nalo gumu kueleweka?
 
Kwa maana hiyo hata sisi tunaounga mkono uwekezaji sauti yetu ni sauti ya Mungu sio?
 
Kwa maana hiyo hata sisi tunaounga mkono uwekezaji sauti yetu ni sauti ya Mungu sio?

TEC wanaongelea watu wengi wenye akili timamu.
Nyie na wahariri waliokwenda Dubai mmepokea milioni 20 kila mtu ili kuharibu ukweli
Nyie wala rushwa.
Sauti yenu haiwezi kuwakilisha sauti ya Mungu
 
TEC wanaongelea watu wengi wenye akili timamu.
Nyie na wahariri waliokwenda Dubai mmepokea milioni 20 kila mtu ili kuharibu ukweli
Nyie wala rushwa.
Sauti yenu haiwezi kuwakilisha sauti ya Mungu
Wangesema basi kwenye waraka wao kuwa sauti ya watu wenye akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…