Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Tafaadhali wana JF kuweni na subira msiporomoshe matusi kwa mleta mada, wa kulaumiwa ni serikali huyu ni zao la kusoma bila mtaala, muulizeni maswali magumu awape majibu mepesi,
Swali langu kwa mleta uzi ni kuwa anamfahamu vipi mnyika?
 
hakuna anaweza kumfikia kwani ukiona mbunge aliyeaminiwa na watanzania wakampa dhamana ya kuwaongoza kwa muda wa miaka mitano alafu anaongozwa na mbunge mwenzake ili afanye anavyotaka pata mashaka na mbunge huyo
 
Composed, poised, and polished!

Dogo wa Kikwete na Nape sidhani kama wanaweza kuandika kama alivyoandika Mnyika hapa!

mkuu ingekuwa nape na rizione walisoma huku wanafanya harakati kama za mnyika hakika matokeo yao yangekuwa zaidi ya keep left hivi tu walikuwa full time ila ndo magumashi plus!
 
Nchi zote zilizoendelea Duniani, ukiomba kazi wanakuambia tutumie CV yako siyo cheti cha kuhitimu masomo. Hapa kwetu watu wamejaa kasumba za kijinga wakidhania cheti cha masomo ndiyo chenye kudhihirisha uwezo wake.

Angalia watu kama akina Kigwangala, ni watu hopeless kabisa lakini wana vyeti vya kuhitimu udaktari. Ukimwuliza aliwahi kufanya kazi wapi, hakuna popote alipowahi kufanya kazi zaidi ya internship. Mtu wa namna hiyo uwezo wake wa kutibu mgonjwa unazidiwa na Clinical Officer anayeitumika fani yake.

Sasa hivi bungeni wamejaa madaktari wa vyeti kibao lakini fikra ni zero. Serikali tuna maprofesa kama akina Jumanne Maghembe ambao uwezo wao wa kuchambua na kutenda mambo haona tofauti na akina Majimarefu.

Ongera Myika kwa kuweka wazi, wananchi tumekuchagua sio kwa shahada bali uwezo ulionao. Kwa jinsi unavyochangia bungeni na unavyoendesha siasa unajitofautisha na wasomi vyeti. Siku moja tulimuuliza Mtikila pale SUA kuhusu elimu na majibu yake alisema yeye ahamini katika vikaratasi bali utendaji wa mtu. Chadema songa mbele ,tumeingia sebureni kwao wamelimbilia chumbani -tunawafata hukohuko
 
habari zilizoenea mitaani ni kuwa nape alipata division 0 mtihani wa kidato cha 6, mwenye uhakika au yeye mwenyewe atuhakikishie. Na aeleze aliwezaje kwenda chuo kikuu baada ya kupata division 0 mithani wa kidato cha 6.

mature age entry ;
unaonyesha cheti cha form 4 ; uwe na c -5
umekaa mtaani miaka 5
 
Habari zilizoenea mitaani ni kuwa Nape alipata Division 0 mtihani wa Kidato cha 6, mwenye uhakika au yeye mwenyewe atuhakikishie. Na aeleze aliwezaje kwenda Chuo Kikuu baada ya kupata Division 0 mithani wa kidato cha 6.

Haya Mkuu Nape Nnauye unaombwa kutolea ufafanuzi hoja hapo juu ikiambatana na ushahidi thabiti. Please, be straight and to the point. Na kama tuhuma husika ni za kweli, tafadhali fafanua uliingia Chuo kwa vigezo vipi vya kitaaluma potelea mbali sponsorship ambayo inawezekana ulilipiwa na wazazi au jamaa zako na sio na Serikali ambayo imeweka bayana kiwango cha ufaulu ili kupata sponsorship.

Mkuu tuko online tunasubiri majibu.
 
Last edited by a moderator:
a ngapi? thubutu, hizo a za mitihani ya kufanyiwa na mapadre seminari maua sawa. chezea a level wewe kwa wale wanafunzi mayai toka shule za private.

eti daraja la pili hahaaaa haaaa wiiiiiiiii wanasiasa waongo. daraja la pili angechaguliwa chuo kuendelea na masomo.

mbona zitto kitila walikuwa wanasoma na kufanya mambo ya siasa.

hadanganywi mtu na maelezo marefu kama biblia.

wanasiasa waongooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

ya form six yalikuwaje? A+ ngapi mh.mbunge?
 
Siasa bana, mtu ana A tisa 4M4 tena enzi hizo alafu mnadhani mtalingana upeo!

Form six div 2 Chuo kasoma Udsm hadi mwaka wa tatu then kutopewa yale makaratasi kushushe miaka aliyopoteza pale bila kufeli!

Magamba mnajiumbua tu! soon tutaleta mlolongo woooooote wa elimu ya nape mjione hizi elimu za vyeti zilivyo!
 
"Nape Nnauye na Ridhiwani Huwa hatupendi kujadili trivial Issues lakini hapa wacha tuseme.Siasa za majitaka anazoeneza Nape nnauye juu ya CHADEMA na viongozi wake hazitoi taswira njema kwa vijana.Nimeshangaa kuona anahoji juu ya Elimu ya Mnyika huku akijua kwamba kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na Elimu na kuwa na vyeti.Kipimo cha Elimu ni performance.Mnyika ameweka Rekodi ya kuwa mbunge bora kwa mujibu wa tovuti ya bunge kwa mwaka 2012 akiwafunika wabunge wenye Ph.D na wengine ni Maprofesa

Sijui Nape anatoa wapi Termerity ya kuhoji Elimu za watu huku akijua kwamba yeye alikuja India Mwaka 2005 kusomeshwa na chama chake huku wakitumia nguvu kubwa ya ubalozi kupata admission kule acharya University kwenye Course ya journalism.Ni nani asiyejua kule Acharya ulikua unafanyiwa assignment na baadhi ya wanafunzi ulipokua unakimbilia Tanzania kwa ajili ya Siasa? Sitaki kuwaita classmates wako wa journalism hapa ,watakuvua nguo.Njoo useme ripoti ya ziara ya kitaaluma ya Mwezi April/May 2006 iliyofanyika Jimbo la Kerala ni nani alikuandikia?

Sikutegemea Ridhiwani naye adandie hoja hii kwa ushabiki uliopitiliza.Maanake tunaweza kumwambia alete Tasnifu yake (thesis) ya Shahada ya Uzamili katika sheria-LLM kule Hulls University .Hataweza kuileta.Tuanweza tukaanza kujadili pia kigezo chake cha kufanya kazi IMMA Advocates maana tunajua IMMA Advocates alikofanya practice mmojawapo wa wakurugenzi wake Lawrence Masha alikuja kuteuliwa kuwa Waziri kwenye serikali ya Baba yake Ridhiwani ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM kilichomsomesha Nape Nnauye na kutumia nguvu nyini kupita ubalozi kuhakikisha anapata udahili

Hii kasi ya kudandia aliyoonyesha Ridhiwani inamfanya asahau mambo ya msingi maana kama tungekua tunahoji Elimu na vyeti amesahau kuwa kwenye kura za maoni za CCM mwaka 2005 mtu ambaye angefaa kuliko wote kwa vigezo hivyo basi ni Prof.Mark Mwandosya au Dr.Salim Ahmed Salim maana hawa wana CV zilizotukuka na wana nishani za kimataifa ukilinganisha na JK.Hawa wote walidhulumiwa kisaiasa kwa siasa za majitaka ambazo Ridhiwani kikwete na Nape wanaziendeleza.Kwanza Nape kabla hujajadili hili njoo utueleze Shahada yak ya Uzamili ya Mzumbe ni nani alikuandikia dissertation ambayo iliwasilishwa na Mwanasheri?Umesahau Wabunge na Mawaziri kutoka CCM ndiyo waliothibitishwa na TCU kwa kuwa na degree fake?Usijaribu kututoa kwenye ajenda za msingi.Tutawaaibisha

Tuache gutter politics tujadili namna ya kuboresha sera ya elimu maana leo hii wadogo zetu wanaumia sana kutokana na matokeo mabaya.Nashangaa hata wale waliosomeshwa nje tena vyuo Bora ndiyo wanaoendekeza siasa za majitaka.
The future of this country is being jeopadised by the intellectual slavery of our top leaders, politically, religiously and judiciously. From all indications, it becomes convincing that Tanzania can never never be good unless our leaders are delivered from intellectual cancer of greediness, self-centeredness and callousness."

https://www.facebook.com/ben.saanane?fref=ts
 
Kama kiongozi makini unahitaji kwanza uwe na uwezo wa kutafakari jambo, mbunge huyu uwa hatafakari bali anafuata kila anachoambiwa

1. hoja ya maji dar arijaribu kukopi na kupaste ya wizara ili ajiafutie umaarufu hii alifanya kwa kufuata mawazo baadhi ya wabunge cdm anaodhani kuwa wana uwezo zaidi yake
2. kauli anazotoa bungeni na nje ya bunge haziendani na mtu makini mwenye nia nzuri na watanzania kwa mambo hayo machate tu mbunge huyu upeo wake wa kufikiri bado mdogo sana

Fyata mkia unyamaze we ni kilaza kabisa, umesoma mpaka wap?
 
Vichaa wengine ndiyo hawa. Hawajui kuwa hata unapoomba kazi, format ya profile inaendana na kazi unayoiomba. Hiyo format yako inakidhi vigezo kama unataka kuomba kazi ya kufundisha (if you want to become an academician). Sisi ambao tupo kwenye industry ya production, ukinitumia maombi ya kazi halafu profile yako ukaiweka kwa muundo huo, sipotezi hata muda, hata kwenye interview sikuiti.


Mimi nataka paragraphy yako ya kwanza, uniwekee:


Achievement ( I want to know if you can deliver, I pay you from what you produce not because of what you have in your head or the number of certificates you possess)

Mengine baadaye.

Acha bla bla jibu hoja kwa format hii;

Education
Include dates, majors, and details of degrees, training and certification
High School
University
Graduate School
Post-Doctoral Training

Professional Qualifications
Certifications and Accreditations
Computer Skills
Awards
Publications
Books
Professional Memberships
Interests
 
1. nikiongozi anaetafuta umaarufu bila kuumiza kichwa chake kama alivofanya juzi bungeni kwa kukopi kazi ya wizara na kudai ni yake na kuwaamisha watanzaia bila kujua watanzania wa sasa wameshajua hana uwezo
2. Ni kiongozi asiyependa kuwa mkweli kadisco chuo anataka waamin kuwa amehairisha mwaka mara ana elimu ya chuo kikuu
 
thread ya kipumbavu kabisa,unashambulia elimu ya mtu yako inakusaidia vipi?

Hawajitambui hawa.. Wanatumika maana cijaona kwenye siasa chama tawala badala ya kuzungumzia utekelezaji wa sera na ilani zake.. Wanawashambulia wapinzani tena kwa personal attacks..!
 
Kama kiongozi makini unahitaji kwanza uwe na uwezo wa kutafakari jambo, mbunge huyu uwa hatafakari bali anafuata kila anachoambiwa

1. hoja ya maji dar arijaribu kukopi na kupaste ya wizara ili ajiafutie umaarufu hii alifanya kwa kufuata mawazo baadhi ya wabunge cdm anaodhani kuwa wana uwezo zaidi yake
2. kauli anazotoa bungeni na nje ya bunge haziendani na mtu makini mwenye nia nzuri na watanzania kwa mambo hayo machate tu mbunge huyu upeo wake wa kufikiri bado mdogo sana
Tatizo ni uwezo wa watu wenye elimu ndogo kumwelewa mtu kama Mnyika. Watu wa ubungo wanajua anachokifanya kwani anashughulikia shida yao. Serikali imekua inafanya usanii kuhusu maji Dar-es-Salaam huku ikitoa tenda zenye kuwanufaisha viongozi bila kutatua shida ya maji jijini. Watu waliyoelimika kweli wanaliona hilo tatizo.
 
msipende kuamini hata ambalo haliwekani hana uwezo wa kupata dv 2 vip adisco chuo
 
Back
Top Bottom