Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Mheshimiwa Mnyika, unaweza kuwaza sana ukaona kuwa huenda Mungu alikuwa na sababu usipate elimu ya moja kwa moja. Elimu yako iwe na vituo, ili utumike kuletea Taifa lako mabadiliko yanayostahili. Ungeweza kusoma sana ukashawishika na cheo cha CCM. Na kwa kuwa usingefanana na mafisadi ungeweza kupoteza maisha. Nakusifu kwa msimamo wako na ujasiri wako. Hakuna sababu hata kidogo ya labda kujisikia dhaifu mbele ya wenye madigirii hata kama matano, maana hawajaweza kulithibitishia Taifa faida ya hizo shahada. Ipo mifano mingi sana hapa duniani ya watu ambao hawakupata elimu ya chuo lakini wametenda mambo makubwa sana. Bill Gates ni mfano hai.

Na pia ufahamu kuwa kuchelewesha kwa Elimu hakubomoi daraja la kukufikisha uendako. Raisi maarufu sana wa Marekani Abraham Lincolin alikuwa house boy wa mwanasiasa, akawa anajisomea vitabu vya tajiri yake, mwishowe akajiunga na shule hadi chuo mpaka akaja kuwa Raisi maarufu sana wa Marekani. Ndiye raisi ambaye Mungu alimtumia kuleta yale mabadiliko muhimu sana katika historia ya utumwa Marekani. Usikatishwe tamaa na chochote, kaza buti songa mbele na mbele daima. Mungu akubariki.
 
Maelezo mengi lakini hayajafika mwisho kwa kutueleza kiwango cha juu cha elimu kilichofikiwa na mh. Mnyika. Kwa maana nyingine mh amejibu swali ambalo hajaulizwa halafu akaacha lile aliloulizwa
Wewe ndio Ridhiwani Kikwete? aliyejibiwa anasema amelizika halafu unatokea mwehu mwingine unaleta uharisho wako hapa? kuna vijana wengi sana mtaolewa nchi hii tukiruhusu ndoa za jinsia moja.
 
siwezi kuelezea jinsi mh.mnyika alivyo nikosha kwa maelezo yake mazuriii!ana jua haipingiki hata kidogo,amejibu kwa ufasaha mh. mbunge.Hongera sana kamanda maji walete sasa elimu si ndiohiyo?
 
Big up Mnyika, well said. Even if it is a waste of time and resources to deal with stupid minds (not ignorant minds), it may appear cost effective to provide clarifications to individuals sorrounding the mouths of stupid minds.

It is an invaluable information that you have provided. For me, so longer you have acquired the necessary skills to enable you excute and pursue your Godly driven purpose, that is more than essential. Even if you were to read just a single page, in a 10 minutes time, so longer you can use that knowledge to execute your purpose, it is more than enough. if you wsh to continue studying even at your retirement age, you can still do it.

Never spend additional time to respond to corrupt minds that holds their prides on certicates and not what they have stored as knowledge and skills in their minds.

For example what is the value of having Dr Kawamba (3 degrees) plus Professor Magembe (4 degrees) plus (professa Mwakyusa (4), Prof Mwandosya (4) = 15 degrees, and others, in the cabinet of ministers, if they cannot come up with even a single concrete plan to resolve water problem in a single constituent, like Ubungo or even come up with a plan to buy one desk in one secondary school????

Sorry, Mnyika, i feel like you have spent a lot of time responding to corrupt minds that should have been used to come up with constructive ideas in bring development to our country. Next time, where necessary just repond to 5 to 6 lines bas!
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM. Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam). Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa. Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita. Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno. Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo. Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi. Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree). Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo. Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu. Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi. Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu. Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani. Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita). Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa. Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?JJ
.."dio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge.." umenifurahisha tazana watu kama akina Sofia Simba+Abood mbunge wa moro na wengine lukuki tuuu wale wasemao mai deile bredi is injiniaringi....na tanzania imepata uhuru mwana 11961...
 
Kamanda Mnyika,kwa kuzingatia utumishi wako uliotukuka kwa wananchi wa Ubungo vyuo vifuatavyo vimeamua kukutunukia degree:
  • Modern commercial institute
  • English fountain
  • Njuweni
  • Chuo cha sanaa Bagamoyo
 
Mhe. Naona watakoma kuhoji tena aibu yao tandazeni vyeti au riz yatakuwa ya kama ya sister mwana anayesabisha mwaka no jina kamili kwenye ncta ya f4
 
Naamini Mungu alipitia kwa Yesu kuonesha uwezo wake,miaka hii atapitia kwa viongozi wa CHADEMA kutuonesha ukweli,peopooz
 
Kwani uongo mfumo wa kimarekani wana associate degree tena mtu anakuwa college yaani wewe kwa akili yako Mnyika kwa pass alizopata toka darasa la saba unataka aone aibu ndio maana tunasema vichwa vyenu vimejaa sisimizi kwa sababu munataka kutulazimisha tuamini kwamba kuna mahala alijikwenza kwa crendentials asizokuwa nazo

Aliysema uongo nani?! Wewe vipi!!!! Unaijua hiyo inayoitwa Associate Degree au unaongea tu!! Kwahiyo mtu akisoma miaka mitatu popote pale as far as hajafanya mtihani wa mwisho hapo ndo anakuwa amepata Associate Degree?! Yaani bado tu pamoja na kuandika pumba bado hujafahamu ni nani kati yetu kichwa chake kina sisimizi?! Ikiwa hata Associate Degree huifahamu, sijui tukuweke kundi gani!!!

halafu kusema Mnyika alipata pasi mzuri toka darasa la saba ni hoja ya kijuha! Na kama kigezo ni kufanya vizuri Darasa la saba na Form IV, kwetu sie ambao tunafanya analysis kwa graph kwa wepesi zaidi, basi graph ya Mnyika haivutii!
 
Aliysema uongo nani?! Wewe vipi!!!! Unaijua hiyo inayoitwa Associate Degree au unaongea tu!! Kwahiyo mtu akisoma miaka mitatu popote pale as far as hajafanya mtihani wa mwisho hapo ndo anakuwa amepata Associate Degree?! Yaani bado tu pamoja na kuandika pumba bado hujafahamu ni nani kati yetu kichwa chake kina sisimizi?! Ikiwa hata Associate Degree huifahamu, sijui tukuweke kundi gani!!!

halafu kusema Mnyika alipata pasi mzuri toka darasa la saba ni hoja ya kijuha! Na kama kigezo ni kufanya vizuri Darasa la saba na Form IV, kwetu sie ambao tunafanya analysis kwa graph kwa wepesi zaidi, basi graph ya Mnyika haivutii!

Umejibu nini sasa google utapata maana ya associate degree dunia hii kila kitu bwerere,humuwezi Mnyika wala hutamshusha hadhi unajisiliba kinyesi usoni huna la maana kawatandika fimbo mumebaki kujinyea nyea yaani mtu awe mwanafunzi bora Dar es salaam nzima na baadaye A 9 sekondari useme hutambui naona unaakili ya mbuzi si mzima weye
 
Mia ya Nape na Ridhiwani ni kututoa kwenye matatizo yaliyosababishwa na utawala mbovu wa baba yake maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ni ndoto
ameingiza nchi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Ametumia pato la taifa kwenda kubembea jamaica

Hapo ndipo ninapopata mashaka na uwezo wenu wa kuchambua mambo! Hivi ni nani basi anayepaswa kulaumiwa zaidi? Tuhuma dhidi ya Mnyika kuhusu elimu yake hazikuanza jana wala juzi! Sasa kwanini siku zote hizo amebaki kimya na anakuja kutoa ufafanuzi siku ya kutolewa kwa matokeo mabovu ya kidato cha nne? Watu wameacha kujadili matokeo ya kidato cha nne, na sasa wanajadili hoja ya Mnyika!! Sasa kama ni kulaumiwa ni kwanini asilaumiwe Mnyika ambae amekuja ku-divert hoja ya matokeo ya kidato cha nne?

Tukija upande wa pili.....wafuasi wake nanyi mmejazana hapa kutetea hoja ya Mnyika! Wengine wameanzisha THREAD mpya kutokana na thread hii hii! Sasa kama nyie ni werevu na mlifahamu lengo la Nape ni wenzake ni ku-diverge hoja za msingi; inakuwaje basi basi nanyi mnakuwa diverted kirahisi hivi?!

Kama ni kweli lengo la Nape na wenzake wametumia hoja ya elimu ya Mnyika ili ku-diverge hoja za msingi, basi hivi sasa wamemtumia Mnyika mwenyewe aje hapa ili a-diverge hoja ya matokeo mabovu ya kidato cha nne!
 
Umejibu nini sasa google utapata maana ya associate degree dunia hii kila kitu bwerere,humuwezi Mnyika wala hutamshusha hadhi unajisiliba kinyesi usoni huna la maana kawatandika fimbo mumebaki kujinyea nyea yaani mtu awe mwanafunzi bora Tanzania nzima A 9 sekondari useme hutambui naona unaakili ya mbuzi si mzima weye

Acha ushamba wewe, ya Mnyika sio Associate Degree.....! Google we mwenyewe coz' bado hufahamu what Associate Degree is! Mnyika ni kwamba HAJAMALIZA CHUO....yaani ama ame-postpone au ame-abscond! we vipi? By the way, more often than not, Associate Degree inakuwa ni miaka miwili especially kwa kozi kama aliyokuwa anasoma Mnyika!
 
Kamanda Mnyika,kwa kuzingatia utumishi wako uliotukuka kwa wananchi wa Ubungo vyuo vifuatavyo vimeamua kukutunukia degree:
  • Modern commercial institute
  • English fountain
  • Njuweni
  • Chuo cha sanaa Bagamoyo

Mbona hujataja The Amazon College pale NSSF Ubungo?! Pia kuna Zoom Polytechnic pale Magomeni Usalama!
 
Sifahamu na wala sitaki kufahamu juu ya elimu zao hao ridhiwani na nape lakini kwa tunavyowafahamu hata kama wangekuwa na daraja la uprofesa bado kamwe wasingeweza kukufikia hata kwa 1%.ni nani asiyeijua elimu ya bongo hasa kwa watoto wa wakubwa wengi wao vyeti tu na ma-cv kibao lakini kichwani....!!!!!.elimu yako inawakilisha elimu ya watanzania kibao(umeihangaikia mwenyewe),naamini huyo ridhiwani hiyo elimu yake na hata daraja alilonalo kuna nafasi ya mkono wa baba yake.usingejisumbua kuandika waraka wote huo wanakupotezea muda tu hao maana wajibu wako kwetu ni mkubwa mno zaidi yao.
 
Nawashaangaa wabongo maana mnapenda kubishana ka kuangalia fulani ana vyeti gani badala ya kuangalia fulani ana nini chenye faida kwa nchi, mbona wapo viongozi wengi tu na wazuri waliowahi kuwa juu ya ulimwengu na hawakuwa na hayo makaratasi ya vyeti mnayojisifu nayo..?
 
Hata Bill Gates, Mark zuckerberg,Larry Ellison na wengine wengi hawana vyeti na wamefika mbali sana kuliko wengi tulio na vyeti. Elimu ni ile inayokusaidia kuifaidisha jamii inayokuzunguka na sio vinginevyo. college droppers wengi huwa wanafanya vizuri
 
Mimi ninazo degree mbili, nimeajiri watanzania kibao na ninawalipa mwisho wa mwezi,,, lakini siwezi kukifanya kile ambacho Mh JJ Mnyika anafanya bungeni. This guy is genius, mtu kama huyu huwezi kumnunua kwa gharama yoyote. Nyie kaeni na maelimu yenu ya vyeti tu lakini hamna uwezo wa kufanya chochote bila kubebwa. Mnajikomba kwa maCCM kubembeleza mkate uende kinywani but this guy JJ is fight in his own grounds, his destiny is in himself, you you you your destiny is in Nape's hand

Great!!!
 
lengo la elimu ni suluhu ya matatizo
kama john mnyika tayari yeye ni suluhisho degree ya nini?
Maana tunawashuhudia wasomi wengi uku mtaani ni ma mburula wanadai wanazitumikia kazi kuliko jamii inayo mzunguka
nape acha ujinga ridhiwan ukitaka kuruka agana na nyonga ona sasa una kiri hadharani haukua sahihi shame on you
 
Acha kukurupuka wewe wapi amekwambia amehitimu chuo unaleta ushabiki wa kipuuzi hapa

Acha kukurupuka wewe wapi amekwambia amehitimu chuo unaleta ushabiki wa kipuuzi hapa

Gonga hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wengine-kuhusu-elimu-yangu-na-niliposoma.html

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Soma hapo, tatizo lenu maccm wavivu sana kusoma
 
Hongera JJ kwa CV nzuri....wanaotaka CV yako kielimu ni wazi kwamba wanashangazwa na utendaji wako uliojaa hekima na busara.. Wameshindwa kusoma plate namba...uko spidi ajabau. Keep it up!!!!!!
 
Back
Top Bottom