Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Muda unapotea kujadili A Tisa za mnyika...na yeye kutomaliza degree yake...? Hiyo degree akiamua ku carry credits Ana uwezo wa kuimaliza hata mwaka huu Akitaka....na ndani ya miaka mitano akaafanya kabisa na masters hadi phd......

Tungetumia Muda huu kujadili devision Zero ...260'000 ......ndani zikiwemo F za hesabu 300,000 na ushe na kati ya hizo F......160,000 wakipata Alama Kati ya 0 hadi 9 ......Matokeo mabaya kabisa kwenye historia ya Tanzania ( source NECTA )

93% ya watahiniwa wote wa Form 1V mwaka jana wamefeli! 93%! Sijui ni nchi gani ukanda huu ina viwango vya aina hiyo? Na jambo la kushangaza ni kwamba, kwa miaka 3 mfululizo matokeo yamekuwa ni mabaya.

Mwaka kesho itakuwaje kama tutawaachia watu wale wale waendelee kuongoza hii Wizara? Naibu waziri hajui hata Tanzania imetokana na nini?

Wale waliofeli mwaka jana na juzi wako wapi? Na hawa laki 3 na ushee wataenda wapi? Hapo kweli tunaweza kukwepa social unrest?
 
Ingekuwa vizuri kama ungekuwa unafanya research kabla ya kuropoka ili usipotoshe wenzio...mwaka 2004 Riz1 bado alikuwa darasani,na amemaliza 2005.. Uwakili hatufanyi mitihani kama unavyofikiria!!!bali ni oral interview;sasa cjui hao IMMa waliingia nae kwenye panel ile na kumsemea/kumjibia maswal kama unavyodanganya hapa???tuache ushabiki maandazi,haulipwi..utapiga domo wewe wenzio wanakula maisha..

Ridhiwani kilaza tu na niliyoeleza ni ukweli, kama kukosea ni miaka tu. Otehrwise suala la kuwa wakili, mpango mkubwa sana ulisukwa apite, oral, cunnilingus, haijalishi, yote yapo wazi pale IMMA. Na kuhusu kula maisha, hata sisi wengine twayala vizuri sana tu na hatuna wasiwasi na chama gani au nani atachukua uongozi wa nchi, sio wewe ambae nadhani ndiye mhusika uliyebadili ID ya kike kwa madhumuni ya kupambana na hoja za kweli kama hizi, kwani siku zenu zinahesabika, na jinsi miaka inavyozidi kwenda mbele, hali ni ya mguu ndani, mguu nje, ndio maana mnapanga safu yenu iende ikulu ikawalinde. tuombe uzima tu, ili tushuhudie uharamia wenu academically, kiuwakili, na kifisadi, hatima yake itakuwa ni nini.
 
Ridhiwani Kikwete, anaposema wataleta maji Katika jimbo la Ubungo anasema hivyo kama nani???. Ni upuuzi kudhani kwamba kuna kikundi au kundi fulani la kisiasa linaloweza kutatua kero za wananchi.. Ridhiwani hana nyazifa yoyote wala nafasi ya kujikamua na kusema 'TUTALETA' maji. Huu ni utamaduni uleule wa kujidhani kwamba kwa visababu fulani Mtu fulani ana 'UWEZO' wa kufanya hata yale yalio nje ya wajibu wake. Wananchi wenyewe ndio Kundi pekee litalojiletea maendeleo. Serikali inatakiwa tu kuratibu Mipango na kuwzesha shughuri za kujiletea maendeleo kwa kutumia Kodi inazokusanya.,,, WANANCHI WENYEWE KWA KODI ZAO WAKIONGOZWA NA SERIKALI YAO( kama inaweza kuwaongoza) WATAJILETEA MAENDELEO YAO...sio kundi au kikundi cha siasa kama CCM au CHADEMA.. Ridhiwani akome kufikiri namna hiyo.
 
Ridhiwani Kikwete, anaposema wataleta maji Katika jimbo la Ubungo anasema hivyo kama nani???. Ni upuuzi kudhani kwamba kuna kikundi au kundi fulani la kisiasa linaloweza kutatua kero za wananchi.. Ridhiwani hana nyazifa yoyote wala nafasi ya kujikamua na kusema 'TUTALETA' maji. Huu ni utamaduni uleule wa kujidhani kwamba kwa visababu fulani Mtu fulani ana 'UWEZO' wa kufanya hata yale yalio nje ya wajibu wake. Wananchi wenyewe ndio Kundi pekee litalojiletea maendeleo. Serikali inatakiwa tu kuratibu Mipango na kuwzesha shughuri za kujiletea maendeleo kwa kutumia Kodi inazokusanya.,,, WANANCHI WENYEWE KWA KODI ZAO WAKIONGOZWA NA SERIKALI YAO( kama inaweza kuwaongoza) WATAJILETEA MAENDELEO YAO...sio kundi au kikundi cha siasa kama CCM au CHADEMA.. Ridhiwani akome kufikiri namna hiyo.
Kijana Ridhiwani Kikwete ni uzao wa sultani Jakaya Kikwete. Mtoto wa Sultani ni Sultani ajaye. Asemalo ni Mamlaka imesema.
 
Last edited by a moderator:
Kwa walio wahi kupita shule (sekodari) wanaelewa inahitaji uwezo wa juu kiasi gani kupata A 9. Hii ni zaidi ya kipaji maalumu. Nachelea kusema mheshimiwa Mnyika ndiye Mbunge Pekee katika bunge la sasa aliyefaulu sekoari kuliko wote

A 9 kwenye mfumo wa elimu mbovu hata hizo A's zenyenye nazo zitakuwa ni mbovu. Nachagiza ujumbe wake wa kisiasa na mitazamo ya jamii tu.
 
Mia ya Nape na Ridhiwani ni kututoa kwenye matatizo yaliyosababishwa na utawala mbovu wa baba yake maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ni ndoto
ameingiza nchi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Ametumia pato la taifa kwenda kubembea jamaica
ameruhusu rafiki zake waarabu na Katibu wake mkuu kuvuna wanyama wetu kwa aslimia 60
Ameefirisi misitu kwa silimia 80 mpaka misitu kama sao hill imebaki historia
Anavuna madini ameruhusu mpaka uranium ivunwe wakati nchi haina uwezo kujikinga na madhara yake
asilimia 94.5 wanafunzi wa sekondari wamefeli
ameshindwa kutatua janga la njaa wananchi wanakufa vijijini
ameruhusu mauaji ya wana dini wote waislamu kwa wakristo
sasa elimu ya Mnyika itajibu haya au munatutoa kwenye mjadala wa kitaifa na siku zote munafanya hivyo tunawajua nyie

Usijali mkuu tunapiga kotekote mumo kwa mumo wanahisi wanatutoa kwenye mada kumbe tunakandamiza ndani kwa ndani, yaani uwezo wao wa kufikiri ni mdogo kuliko punje ya halidari
 
A 9 kwenye mfumo wa elimu mbovu hata hizo A zenyenye nazo zitakuwa ni mbovu. Nachagiza ujumbe wa kisiasa na mitazano ya jamii tu.

Hivi unazisikiaga hoja zake au unajiongelesha mkuu? Mfumo mbovu wa elimu unawaathiri vilaza wewe kama nikichwa nikichwa tuuu ndo maana anacheti cha form six na Maghembe ni prof lakini anamuhenyesha si unaona bunge lenu lakibaguzi lakini linatii amri kwa kichwa kama hiki? Mbona una ubovu wakufikiri tena wakati uko JF au umeathiriwa na mfumo mbovu
 
Hivi unazisikiaga hoja zake au unajiongelesha mkuu?

Kipi ni bora, kujiongelesha au kudandia comment ambayo haikuelekezwa kwako. Hoja zipi hizo zitakazo nifanya kuziona za ajabu.
Mfumo mbovu wa elimu unawaathiri vilaza wewe kama nikichwa nikichwa tuuu ndo maana anacheti cha form six na Maghembe ni prof lakini anamuhenyesha
Hili angalizo nila aina yake na ndiyo mara yangu ya kwanza kukumbana na kitu kama hii. Kilaza ndiyo yupi huyo Tanzania.

si unaona bunge lenu lakibaguzi lakini linatii amri kwa kichwa kama hiki? Mbona una ubovu wakufikiri tena wakati uko JF au umeathiriwa na mfumo mbovu

Bunge letu!!. Kwani wewe uko nchi gani hiyo. Hata kichaa naye ana uwezo wa kuona mwingine kichaa. Sishangai maneno yako.
 
Nape na Riz1 akili zao mbovu. Wanachofanya is to diverge attention of Tanznians kuhusu ubovu wa serikali. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuanza kujadili personalities badala ya kujadili masuala yanayolididimiza taifahili. Mfano

1. Kudidimia kwa elimu
2. Reli zetu kutofanya kazi vizuri
3. Udini unaotafuna umoja wetu
4. Viongozi wa serikali kutowajibika na kuwajibishwa kwa kutofanya kazi au kuharibu na kulitumbukiza taifa katika lindi la umaskini.
5. nk..........
Nape na Riz1 ni nzi tu, hata waikitwa nzi wa kizungu.
 
Tumpe Mhe. Mnyika honorary doctorate. Mnasemaje wanajamvi???
 
Sijuia nina mtazamo tofauti. Binafsi niwatake tuone kuwa haya yote yanatokea ili kuwathibitishia wale ambao bado hawaamini kuwa JK ni dhaifu na CCM ni puuzi. Naelewa adha na shida kubwa ya kijamii na hata kiuchumi kwa matokeo haya. Ila pia thisi is 'eye opener' na hili Jeshi kubwa lililofeli ni miongoni wa waleta mabadiliko. kinyume na hapo tutarajie mabaya zaidi.

93% ya watahiniwa wote wa Form 1V mwaka jana wamefeli! 93%! Sijui ni nchi gani ukanda huu ina viwango vya aina hiyo? Na jambo la kushangaza ni kwamba, kwa miaka 3 mfululizo matokeo yamekuwa ni mabaya.

Mwaka kesho itakuwaje kama tutawaachia watu wale wale waendelee kuongoza hii Wizara? Naibu waziri hajui hata Tanzania imetokana na nini?

Wale waliofeli mwaka jana na juzi wako wapi? Na hawa laki 3 na ushee wataenda wapi? Hapo kweli tunaweza kukwepa social unrest?
 
1. Shule ya msingi, John Mnyika alikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa darisalama. Akachaguliwa kwenda Ilboru lakini akaamua kwenda seminari. (Naachana na hili kwa kuwa ni swala la kiimani)

2. Form 4 akapata A masomo tisa. Katika mwaka ambao matokeo yalikuwa na mushkeli kwa uvujaji wa mitihani. Angeweza kwenda shule yoyote na mchepuo wowote. Akaamua kwenda Tambaza.

3. Form 6 akapata matokeo mazuri tuu (ambayo hayakuwekwa wazi kama matokeo ya form 4)

4. University akaamua kusoma evening classes. (Hakumaliza kwa sababu alizozitaja hapo juu)

Kwa wenye busara, mlolongo wa elimu wa huyu bwana unanuka samaki aliyechina. Mimi binafsi nimesoma Tanga school, wakati wa headmaster Tetti. Wakati sisi tuko O'level pale Tanga school alikuja mwarabu mmoja kujiunga form 5 (PCM) tulikuwa tunamwita "yarabi salama". Yarabi salama yeye wakati akiwa form 5 PCM alikuwa haelewi kwa nini namba ikitoka upande mmoja wa equation na kuvuka alama ya sawasawa na kuhamia upande mwingine mwingine, basi inabidi alama yake ibadilike, kama hasi itakuwa chanya na chanya huwa hasi. Form 5 PCM huyo. Na bwana yarabi salama alikuwa amepata alama A katika hesabu O level. Baadaye ikagundulika kwamba wakati wenzake wanafanya mitihani, yeye alikuwa anazaa mitihani.

Sijui kama msamiati wa kuzaa bado unatumika siku hizi, lakini kuzaa maana yake ni kwamba kuna watu wana networks na mitihani inapotoka na wanapoingia kwenye chumba cha mtihani, hawaji kufanya mtihani ispokuwa wanakuja na "booklet" zao ambazo maswali yanakuwa tayari yameshafanywa. Sasa wakati wenzao wanafanya mtihani wao wanaandika namba yao ya mtihani tuu kisha wanazaa.

a) Sasa, najiuliza. Mnyika amesema kwamba alikuwa wa kwanza mkoa wa darisalama. (Sibishi, lakina Sijui amejuaje)
b) amepata A tisa form IV; lakini hakusema amepata A ngapi form VI. Jee inawezekana ni kwa sababu matokeo yake ya form 6 hayashabihiani na yale ya form 4?
c) A tisa, lakini hakwenda Ilboru. Kwanini mwanafunzi hodari asiwe na hamu na shauku ya kusoma na wanafunzi hodari wengine? Jee inawezekana bwana Mnyika alikuwa anaogopa "to get found out?"
d) Baada ya kupata matokeo mazuri form 6; kwanini asome jioni? Jee alikuwa anaogopa kusoma na wanafunzi hodari?
e) Mpaka leo bado hana degree. [anisamehe kama nimekosea katika hili]. Ni kweli mwanafunzi mwenye uwezo wake wa kitaaluma atakubali kuishia njiani kwa namna aliyoishia yeye?

Sasa kila nikimtafiti huyu bwana Mnyika, samahani, lakini neno kuzaa linapiga kengere zote akilini mwangu. Nadhani huyu bwana ni miongoni mwa wale wenye bahati nzuri ambao huweza kuipata mitihani kabla ya siku ya mtihani.
 
maarifa binafsi yanahusika kuliko elimu ya darasani isitoshe vyeti vinatengenezwa tu kuna viongoz kbao wana degree na masters lakini majukumu wanayofanya ni kama wameishia la darasa la 7. Tunataka kazi sio malumbano ya kipuuzi
 
Haya Nape na wewe tuwekee matokeo ya elimu yako ya awali yaani Drs. la 7, Form IV, na Form VI hapa jamvini. Tuanzie hapo kwanza.

Vinginevyo tukisema huko vyuo vikuu uliingia kwa favour fulani tutakuwa hatukosei. Mnyika kwa matokeo yake anaweza kwenda chuo kikuu chochote dunani hata baada ya miaka 20 ijayo. Tunaomba grades zako tujiridhishe jinsi ulivyoingia Chuo. Hilo tu kwa sasa mheshimiwa.
Nape haraka lete hivyo vyeti vya kununua
 
Unaelewa maana ya tuhuma au huelewi?! Mie nimesema amedanganya au nimesema anatuhumiwa kudanganya?! By the way, kwenye maelezo yake mwenye si amesema amesoma chuo kikuu miaka mitatu!!! We unafikiri maana yake hapo ni nini kama sio kuwadanganya waiofahamu? We unafikiri mtu aliyeishia elimu ya chini akaja kumsikia Mnyika anasema amesoma chuo kikuu miaka 3, unatarajia ataelewa nini?

Wewe ndio malipyoto kabisa, amesema alisoma UDSM miaka mitatu hakusema amegraduate UDSM! Ni kweli kasoma hiyo miaka mitatu na kuahirisha kwa sababu alizozisema, ana uwezo wa kurudi wakati wowote na kumalizia na si kitu kigeni. Ukiweka chuki zako binafsi pembeni utaelewa maana unatawaliwa na chuki dhidi yake, hutaelewa!
 
hongera mnyika kwa majibu yako kwa hao watu ila pia nimerithika na majibu na radhi ya ridhiwani kwa mnyika amejibu kwa utulivu baada ya kupewa ukweli wa elimu ya mnyika. nimependa majibu yake utafikiri hayuko gambani vile (ila ni kijana mwenzetu avutwe kwetu hata kama kuna mamlaka inayomzuia kufanya ivo.....SISI NDIYO NURU YA TAIFA basi na TUWE NURU YAO)
 
Kumbe ni mzee mwenzangu, ngoma draw. Nimekuuliza umewahi kusikia kisa cha Father Kit Cunningham?

Wewe hujasoma seminari

Duuuuh...kumbe nawe umekula mvua za kutosha. Cha ajabu busara zako hazifanani na umri wako, sorry to say so!
 
Back
Top Bottom